KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nchi ingeanzisha university teaching hospital ili adactari na manesi wawe na viwango vya juu vya kitoa huduma. Vyuo vilivyopo vinatoa madactari n manesi waso na viwango.
 
Pia watu wasidharau hospital za mikoa na rufaa maana ndoo zinazotoa rufaa chapu kwenda mhimbili
sahihi ,unampaje mtu rufaa ameisha apewe rufaa akiwa bado ananguvu kiasi Cha kujitegemea

Ocean road waliomweka mgonjwa anazidiwa hawalaumiwi wanalaumiwa hospitali nyingine ambayo hatamgonjwa haijamshughulikia
 
Nilikuwa na mgonjwa wangu ambaye alikuwa anasumbuliwa na Saratarani, alikuwa anapatiwa huduma Ocean Road, tukiwa hapo tukapata referral ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga), Dar es Salaam.

Wakati tunaelekea Muhimbili tukapita Hindu Mandal kwa kuwa kuna Daktari ambaye pia tulihitaji kumuona, wakati tukiwa hapo tukapata huduma nzuri tu ya muda.

Tukapatiwa Ambulance iliyotupeleka hadi Muhimbili, wakampokea vizuri mgonjwa na kumpa huduma mbalimbali.

Muda mfupi baadaye wakatuambia kuwa tunatakiwa kulipia chumba kwa gharama ya Shilingi 50,000, pale Mwaisela, huku akiwa anaendelea kupatiwa matibabu ikiwemo kupewa Oxygen kwa kuwa mgonjwa alionakana ana shida ya kupumua.

Baada ya kulipa, wakatuambia hakuna vitanda hivyo wanataka kutupeleka Hospitali ya Mloganzila.

View attachment 3065740

Sisi tukakataa, muda huo ni saa kumi alfajiri, tukawambia tunaomba kama kweli hakuna kitanda basi mgonjwa abaki pale ‘Emergency’ hadi asubuhi kwa kuwa tayari tulishalipia chumba na kuanza kuangaika n ambulance kuelekea Mloganzila wakati tumeshafanya vipimo na taratibu nyingine itakuwa ni usumbufu na pia sio njema kwa mgonjwa.

Ukatokea ubishani pale, sisi tukakataa, lakini Madaktari wa Muhimbili waliokuwepo wakafanya maamuzi ya kibabe wakasema mgonjwa wetu Lilian anaingizwa kwenye Ambulance kupelekwa Mkoganzila.

Wakati wakifnya maamuzi hayo, kuna Nesi mmoja akasema “fanyeni haraka Oxygen inaisha”.

Walipofika Kimara, ndugu yetu aliyekuwa kwenye Ambulance akanijulisha kuwa Oxygen imekata, hadi wanafika Mbezi tayari Oxygen ilikuwa imeshakata na mgonjwa wangu akafariki.

Inawezekana ni siku yake ilikuwa imewadia lakini kilichotokea ni uzembe wa baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili na watendaji wengine kadhaa waliokuwepo.

Kwanza najiuliza kwanini walitulipisha kitanda wakijua hakuna kitanda, pili kwanini walimwekea mgonjwa Oxygen kidogo na kwa kauli iliyotolewa pale ni wazi walijua hiyo haitamfikisha Mgonjwa Mloganzila.

Tatu kulikuwa na haja gani ya kumpeleka Mloganzila wakati tayari kulikuwa kunaelekea kukucha na mmoja wa Madaktari aliwaambia wenzake tubaki pale lakini wenzake hawakumsikiliza.
View attachment 3065743
Ambulance iliyombeba dada yangu.
Baada ya msiba nilipouliza mmoja wa Madaktari wa Muhimbili kwanini walitupa Oxygen kidogo anadai lile lilikuwa jukumu la watu wa Ambulance kukagua na sio jukumu lao.

Walichokifanya Madaktari hao wa Muhimbli waliokuwa zamu Usiku wa tukio hakikuwa cha kibinadamu na kama wanafanya hivi basi maisha ya watu wengi yapo hatarini.

