Dada wa kazi alipobugia shaving cream ya madam wake

Dada wa kazi alipobugia shaving cream ya madam wake

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ilitokea huku kwetu Kwatogole, dada wa kazi kwenye familia ya mume mke na mtoto wa kike wa miaka miwili. Siku ya kwanza mtoto alikua analia baada ya kula, mama alitoa ki tub kidogo cha ice cream alimpa dada alimshe mtoto. Dada alionja kidogo aliipenda na kuwaza kuchwani hawa watu wanakula vitamu.

Siku ya pili ilikua weekend, mama ameamka hakutaka kuwasumbua mume na mtoto wake chumbani, alifika sebuleni akaanza kupaha shaving cream makwapani, mara mtoto alianza kulia, alikimbia chumbani kumchukua mtoto aliporudi alimkuta dada ana kamua shaving cream mdomoni.

Mama alipiga kelele na kupata msaada na mume na majirani walitokea. Ilibidi dada apelekwe zahanati kwa huduma ya kwanza.

Tangu ile siku kila alichoona ni kigeni kwake hakula mpaka apewe uhakika na wenyeji wake kuwa anaweza kula.
 
Siwezi kusema ni mshamba bali ni ugeni wa hivyo vitu kutokana na utamaduni wa vyakula alivyozoea huko kigoma. Hata mimi siku nilipoona mayonaizi inatumika kwenye vyakula kama chipsi nilihisi ni shawaha za wanaume kumbe I was wrong
 
Hadi sasa najaribu kukumbuka ni wapi nishawahi kuona ice cream ya kwenye tube like toothpaste...🤔🤔🤔
 
Hadi sasa najaribu kukumbuka ni wapi nishawahi kuona ice cream ya kwenye tube like toothpaste...🤔🤔🤔
1656403426255.png
 
😆😆😆😂😂😂🤣🤣🤣🚬🚬🚬🏃🏾🏃🏾🏃🏾
 
Back
Top Bottom