Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,229
- 13,442
Zungumza na Dada yako Kama kweli ameokoka hawezi Fanya hivyo huko ni ulokole fake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku hizi si hauozeshwi mpaka uwe na cheti cha kupimwa HIV?
Uungwana ni kuambiana ukweli.
Huyo dada'ko kama anamficha huyo mchumba bado hajaokoka kama unavyodai, anajidanganya tu.
Pengine na mchezo kisha mpa. Si mnasema siku hizi hamuoani mpaka mlane kwanza!
Kuokoka kiukweli ni kujisalimisha kwa Mwenyeezi Mungu aka Kusilimu, vinginevyo ni uongo tu.
Waachie wenyewe
Ukimwi sikuhizi wakawaida sna
Habari zenu wana Jf,
Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili.Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.
Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha mtu.Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.
Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.
Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.
Kuna dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.
Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa.Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.
Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu
Wadau, nahitaji msaada wa mawazo
Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?
Dah watu wana roho mbaya sana. Tunauana hivi hivi!!!!!!!!!!!. _nn zake na
unasononesha sana.
Da Asia unampotosha mwenzako hivi hivi, live kabisa.ushauri wangu ni kua tatizo la dada yako ni lake na ni maisha yake na huyo mchumba wake. si jukumu lako wewe kuingilia mambo yasiyokuhusu. Jali maisha yako na waache waendelee. Jiweke kwenye nafasi ya dada yako, halafu dada yako angeenda kusema kwa mchumba wako status yako, how would you feel.... Kama ni lazima usaidie, jitahidi kumuongoza dada yako a built ujasiri wa kumwambia mchumba wake yeye mwenyewe na sio wewe ndio uwe msemaji. Ukimwi sio ugojwa kama cancer na diabetes bali ni mfumo kubadilika mwilini. wewe mwenye kiherehere unaweza ukaondoka duniani kwa jambo dogo sana ukawaacha wakaendelea kuishi miaka mingini 20 na watoto wenye afya tele. achana na hii kitu, its too personal. nyinyi kama familia endeleeni na maandalizi ya harusi wala msizungumzie hili jambo maana si lenu bali ni la dada yenu, atajua mwenyewe jinsi ya kulitatua kwa mchumba wake. kwanini uumie moyoni kwa jambo ambalo si lako. binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Kabla hawajaamua kuoana ilikua ni jukumu lao wenyewe kuamua kwenda kucheki afya zao maana mwisho wa siku ni kwa maisha mazuri, sasa kama hawakufikiria hilo wewe nini wa kutaka kuropoka. incase unamwambia halafu asikuamini akakuona unamfanyia roho mbaya hasa kwa kuhisi unaharibu kwa vile ni ndugu wa kambo, utajisikiaje? kama si aibu iliyokithiri. waache na maisha yao, na wewe endelea na ya kwako.
Waachie wenyewe
Ukimwi sikuhizi wakawaida sna
Da Asia unampotosha mwenzako hivi hivi, live kabisa.
- Eti vvu sio issue kama diabetes/cancer kwa hiyo aache kiherehere.
- Eti hayo ni maisha yao kwa hiyo awaache nae aishi kivyake.
Please, acha kupotosha umma na wale wenye uelewa mdogo.
Da Asia unampotosha mwenzako hivi hivi, live kabisa.
- Eti vvu sio issue kama diabetes/cancer kwa hiyo aache kiherehere.
- Eti hayo ni maisha yao kwa hiyo awaache nae aishi kivyake.
Please, acha kupotosha umma na wale wenye uelewa mdogo.
Nakueleza kutoka moyoni. Unashiriki kumuangamiza (kumuua/kumtesa) binaadamu mwenzio ambaye hana nia mbaya na nyie. Ungejisikiaje yeye ndo amemfanyia dada yenu.
Hata kama sio jukumu lako kumueleza. Onyesha kwa ndugu zako (familia) kuwa hujapenda hiyo isu, kwa kujiengua katika hili. Ikiwezekana hilo la nyumbani kwako kuwa ndio kama mzazi liwe la kwanza.
Nakuhakikishia hili litakusumbua (haunt) maisha yako yote.
I will never do search a thing.
Learn to stand alone, standing alone for the truth. Just know God is with you coz you're doing the right thing.
Ingekuwa wewe je?
Mie UKIMWI nauona ni wakawaida mno,unaweza kuishi nao for the rest of your life na ukapata watoto nakadhalika wa kadha.
Fuatilia kama hawajavuana chupi umwambie bhana.
ushauri wangu ni kua tatizo la dada yako ni lake na ni maisha yake na huyo mchumba wake. si jukumu lako wewe kuingilia mambo yasiyokuhusu. Jali maisha yako na waache waendelee. Jiweke kwenye nafasi ya dada yako, halafu dada yako angeenda kusema kwa mchumba wako status yako, how would you feel.... Kama ni lazima usaidie, jitahidi kumuongoza dada yako a built ujasiri wa kumwambia mchumba wake yeye mwenyewe na sio wewe ndio uwe msemaji. Ukimwi sio ugojwa kama cancer na diabetes bali ni mfumo kubadilika mwilini. wewe mwenye kiherehere unaweza ukaondoka duniani kwa jambo dogo sana ukawaacha wakaendelea kuishi miaka mingini 20 na watoto wenye afya tele. achana na hii kitu, its too personal. nyinyi kama familia endeleeni na maandalizi ya harusi wala msizungumzie hili jambo maana si lenu bali ni la dada yenu, atajua mwenyewe jinsi ya kulitatua kwa mchumba wake. kwanini uumie moyoni kwa jambo ambalo si lako. binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Kabla hawajaamua kuoana ilikua ni jukumu lao wenyewe kuamua kwenda kucheki afya zao maana mwisho wa siku ni kwa maisha mazuri, sasa kama hawakufikiria hilo wewe nini wa kutaka kuropoka. incase unamwambia halafu asikuamini akakuona unamfanyia roho mbaya hasa kwa kuhisi unaharibu kwa vile ni ndugu wa kambo, utajisikiaje? kama si aibu iliyokithiri. waache na maisha yao, na wewe endelea na ya kwako.
Hii chai kabisa
halafu muanzisha mada kila siku unakuja na chai mpya
eti mahari tushakula kabisa,mara barua upokee wewe huku baba yako yupo
cc BADILI TABIA