Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Habari wakuu,
Kumekua na hii tabia inayokuwa kwa kasi inayofanywa na wadada wanaofanya kazi za nyumbani. Tabia ambayo imegharimu na inaendelea kuwagharimu watu, hivyo wanajamvi muwe makini na watu hawa mnaowachukua kwa lengo la kusaidia kazi za nyumbani.
Iko hivi, utakuwa na uhitaji wa kupata mtu wa kusaidia kazi hapo nyumbani, utatafuta huku na huko utapata mtu, utaambiwa mtu kapatikana sehemu fulani, utatuma nauli muhusika anafika. Baada ya muda fulani kati ya wiki hadi mwezi mmoja yule binti anaiba hapo nyumbani kwako chochote kitakachokuwa karibu (hasa pesa, sababu atakuwa ameshasoma mchezo wote hapo nyumbani na anajua hela zinakaa wapi) na kuondoka kurudi kwao.
Wewe baada ya kuibiwa utapiga simu kwa wazazi au walezi wake na kuwapa taarifa kwamba binti yao amekuibia kiasi kadhaa na ametoroka kurudi kwao unataka vitu vilivyoiba virudishwe, hapa ndipo meza inapogeuzwa.
Wazazi watakwambia kwanza mtoto wao hajafika nyumbani hivyo hiyo kesi ipo kwako, halafu umemtorosha mtoto wao wakati bado ni mwanafunzi. Wewe utaogopa kuwa na kesi ya kumtorosha na kumkatisha masomo binti yule hivyo unakaa kimya yaishe, huku nyuma mpango wao umefanikiwa wanatafuta mtu mwingine wa kumuingiza mjini.
Kuna ambaye alijiongeza akapiga simu kwa majarini ambapo alimchukua binti huyo na kuambiwa kuwa binti ameshafika nyumbani. Baada ya kutoa mikwara miwili mitatu pesa alizoiba huyo binti zikarudishwa kwa muhusika.
Hivyo watu muwe makini na mnapopata wadada hawa wa kazi, wengine wanakuja na mikakati yao kabambe wakishirikiana na wazazi/walezi wao, wanasubiri atakayejitokeza wamuingize mkenge.