Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Mwambie aende kwenye vituo vyao vya dawa, atakutana na hb wa ukweli mwenye status kama yake.
 
Waachie wenyewe
Ukimwi sikuhizi wakawaida sna

Na wewe usikute ni walewale, kwa ushauri huu unaeza kumwekea ata sumu kwenye chakula. Sio kwamba na wewe ukiukwaa basi unamvuta na mwenzio hukohuko hii ni dhambi ya uuaji jitahidi kutenda mema na Mungu atakubariki
 
Ila usiogope, ka vp nipe namba ya huyo jamaa nimpigie na nimwage mchele. Nakusaidia buuuuureee, sitaki hata shinkumi
 
Unaweza usife kwa UKIMWI lakini ukafa kwenye bodaboda au kupigwa na kina AROOO RIRIKUWA NI RIJAMbAZI

Ndivyo mnavyo justify maisha ya mtu? Kama yako unaya justify hivyo, usijustify ya mwenzio. Ukimwi ni kitu ingine kabisa.
 
KAMA HUTAKI KUSHIRIKI HIYO SIRI AMBAYO NI DHAMBI KWA MUNGU

USHAUIRI

PLEASE PLEASE, FANYA JUU CHINI DADA AKO ASEME MWENYE KWA KINYWA CHAKE,


AKIGOMA NABIDI MWITISHE KIKAO na muwaambie maharusi kila mtu aseme siri zake kabla ya ndoa

Hayo yamesha fanyika sana,sio geni hilo

UKIACHA WAOANE NA HIYO SIRI,ITAKUTESA MPAK KUFA KWAKO
 
Wasikuushulisha kijana dunia ya leo tuna matatizo kweli sifikirii km jamaa km hajamfunua huyo mchumba wake km unaona uzito kusema naunataka kutoa dukuduku fata ushauri wa jamaa huko nyuma nunua laini mpya mtumie nbonge la sms ataisoma number na atajua ukweli km unaujasiri mwambie tt face2face ila km jamaa kala na hajui daaah tafuta ambulance kabisa
 
Kitu kimoja cha kuwa muangalifu. Watu walioathirika huwa wana vinyongo sana. Anaweza kukugeukia akakuharibia wewe. So pia hiyo tahadhari chukua.

Yupo dada mmoja aliua watoto wa dada yake kwa kupiga mswaki kutumia miswaki ya hao watoto. Akawaambukiza. Sababu ni ya kijinga. So pia kuwa makini. Unaweza fata ushauri wa kuazima simu ya mtu ambaye haeatamjua ukatuma sms. Just to be in the safe side.
 
Fanya kitu sahihi ili usisutwe na dhamira yako...
 
Ki ukweli uyo wokovu wake una mashaka y atake kumuua kijana wa watu ndoa kitu gani kaka mwambie vaa kiatu chake ila mwambie kiume sabbu uwezi kujua anampnda vipi na mapenz ni upofu unaweza kumwambia akamsimulia dada yko ukawa ugomvi na wew
 
Njia nyingine ni ya wewe kuweka zuio kanisani (ama kwengineko ndoa inapotarajiwa kufungwa).

Lakini kabla ya hiyo, semeni vizuri (si kumlazimisha bali ni councelling) na dada yenu ili aweze kuwa wazi kwenu na kwa huyo mume mtarajiwa yeye mwenyewe (njia hii itapepusha mambo mengi kuliko njia nyingine yoyote). Inawezekana keshatembea na jamaa na washachomoa mimba kadhaa na hivyo suala la kuweka wazi HIV status linakuwa na suala la taarifa zaidi kuliko kuokoa maisha. Inawezekana huyo jamaa pia nae ni muathirika vile vile kama alivyo dada yenu (huwezi pima HIV kwa macho!).
 
Hivyo watu bado wanachumbiana bila kupima Karne hii? Huyo msomi usomi upo wapi?
Dunia ya sasa kabla hamjagegedana, kupima kwanza.

Wewe kaka Waite wote dada yako na huyo shem wako waambie wakapime ukimwi, au msisitize huyo shem wako amchukue dada yako wakapime.
 
Kama unajistukia kumwambia ukweli basi nitumie namba yake mimi nimwambie. Lakini una uhakika kua jamaa hajawahi kula mzigo??
 
Hata kwa kupitia uzi huu inaezekana ujumbe ushafika
 
Habari zenu wana Jf,

Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili.Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.

Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha mtu.Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.

Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.

Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.

Kuna dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.

Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa.Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.

Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu

Wadau, nahitaji msaada wa mawazo

Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?

Kama wewe kaka mtu wa damu tu unakiri kama dada yako kanona na wowowo matata sana..unadhani huyo jamaa asiye na undugu nae atakuelewa hata ukimwambia ana ngoma??..kama hujipendi basi we kajaribu kumwambia kama hujarudi na ngeu. Jamaa hawezi kukubali na sababu unaijua vizuri
 
Back
Top Bottom