Kwa nini nimewasilisha malalamiko yangu hapa JamiiForums, nataka Dunia ijue kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Muhimbili wanatakiwa kujirekebisha, najua roho ya dada yanu haiwezi kurudi ila basi angalau wasingetuonesha wazi kuwa wanataka ndugu yetu afe, pia iwe somo kwa wengine wawe makini.
View attachment 3065744
Miamala ya malipo tuliyofanya kabla ya Mgonjwa kulazimishwa kupelekwa Mloganzila
Hospital za serikali za tz ni lango la kifo,nchi ina laana hiyo,madaktari na wauguzi hawana utu hata kidogo, walivyo mazuzu watakuja kukanusha, poleni sana Mungu atawalipia tu
 
Mwingine kalalamika ndugu yake kafia kituo cha afya kimara kwa uzembe wa aina hii. Nchi imeoza.
Kimara ni kwa kipuuzi mno, hizo case ni kawaida pale. Wahudumu wa afya wanapiga soga chumba cha daktari😂 huku kuna mgonjwa serious anataabika.
 
Nafikiri kilichokosekana hapo ni 'Proper Counseling ' tu. Mgonjwa anaonekana alikuwa kwenye terminal illness, hata ORCI wameamua kumpeleka kwingine hawataki 'Death' nyingi zitokee kwao.

Lakini, ndugu yako alijuaje Oksijeni imekata? What if mgonjwa alianza kupoteza maisha kabla ya hiyo Oksijeni kukata?

Yote kwa yote, Pole sana komredi kumpoteza dada.
Nachokiona tu ni kuwa ukiona Mgonjwa wako anatolewa muhimbili na kupelekwa Mloganzila mara nyingi anakuwa kwenye terminal stage. Ikiwa atapona basi jua ni miujiza ya Mungu tu. Ila mara nyingi watu wanaokuwa directed Mloganzila huwa hawatoboi.

Nina aunt yangu alipigwa stroke ya kichwani mishipa ika burst na kusambaa damu kichwani. It took about four days akiwa Mloganzila before death took charge.
 
Kwahio tukiambiwa mgonjwa anahamishiwa Mloganzira tuanze kuandaa maturubai?
 
Daktari wa Muhimbili anamuona Askari Polisi mla rushwa tena mzembe, Anamuona pia Mkatisha Tiketi wa SGR kuwa naye ni janja janja tu, Askari Polisi Anamuona Daktari mzembe tu, Mkatisha Tiketi naye Anamuona Daktari mzembe mzembe tu, pia watu wanaolalamika kwenye huu Uzi nao kwenye nafasi zao wanakula rushwa pia ni wazembe tu.
Siku Kila mtu akiwa mwaminifu kwenye kazi yake au nafasi yake aliyopewa basi haya malalamiko yatapungua mno au yataisha kabisa.
KILA MTU ATOE HUDUMA KWA UAMINIFU SEHEMU ANAYOFANYIA KAZI.
 
Nilikuwa na mgonjwa wangu ambaye alikuwa anasumbuliwa na Saratarani, alikuwa anapatiwa huduma Ocean Road, tukiwa hapo tukapata referral ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga), Dar es Salaam.

Wakati tunaelekea Muhimbili tukapita Hindu Mandal kwa kuwa kuna Daktari ambaye pia tulihitaji kumuona, wakati tukiwa hapo tukapata huduma nzuri tu ya muda.

Tukapatiwa Ambulance iliyotupeleka hadi Muhimbili, wakampokea vizuri mgonjwa na kumpa huduma mbalimbali.

Muda mfupi baadaye wakatuambia kuwa tunatakiwa kulipia chumba kwa gharama ya Shilingi 50,000, pale Mwaisela, huku akiwa anaendelea kupatiwa matibabu ikiwemo kupewa Oxygen kwa kuwa mgonjwa alionakana ana shida ya kupumua.

Baada ya kulipa, wakatuambia hakuna vitanda hivyo wanataka kutupeleka Hospitali ya Mloganzila.

