KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Poleni sana kwa kadhia hiyo, pamoja na kujitahidi kuweka kila tukio wazi lakini kuna baadhi ya taarifa haukupaswa kuzianika hadharani kwa ajili ya kumsitiri marehemu kutokana na matatizo aliyokuwa nayo, anyway inawezekana ni kwa kutokujua ndio maana imetokea hivyo. Niwape pole sana watani wenzangu kina Mbaga na Mwenyenzi Mungu amrehemu dada yetu.
 
Hospitali zetu kulipishwa bila kupewa huduma husika ni jambo la kawaida, serikali inataka pesa za kununua sare za suti za watumishi kwa ajili ya kampeni.
 
Pole sana tena sana Mungu atakulipia kwa hili, kwa jinsi ulivyolielezea hili wewe ni muungwana sana na nia yako kulinda wengine ya Dada umeyakubali. Natamani muhusika mmoja apite hapa na aone huu uzi ili wafanye kitu kurekebisha haya mambo japo tunajuwa kuna madudu mengi sana kwenye Hospital zetu.
 
Wajinga kama wewe bado ni wengi sana nchi hii..

Sasa kama kifo ni mpango wa Mungu hospitali tunazo za nini, si tuache tu watu waugue wafe kwa sababu ni mipango ya Mungu?
 
Tatizo baba yake hakua kiongozi mkubwa CCM, huenda naye angekuwa waziri na wasingeanza kumlipisha kabla ya huduma.
 
Mkuu pole sana kwa kufiwa na dada yako lakini mkiambiwa kuwa mujaribu na kutumia Dawa za Asili kutibu maradhi sugu kama hayo ya Saratani Ukimwi Hepatiti B Virus maradhi ya kisukari na maradhi Presha munadharau dawa za asili maradhi hayo niliuyoyataja hakuna dawa Yoyote ya Hospitali itakayoweza kutibu na kuponyesha mgonjwa. Ukimpeleka mgonjwa Hospitali akiwa na hayo maradhi ujuwe unampeleka kwenda kwenye kifo kwani hataweza kupona kwa dawa za Hospitali sio rahisi kabisa.Pole sana na uguwa pole kwa kumkosa Dada yetu RIP.
 
Hospitali zetu kulipishwa bila kupewa huduma husika ni jambo la kawaida, serikali inataka pesa za kununua sare za suti za watumishi kwa ajili ya kampeni.
Tatizo mawasiliano unakuta daktari yeye hahusiki na vitanda Wala sehemu ya kugawa dawa wala sehemu Hizo za huduma nyingine ziwe maabara nk

Yeye akiona mgonjwa amemwandikia kuwa akalazwe n wapi atalazwa sio KAZI Yake hao walazaji ndio watajua kama watamlaza kwenye bodaboda au mtaroni au kwenye daladala haimhusu na pia kabla kulazwa inatakiwa kulipia Kwanza daktari akiandika ulazwe .Mpokea malipo sio daktari na hahusiki na kulaza MTU yeye hupokea malipo Tu akishapokea ndipo huota go ahead uende huko Kwa walazaji wajue wakulaze wapi

Sasa na wao wakipokea ndipo huanza kuhaha watamlaza wapi Hilo halihusu madaktari wala Mpokea pesa NI wao watafute pa kulaza

Hospital a serikali kuna urasimi na NI.pasua kichwa hawaruhusu MTU mmoja kufanya majukumu yote.au kuwa na information zote na kufanya maamuzi
Hapo

Pia hiyo mitungi ya gesi sio KAZI ya manesi kujaza wao huhusika Tu kuwekea Tu mgonjwa .Wanaojaza oxygen wengine

Ukiumwa NI.kukazana kuomba Mungu Sana tu pia badala Tu ya kuwa na Imani kubwa Sana Kwa hospital Tu

Msione watu wanajazana Kwa Mwamposya kuna maneno msije ona wajinga au wamechanganyikiwa
 
Poleni sana ila mgonjwa wenu alikufa natural death kwahiyo hapo ulipoandika siku zake zilikuwa zimefika pigia mstari saratani sio ugonjwa mdogo ujue na inawezekana ilikuwa ishafika mpaka kwenye mapafu huko.
Hakuna mtu ambaye hatonja mauti. Tunapokwenda hospitali tunategemea hospatali kutusaidia kuahirisha vifo vyetu. Iwapo hospitali inarahisisha kifo badala ya kuahirisha kifo basi hospitali hiyo ina tatizo.
 
Nimeshindwa kuelewa komenti yako, hata hivyo wodi zote zina uongozi wake wanaotoa taarifa kama zimejaa au vipi, nawapokea malipo hutakiwa kujua wodi gani ina kitanda na mgojwa huanza kupokelewa wodini ndipo unalipia kitanda ambacho hata hivyo ni aghari kuliko hotelini! No breakfast, no AC, no hot water, no clean bedsheets, no private nurse and most of all no no no ni dhuluma tu.
 
Hakuna mtu ambaye hatonja mauti. Tunapokwenda hospitali tunategemea hospatali kutusaidia kuahirisha vifo vyetu. Iwapo hospitali inarahisisha kifo badala ya kuahirisha kifo basi hospitali hiyo ina tatizo.
Hospital huwa wanaahirisha kifo sidhani.Hospitali NI wakweli Sana ndio maana huwa kuna mortuary wamejenga hospitalini kuwa mwenye macho haambiwi tazama kuwa MTU akikanyaga hospitali ajue kuna mawili kupona au kuishia kwenye jengo la mortuary analiliona hawafanyi Siri jengo liko wazi kama yalivyo majengo ya madaktari ,maabara,wodi nk
 
Very serious note.
Uzembe tu hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…