Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Hizi Imani za wageni sisi hatuziwezi maana sifa yetu kubwa ni unafiki.

Kijana wa watu huenda anatafuta faraja lakini atakachoambulia ni kinyume chake. Watu husema taarifa sahihi humsaidia mtu kufanya maamuzi sahihi. Mwambie ukweli shemeji yako. Hata kufumbia macho uovu ni UOVU.
 
Mkuu umepata nafasi ya kuokoa uhai wa mtu..Jaribu kuitumia
 
Habari zenu wana Jf,

Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili.Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.

Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha mtu.Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.

Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.

Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.

Kuna dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.

Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa.Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.

Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu

Wadau, nahitaji msaada wa mawazo

Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?

Nimependa unakunywa chai ya laki mbili.
Duuh gharama kweli
kifo kileee.
Mhh qwikwiii ...
Aisee ww shmj hahaaaa qwikwiii lunch yako sh ngapi ?. ...
Qwikwiiiiii.
 
Kwa jinsi sisi vijana ambavyo hatujielewi, lazima huyo dada yako amepigwa pipe za kutosha kabla hata hawajatambulishana.
 
Hiyo dhambi itawagharimu na kuwatafuna waache waendele kupokea na hela za Chai....
 
Kwakuwa ni walokole labda hawaja chakachuana bado ila swali wataowanaje bila kujua status yao. kwa sisi madhehebu yetu lazima kwenda kujua afya kabla ya ndoa na uthibitisho unapelekwa. sasa sijui hao wapendwa ila ni muhimu kumjuza jamaaa mkiwa mshamweka sawa dada yenu kuwa jamaa tunamwambia ukweli au amweleze mwenyewe
 
laws of contract ACT of parliament 2002 *ap1 section 1 para 1 ,h,b,e
zinajibu tatizo lako.
 
Halafu ni kweli kabisa sawa za ARV zinafanya watu wanameremeta sana... nna mifano hai kwa watumiaji hakika kama ni mwanamke lazima wezere litokeee. chezea ARV wewe
 
Nadhani hukuwa na nia thabiti ya kuliepuka hili na kumwepusha huyo shemejio mtarajiwa. Itakuwaje mpaka jamaa analeta mahari bado wewe na Nduguzo mmekaa kimya? Kwani mlikuwa hamjui? Haya mmeshabugia hiyo pesa eti bado unasifia Dadako Muathirika kuwa ana TAKO badala ya kumkataZa asiingie kwenye mahusiano na mtu ambaye hajui status yake huko ni Directly unashiriki kwenye UMAUTI wa Shemejio mtarajiwa
 
Kama wewe kaka mtu wa damu tu unakiri kama dada yako kanona na wowowo matata sana..unadhani huyo jamaa asiye na undugu nae atakuelewa hata ukimwambia ana ngoma??..kama hujipendi basi we kajaribu kumwambia kama hujarudi na ngeu. Jamaa hawezi kukubali na sababu unaijua vizuri


Watu siku hizi wame elimika sana. Wanajua kuwa mnene sio kipimo cha afya.
 
Hii chai kabisa

halafu muanzisha mada kila siku unakuja na chai mpya
eti mahari tushakula kabisa,mara barua upokee wewe huku baba yako yupo
cc BADILI TABIA

Usisahau pia kuwa kwenye hiyo mahari baba hakupata mgao,wamegawana 'makaka' Amesahau kuwa "Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu"
 
Last edited by a moderator:
Kitu kimoja cha kuwa muangalifu. Watu walioathirika huwa wana vinyongo sana. Anaweza kukugeukia akakuharibia wewe. So pia hiyo tahadhari chukua.

Yupo dada mmoja aliua watoto wa dada yake kwa kupiga mswaki kutumia miswaki ya hao watoto. Akawaambukiza. Sababu ni ya kijinga. So pia kuwa makini. Unaweza fata ushauri wa kuazima simu ya mtu ambaye haeatamjua ukatuma sms. Just to be in the safe side.

Unamaanisha nini kwa kusema, 'huwa wana vinyongo sana' ?
 
Unamaanisha nini kwa kusema, 'huwa wana vinyongo sana' ?

Wapo ninao wafahamu wengi wakutosha kusema hivyo. Inawezekana si wote ila wengi wao wako hivyo. Uangalifu mkubwa unahitajika kuishi nao. Mfano ni kama huo nilioutoa hapo juu.

Sina maana ya kumkwaza mtu lakini. It is what it is i know.
 
Jambo la msingi hapo mshauri wakapime wote hata kama washavuana chupi itakua salama kwako na kama ni dhambi utakua umejivua. We ukimweleza kwa sasa haitasaidia kama keshaambukizwa atataharuki. Waende watapewa canceling wataoana na wanaweza kupata mtoto. Wakapime
 
Back
Top Bottom