Bwana Wake Anaitwa Mr.Raymond Nyamwihula Ambaye na Yeye Pia Ni Mtangazi na Mwandishi Wa Habari Mwandamizi wa Star Tv na Alikuwa Ni Chief Bureau wa Star Tv Jijini A Town ila Kwa Kuwa ana Wivu Kwa Shem Ivona Kamuntu Jamaa Kalazimisha hadi Amerudishwa Sasa Jijini Mwanza ili Aweze Kuwa Karibu na Mke Wake. Namkumbuka Sana Huyu Kaka Raymond Kwani Ndiyo Alinisaidia hata Kupata Hostel Nzuri na Ya Haraka Pale SAUT Mwanza na Ni Hostel Ya Watukutu ila Wenye Akili Darasani na Iliyokuwa Chini Ya Wakatoliki Inaitwa Hostel Ya DARFUR. Vitimbi Vya ktk Hostel Hiyo Asikusimulie Mtu na Maasi Yote Ya SAUT Yalikuwa Yanaanzia ktk Hostel Hiyo na Hata Poti Wangu na Comrade Wangu Mwenyekiti wa BAVICHA Mheshimiwa John Heche Pamoja na Ubabe Wake na Ushawishi Wake Mkubwa Pale Chuoni Kipindi Chetu cha Mwaka 2006 hadi 2009 Tulipomaliza Yeye Akiwa Anachukuwa BAED na Mimi BAMC Alikuwa Anaiogopa Sana Hostel Yetu Ya DARFUR na Watu Wake. Japo Ninapishana Nae ktk Itikadi Ya Siasa ila Nisiwe Mchoyo Wa Fadhila na Pongezi na Wala Nisiwe Mnafiki John Heche Yupo Vizuri, Anajiamini na Anaweza Kukitetea Anachokiamini na Ana Ushawishi Mkubwa Sana na Sishangai Kuwa Alisoma Chuo Kizuri na Bora cha SAUT na Najua Makamu Mkuu wa Chuo Aliyemaliza Muda Wake Dr.Fr. Charles Kitima na Wahadhari Wote wa SAUT Wanajivunia Sana John Heche ila Najipanga Sasa Kumshawishi Ahamie Chama Chetu cha Mtaa Wa LUMUMBA Kwani Anahitajika Mno na Patamfaa Sana na Pia Nataka Nimshawishi Aache Kushabikia Timu Mbovu Ambayo Leo Inafungwa na Ruvu Shooting Taifa Na Wiki Ijayo Inakwenda Kufungwa Magoli Idadi Ya Siku Za Wiki ( Juma ) hapa Dar es Salaam na Waarabu Waliochukua Kombe La Super Cup Majuzi.