KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ungekwenda Mwananyamala Hospital Emegeny,ile hospital,wagonjwa wanashughulikiwa sana ,ikitokea kafariki,unajuwa wazi,-huyu wakati wake umefika.Uongozi na wafanyakazi wa Mwananyamala hospital,wanajitahidi sana.
Ni kweli kabisa wanafanya kazi vizuri,ila ukitaka huduma nzuri zaidi penyeza rupia kiduchu tu utapewa first aid class 1.
 
Pole mkuu,
Hii nchi kila kona ni uzembe, tena wa maksudi, UWAJIBIKAJI ni tatizo kubwa sana nchini mwetu, ndio maana hata mashirika yetu yanakufa kufa kizembe.. Mtu anajifanyia ili mradi tu, si kutoka moyoni, sasa sijui kisa malipo madogo au watanzania tu sasa hivi roho zetu zishabadilika rangi, si madaktari, si polisi, si umkute mtu kwenye kimeza chake ofisini, utasikilizwa(kuhudumiwa) vizuri ukitanguliza fedha.
 
Duh sad
 

Surah Al-Baqarah 2:195

"Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema; hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema."

Aya hii inakemea vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha maangamizo au madhara, ambayo yanaweza kujumuisha uzembe katika kutoa huduma za afya. Watoa huduma za afya wanapaswa kuepuka uzembe ili wasiwe chanzo cha maangamizo au madhara kwa wagonjwa wao.

3. Surah An-Nisa 4:58

"Hakika Mwenyezi Mungu anakwambieni mzikabidhi amana kwa wenyewe; na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu."

Sekta ya afya inahusisha amana kubwa ya maisha na afya za watu. Kwa hiyo, watoa huduma za afya wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa uaminifu na uadilifu. Uzembe ni kinyume na kuhifadhi amana hizi.

4. Surah Al-Isra 17:70

"Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tumewapa vya kupanda katika nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza zaidi kuliko wengi katika tuliowaumba kwa utukufu ulio mkuu."

HAWA WATU WACHUKULIWE HATUA STAHIKI.
 
Poleni sana ila mgonjwa wenu alikufa natural death kwahiyo hapo ulipoandika siku zake zilikuwa zimefika pigia mstari saratani sio ugonjwa mdogo ujue na inawezekana ilikuwa ishafika mpaka kwenye mapafu huko.
Natural death Kivipi mkuu? Huyo Dada kafa mapema kwa kukosa /kunyimwa oxygen. Umeambiwa Nurse alitoa tahadhari kuwa fanya haraka oxygen in aisha, na kweli kufika Mbezi ikakata. Hiyo inaiita natural death? Really?
 
Pole sana, yawezekana mgonjwa wako alihudumiwa na mwanafunzi wa udaktari au walikuomba chochote ukakakataa
 
Poleni sana. Bado nasisistiza: hii nchi bila raia kujua wajibu wao wa kuhakikisha tunapata viongozi wawajibikaji na kuwasimamia tusitegemee mazuri. Kla mtu atakumbukana na madhara ya CCM kwa wakati wake. Na Samia pamoja na uozo wake wote ameshasema yuko kwenye madaraka mpaka 2030 ndiyo anarudi Kisimkazi. Utadhani ana mkataba na Mungu.
 
Inaanzia kwenye mifumo ya nchi tu jinsi inavyoendeshwa ndivyo taasisi zote zinavyoreflect. Kiufupi hivi sasa ukipata shida yeyote inayokulazimu kwenda taasisi yoyote ya umma tegemea huduma ya hovyo tu.
Kweli kabisa Ndugu yangu
 
I feel your pain. Pole sana. Kuna baadhi ya watu ni wazembe sana pale Muhimbili.
 
Haya yote yapo covered kwenye sheria ya fidia. Law of Torts. Akiweza ku establish duty kwa wale wazembe baas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…