KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna kitu walijua wamebugi waliamua asifie kwenye jukwaa lao.
Wanakomalia hela na wana tabia ya kuzidisha namba katika ada Kama sio kukulundikia Dawa zisizo tija ili wakupige mshiko.
 
Maxence Melo Moderator
Tafadhali sana tumsitiri marehemu kwa kuondoa hizo documents za hospitali.
Naona mfiwa amepata taharuki iliyompelekea kuexpose taarifa za mgonjwa.
...
Mleta mada kipo kitengo cha kupokea malalamiko hapo muhimbili sio busara kuachama taarifa za dada yako namna hii.(kama ni dada yako kweli)

All in All pole kwa kufiwa...
 
Maxence Melo Moderator
Tafadhali sana tumsitiri marehemu kwa kuondoa hizo documents za hospitali.
Naona mfiwa amepata taharuki iliyompelekea kuexpose taarifa za mgonjwa.
...
Mleta mada kipo kitengo cha kupokea malalamiko hapo muhimbili sio busara kuachama taarifa za dada yako namna hii.

All in All pole kwa kufiwa...
Yaani dah' Diagnosis nje kabisaaa
 
Hata kama saratani ilikuwa ni hatua mbaya sana,njia iliyotumika kumondoa marehemu ni ya kikatili sana,hakuna kitanda,wakati hela ilishatolewa,vipi kuhusu swala la Oxygen nalo kwanini isiwekwe ya kutosha...
Kwenye oxygen hapo wamezingua sana na je kama vitanda vimeisha wangefanyaje?
 
Rushwa kila sehemu, wiki mbili zilizopita kuna binti wa miaka 7 kabakwa na kulawitiwa na kijana wa miaka 17, mitaa ya kiwalani kufika polisi sasa wazazi wa binti ndo km wabakaji ni vitisho tu, ikabidi atafutwe aliyekuwa mkuu wa kituo buguruni ndipo sasa wakaanza kutoa ushirikiano, bila kufahamiana na huyo mkuu wa kituo kesi ilikuwa iwageukie wazazi mwathiriwa, hapo nchi ndipo ilipofikia kiufupi nchi imeoza na inanuka uvundo maza yupo zake kuzurula hajali chochote
 
Mwingine kalalamika ndugu yake kafia kituo cha afya kimara kwa uzembe wa aina hii. Nchi imeoza.
hapo hapo unasikia mwenezi ananzunguka kusimamia ilani mara mama atatuvusha mara ccm mbele kwa mbele nchi inanmambo hii ila uzembe umezidi
 
Pole sana mkuu. Uvumilivu, subira na nguvu visipungue kwako kipindi chote hiki.
 
Duh Pole sana Ndugu yangu, Mimi juzi nusura tumpoteze Ndugu yangu pale MOI, alipata Ajali Tanga, akapelekwa hospital ikaonekana ni issue KUBWA, tukaomba referral kuja MOI. Wakaondoka Tanga kuja MOI wakafika saa nne usiku, tukapokelewa, mgonjwa hakua na jeraha kwa nje ila alilalamika maumivu Sana, saa SITA na nusu usiku akafanyiwa vipimo.

Vichekesho vikaanza, mgonjwa wa referral akapewa majibu kuwa hajaumia yuko poa hayo ni maumivu Tu, tukaandikiwa dawa tukaruhusiwa tukiwa tumembeba mgonjwa wetu. Analia maumivu makali sana.

Asubuhi mgonjwa hali ikawa mbaya zaidi ikabidi tumpeleke hospital Fulani pale TEGETA akafanyiwa MRI ikaonekana ana internal bleeding na tayari mwili ulikua ushaanza ku-react, yaani damu inaisha na anahisi tumbo kuvimba na kushindwa kupumua.

Ikabidi tukubaliane afanyiwe emergency operation kuanzia saa Saba mchana Hadi saa mbili usiku, wakamtoa bandama, ndio ilikua imeumia na kupelekea damu nyingi sana kuvujia Ndani, walitoa damu 2ltrs.

Hayo ndio yaliyotukuta MOI yaani tungerelax tukamuamini yule Dr Leo Hii ningekua msibani.

Poleni Sana Ndugu zangu
Duh! Poleni
 
Pole sana mkuu. Tunaomba Wizara husika na uongozi wa serikali ujitokeze kutoa ufafanuzi juu ya suala hili ikiwezekana wahusika wachukuliwe hatua.
 
Daah! Poleni sana lakini mngeenda mamlaka husika hapo Muhimbili na kuwasilisha malalamiko yenu na hao wahusika kama ingebainika kweli walifanya uzembe hadi kifo kutokea wangewajibishwa.
Kwamba wafanyakazi wa hiyo mamlaka hapo muhimbili hawajuani na hao wafanyakazi wa muhimbili?..hiyo siyo kesi ya nyani kumpelekea ngedere!?..watu wawajibishwe aisee,watu wa kada ya afya hawajali maisha ya mtu,hawaogopi kifo cha mtu
 
Bora mgonjwa angebaki Hindu Mandal huenda angepatiwa matibabu sahihi,

Muhimbili sijawahi kuiaminii hata, tena huko Mloganzira ndo kituo cha vifo hapoo.

Duuuh poleee sana kwa msibaa, [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom