Dada yangu ameniambukiza UKIMWI na hataki tena kunisaidia

Dada yangu ameniambukiza UKIMWI na hataki tena kunisaidia

princewilly

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Posts
259
Reaction score
528
Mimi ni binti wa miaka 23, ni mwanafunzi wa mwaka watatu chuo. Nilikua naishi kwa dada yangu ambaye ndiyo alianza kunisomesha tangu nilipomaliza kidato cha sita baada ya wazazi wangu kufariki. Baada ya kuja kwa dada iniliona tabia mbaya za shemeji, alikua hahudumii chochote, anampiga sana dada na kila kitu anafanya dada, mpaka ada za watoto, shemeji alikuwa akimuomba pesa akikataa anampiga.

Nilikaa nikiwa chuo mwaka wa kwanza mwishoni mwishoni shemeji alikuja kwangu, akaanza kuniambia ni kwanini anampiga dada yangu, alikuwa ananiambia kuwa anamapiga kwakuwa dada yangu ni mkorofi, ana kiburi na ni mchawi anamloga ndiyo maana hafanikiwi. Aliniambia mambo mengi ya dada ambayo yalinifanya ni mchukie dada; akaniambia anataka kutoa pesa lakini dada yangu hataki kwani ni mchawi.

Nilijikuta nakuwa karibu na shemu mpaka tukaanzisha mahusiano, akawa ananipenda ikafikia hatua tunafanya mambo waziwazi. Dada alijua tukawa tunagombana lakini shemeji ndiyo alikuwa ni kila kitu akawa anampiga ananyamaza. Sasa mwaka jana mwezi wa nane nilipata ujauzito, shemeji aliniambia nibebe mimba kwani ananipenda na anataka mtoto na mimi.

Kweli nilibeba mimba, lakini nilipoenda kupima kiliniki nikaambiwa kuwa nimeathirika hivyo nianze kutumia dawa. Nilichanganyikiwa ila nilipomuambia shemeji hakujali. Nilimuambia dada akaishia kuniambia kuwa mbona yeye kaathirika muda tu anatumia dawa shemeji ndiyo aligoma kutumia dawa.

Niliumia sana kwani dada yangu kaniambukiza UKIMWI makusudi, alijua kuwa mume wake anaumwa lakini hakuniambia. Shida nyingine ni kuwa dada yangu kaondoka hapa nyumbani katuachia nyumba mimi na shemeji, nyumba ina jina la dada na ina hati kabisa, shemeji alitaka kuiuza lakini akashindwa, sasa shemeji hana pesa amekua mtu wa hasira.

Kaka natakiwa kulipa ada ya chuo nililipa kidogo lakini sasa hivi shemeji hana pesa na dada ahataki kunilipia na ni mjamzito, nisaidie kaka uongee na dada yangu umuambie kuwa nimejutia kwani sina namna. Kaka yeye ndiyo anatakiwa kunisaidia kwani ni kama yeye ndiyo aliniambukiza, alijua mume wake ana UKIMWI lakini hakuniambia, najua nimemkosea kaka lakini na yeye amenikosea kwani mimi ni mdogo wake, alipaswa kunilinda.

NB: Mnaoishi kwa ndugu zenu tulieni, ukiona mpaka shemeji yako kakutongoza basi jua kuwa huyo ni mshenzi wa washenzi, aisee hivi visa vimekua vingi sana. Najua wakati mwingine ni ngumu kukataa mkishasikia pesa ila jithaminini, hao wanaume ni washenzi, yakiwakuta wanawaacha na aibu halafu hamna kitu, visa hivi ni vingi mpaka basi, aisee mnawakatisha tamaa ndugu zenu kuwasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Niliumia sana, kwani dada yangu kaniambukiza ukimwi makusudi”

Nimejikuta nasonya kiume na kujisemea qummah nina we! Umejiambukiza mwenyewe kwa tamaa zako! We si uliona dada yako anafaidi haya faidi na ukimwi!

Al qiswaswa haqu!
We uliona dada yako ana moyo wa plastic ama chuma sio! Ushukuru kakuacha umevagaa ukimwi kuna wengine wanawauwa waduwanzi kama nyinyi!! Wengine wanafanya operation iso rasmi wanakukata hicho kipapatio kilicholutia jeuri kumtusi dada yako!
 
Pumbavu Zako... We ndo umejiambukiza kenge wewe.


Ulikua unamuita shemeji, Mara umetanua mapaja umebeba mimba yake... Fala sana... Jibebe kuku ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom