Dada Maria Sarungi Watanzania tunajuana kwa Mambo yetu, ila hatujafikia Kuhatarishiana Usalama pale tunapopatwa na Misiba. Umekosea sana Dada..!!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mwanaharakati Maria Sarungi ambaye ni Mtoto wa marehemu Prof. Philemon Sarungi amesema miongoni mwa sababu iliyomfanya kushindwa kuhudhuria mazishi ya baba yake ni pamoja na Suala zima la Usalama wake.

Maria amesema hayo leo Machi 10, 2025 wakati alipotoa salaam kwa njia ya mtandao wakati wa ibada ya kuaga Mwili wa baba yake Marehemu Prof.Philemon Sarungi ambaye alifariki Dunia Machi 05, 2025 nyumbani kwake Osterbay Jijini Dar es Salaam kufuatia Maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua.
@mariastsehai

Chanzo: manaratv

Hivi Dada Maria Sarungi unataka kusema wakikutaka Kweli watakukosa? Nakubali IQ yako ila Siku hizi Sikuelewi Dada Ok?
 
Hapana chezea hii nchi aisee
 


TANGU LINI MWANAMKE AKAMUELEWA MWANAMKE MWENZIE?
 
Kudakwa kila mtu anawezwa kudakwa na maadui zake kirahisi ila sio kirahi kivile kama unadaka kumbikumbi huo utakuwa ni uzembe kuhatarisha usalama wako wakati una sense danger
 
kumekucha.
 
Kama mimi ningekuwa na mamlaka makubwa na amenipa makavu sana tu ningemtangazia aje ashiriki mazishi ya baba yake sitamkamata. Kwangu hana tishio wala hawezi kunipindua. Naacha anitukane tani yake wala sitashughulika naye
 
Ni ishara kwamba hapoi na hana suluhu na fisiemu
 
Ushukuru wewe unatumia ID hawawezi kukutafuta humu unawo wakwaza.Siku wakikujua watakufata huko huko msibani
 
Rudi kwenye uhalisia wako Acha kuigiza. Wewe si mgeni wa matendo ya vyombo vya Dola vya nchi hii. Huwa havitaki kazi ngumu lakini ukijifanya soft target wanakupoteza. Unayemuongelea amenusurika miezi michache tu iliyopita na wengine mkaungana na watesi wake kusema amejiteka.
 
refer case study ya chahali usijitoe ufahamu.
 
Umesahau juzijuzi alitekwa na kunusurika. Sasa si kujipeleka ktk domo la mamba kama angehudhuria mazishi? Maisha yamebadilika sana. Watu wanaishi kwa tahadhari toka utekaji umeanza.
 
Ukitaka kujua chuki imetamalaki juu ya Maria basi jiulize ni sababu zipi zinasababisha Rais hajatuma salamu za rambirambi kwa familia ya prof. Sarungi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…