Jamani wana jamii forum habari zenu? Kuna mkasa ulinikuta nikikumbuka nacheka sana[emoji2][emoji2].
Jumamosi moja niliamka ikiwa siku njema sana,ila ilipofika jioni mambo ayakuwa sawa,inshu yenyewe ilikuwa ivi,si unajua mishe za mjini hapa katika michakato ya kusaka tonge.
Basi nilitoka zangu home nikiwa na elfu tatu kwa jili ya nauli kwenda kazini na kuludi pamoja na kula,basi uko bajeti ilivulugika nikajikuta nimetumia hadi pesa ya nauli ya kuludia,basi jioni ilipo fika si nikagongea nauli kwa mwana basi mwana akanambia nimsubili kidogo basi jamaa alipo kuja akanifinyia noto lakini ela yenyewe alivo nipa alinipa kwa style ya kama tuna shake ands basi alivo nipa nikaitia mfukoni kwa fraha tele nikijua mambo ni [emoji106]sawa.
Basi nilivyo fika kwenye daladala nikakaa siti karibu na mrembo frani hivi,ilivyo fika mda wa kutoa nauli si nikatoa ile noti bwana bwana kumbe noti yenyewe kipande yaani ilikuwa imechanika imebaki kipande nilijuta kuzaliwa basi kama mnavyo wajua makonda na tabia zao alinikazia hadi ikawa noma mwisho wa siku mrembo akani save,tokea pale nilikaa kimya kama nimenyeshewa mvua.
Kwaiyo jamani tukipewa pesa na mhuni tuwe tunachunguza[emoji113][emoji113][emoji113]