KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu Pole sana kwa Msiba.Tafdhali Ondoa Hizi Taarifa binafsi za marehemu Dada huku Mtandaoni.Pamoja na kwamba amefariki bado anastahili Faragha.

Pili Kwa mujibu wa mealezo yako hapo kunaweza kuwa na Kesi ila sifahamu kwa mujibu wa sheria za Tanzania Uwajibikaji wa Madaktari(Professional Malpractice) Ikoje.Mfano eneo la Fidia,etc.


All in all Fuatilia Kwa Ukaribu zaidi na Mungu awape Nguvu katika kipindi hichi kigumu.Apumzike kwa amani DADA Lilian
 
Basi huelewi lengo la tiba ni nini.

In fact hosptiali za nchi nyingi, kwa mfano marakeni hazina mortuary
 
Saratarani

Poleni sana kwa mgonjwa,

Saratani ya kinywa cha mdomo ina changamoto kubwa ikiwa imesambaa ktk mfumo wa pua na mdomo, kichwa, koo kwa ajili ya kuvuta pumzi ya uhai Oxygen. Kinga ndogo chini ya CD4 24, tiba ya miozi chemotherapy katika stage ya ugonjwa ilipofika ripoti inaonesha haitakuwa na manufaa yoyote.

Ilitakiwa madaktari wawapeni ndugu taarifa ya ukweli ya hali ya mgonjwa na ushauri nasaha / counselling kuwa mgonjwa amefikia hali ya mwisho wa uhai hivyo kupatiwa madawa ya kupunguza maumivu na mateso kwa kuwa hauna uwezekano wa kuponyeshwa ugonjwa ukiliomkuba Palliative care /for end of Life.

Hard palate cancer is a rare cancer that forms on the roof of your mouth.
 
Mortuary Marekani hata hapo Kenya nyingi NI private business zinaitwa funeral homes unafia hospital unapelekwahuko ukalipie private huko funeral homes
Siyo sehemu ya hospitali; zinapokea maiti kutoka popote pale kwa ajili ya matunzo ya mwisho kabla ya mazishi. Haina maana kuwa kwenda hospitali ni kwenda kufa na hivyo mortuarym iwepo pale pale kama sehemu ya hospitali.
 
Inaanzia kwenye mifumo ya nchi tu jinsi inavyoendeshwa ndivyo taasisi zote zinavyoreflect. Kiufupi hivi sasa ukipata shida yeyote inayokulazimu kwenda taasisi yoyote ya umma tegemea huduma ya hovyo tu.
 
Jf malalamiko mengi kama haya tunaletanayaficha hamtoi,mimi ndugu yangu mwezi wa 3 huu amelipia vifaa vya matibabu ya Gastro lakini tunaambiwa vimekwisha ma mzabuni hajaleta vingineara mzabuni kaleta vifaa vilivyochini ya kiwango madokta wamevigomea,nililets maandiko humu hamkujali wala kuyatoa mkayakalia,haya hili kwanini hsmkulikalia??
 
Wanaochukua pesa wanawajibika kujua kama vyumba vipo au hakuna, manesi hata kama hawajazi lakini wanatakiwa kujua kama tank lina Oxygen kiasi gani na mgonjwa anapata ya kutosha, ni uzembe tuu hakuna excuse yeyote
 
Ungekwenda Mwananyamala Hospital Emegeny,ile hospital,wagonjwa wanashughulikiwa sana ,ikitokea kafariki,unajuwa wazi,-huyu wakati wake umefika.Uongozi na wafanyakazi wa Mwananyamala hospital,wanajitahidi sana.
 
Nafikiri kilichokosekana hapo ni 'Proper Counseling ' tu. Mgonjwa anaonekana alikuwa kwenye terminal illness, hata ORCI wameamua kumpeleka kwingine hawataki 'Death' nyingi zitokee kwao.

Lakini, ndugu yako alijuaje Oksijeni imekata? What if mgonjwa alianza kupoteza maisha kabla ya hiyo Oksijeni kukata?

Yote kwa yote, Pole sana komredi kumpoteza dada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…