View attachment 3065740

Sisi tukakataa, muda huo ni saa kumi alfajiri, tukawambia tunaomba kama kweli hakuna kitanda basi mgonjwa abaki pale ‘Emergency’ hadi asubuhi kwa kuwa tayari tulishalipia chumba na kuanza kuangaika n ambulance kuelekea Mloganzila wakati tumeshafanya vipimo na taratibu nyingine itakuwa ni usumbufu na pia sio njema kwa mgonjwa.

Ukatokea ubishani pale, sisi tukakataa, lakini Madaktari wa Muhimbili waliokuwepo wakafanya maamuzi ya kibabe wakasema mgonjwa wetu Lilian anaingizwa kwenye Ambulance kupelekwa Mkoganzila.

Wakati wakifnya maamuzi hayo, kuna Nesi mmoja akasema “fanyeni haraka Oxygen inaisha”.

Walipofika Kimara, ndugu yetu aliyekuwa kwenye Ambulance akanijulisha kuwa Oxygen imekata, hadi wanafika Mbezi tayari Oxygen ilikuwa imeshakata na mgonjwa wangu akafariki.

Inawezekana ni siku yake ilikuwa imewadia lakini kilichotokea ni uzembe wa baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili na watendaji wengine kadhaa waliokuwepo.

Kwanza najiuliza kwanini walitulipisha kitanda wakijua hakuna kitanda, pili kwanini walimwekea mgonjwa Oxygen kidogo na kwa kauli iliyotolewa pale ni wazi walijua hiyo haitamfikisha Mgonjwa Mloganzila.

Tatu kulikuwa na haja gani ya kumpeleka Mloganzila wakati tayari kulikuwa kunaelekea kukucha na mmoja wa Madaktari aliwaambia wenzake tubaki pale lakini wenzake hawakumsikiliza.
View attachment 3065743
Ambulance iliyombeba dada yangu.
Baada ya msiba nilipouliza mmoja wa Madaktari wa Muhimbili kwanini walitupa Oxygen kidogo anadai lile lilikuwa jukumu la watu wa Ambulance kukagua na sio jukumu lao.

Walichokifanya Madaktari hao wa Muhimbli waliokuwa zamu Usiku wa tukio hakikuwa cha kibinadamu na kama wanafanya hivi basi maisha ya watu wengi yapo hatarini.

Kwa nini nimewasilisha malalamiko yangu hapa JamiiForums, nataka Dunia ijue kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Muhimbili wanatakiwa kujirekebisha, najua roho ya dada yanu haiwezi kurudi ila basi angalau wasingetuonesha wazi kuwa wanataka ndugu yetu afe, pia iwe somo kwa wengine wawe makini.
View attachment 3065744
Miamala ya malipo tuliyofanya kabla ya Mgonjwa kulazimishwa kupelekwa Mloganzila
Pole sana mkuu na roho ya marehemu ipumzike kwa amani. Kwa mujibu wa makala yako inaonesha dhahiri wahudumu wa afya wanaohusika na mitungibya oxygen hawakuwa makini kugundua mtungu ujaO wa gesi ni imepungua kukidhi kiwango cha umbali kutoka upanga to mlonganzila pole sana kwa kumpoteza mpendwa wako kwa usembe wa oxygen kama ulivyosema.

Nashahuri siku nyingine fivha taarifa ya mpendwa wako.
 
Bora mgonjwa angebaki Hindu Mandal huenda angepatiwa matibabu sahihi,

Muhimbili sijawahi kuiaminii hata, tena huko Mloganzira ndo kituo cha vifo hapoo.

Duuuh poleee sana kwa msibaa, [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Hata Hindu Mandal ingelekewa wagonjwa wanaopelekwa MLOGANZILA rate ya vifo Ingekuwa kubwa
 
Pole Sana madaktari haogopi kumpoteza ndugu, wazembe sana Hao MNH 2012 nilipoteza ndugu yangu kwa majo tuu yalimuishia
 
Back
Top Bottom