Dada wa kazi aliposababisha mtoto wa boss kupata utapiamlo

Dada wa kazi aliposababisha mtoto wa boss kupata utapiamlo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Rachael alipata kazi katika shirika la kimataifa, akiwa pale alikutana na James kijana kutoka Cameroon, wakaka wa Cameroon wako very romantic, Rachael alijikuta ameingia mazima. Walipata mtoto na baada ya hapo James alipata uhamisho kwenda Angola. Kama aliomba uhamisho ule ni siri yake lakini James hakuonyesha commitment yeyote kwa Rachael.

Rachael akiwa haamini, bado alikumbuka zile romantic weekends Saadan na Matema Beach. Alifunga safari kumfuata James Angola, huko alipigwa tukio aliporudi alielewa kuwa yeye ni singel mother. Alielekeza mapenzi yote kwa mtoto wake.

Pale kazini kulikua na Day Care kwa watoto wafanyakazi. Ilikuwa na viwango bora na walichukua watoto kuanzia miezi mitatu. Wakati Rachael anarudi kazini mtoto wake alikua na miezi sita. Asubuhi alimuacha Day Care na jioni walirudi wote nyumbani.

Maisha yalikua mazuri tu mpaka pale Rachael alipoomba nafasi ya kwenda kusoma shahada ya uzamili nje ya nchi. Mama yake Rachael alikua bado katika safari ya kupona baada ya kupata kiharusi na baba alisha aga dunia. Rachael alitafuta dada wa kazi, kwakweli hakuwa na muda mrefu wa maandalizi na dada hakupatikana kirahisi.

Rachel akiwa amekata tamaa kufikia kutakua kuairisha safari, alimpata dada aliyekuwa anafanya kazi kwa mchungaji wao kanisani, aliacha kazi baada ya kubeba ujauzito na sasa yeye na mwanae hawana makazi maalum. Rachael aliona wote wanamatatizo yanaweza kusaidiana. Alimkaribisha kwake na walianza maisha. Mtoto aliacha kumpeleka Day Care kwani hakukua na utaratibu wa uhakika kumpeleka kila siku.

Kabla Rachael hajaondoka aliongea na mwenye butcher ya nyama, awe anapeleka nyumbani kwake nyama kilo mbili J5 na J’mosi. Alilipa bill ya maziwa mwenyewe na dada alimuacha pesa ya mambo mengine.

Yule dada alivyokuwa na akili kisoda, mtoto wake alimpa uji wa maziwa na sukari na mtoto wa Rachael alimpa uji bila maziwa wala sukari. Katoto kalikunywa kwa njaa. Alimpa mtoto wake mtori mtoto wa Rachael alimpa ugali na bamia la mlenda.

Rachael alirudi ili afanye utafiti na kukuta mtoto wake ana utapia mlo, hana nguvu hata za kukimbia. Rachael alilia sana, hasa kumuona mtoto wa dada shavu dodo. Alimuomba kwa kumwambia ninaingia chumbani kwenda kuoga nikitoka nisikukute.

Rachael alipata dada kutoka kijijini kwao na safari hii aliishi na mama yake Rachael. Rachael hakuwa na muda mrefu wa kumaliza masomo baada ya kukamilisha utafiti wake.
 
Masikini wengi tunaroho mbaya na ndio maana hatutoboi. Nina mfano hai hawa wamama wanaouza matunda wakiingia mashambani wanawanyonya wamama wenzao shambani na kupata bidhaa kwa bei ya dhulma ili wapate faida kubwa ila hakuna wanachofanikiwa sababu ya dhulma wanazofanya.
 
Back
Top Bottom