Mafiningo
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 4,435
- 4,662
Sawa kabisa ,,kama kuolewa basi uolewe na unayeridhika nae, siyo tu uolewe halafu unaishi kwa majuto.binafsi nina 29 na sijaolewa na Hilo halinifanyi nijione takataka Kisha nikubali kuolewa na takataka yoyote Kama mtoa mada kisa tu na Mimi nionekane na jamii nimeolewa,,, ukisema tunachagua Sana unamaanisha hatuna haki ya kuchagua wale tunaoona wanatufaa ktk maisha na haki hiyo Ni kwa wanaume tu sisi tuzoezoe tu Bora liende.... kauli Kama hizi ndizo zinafanya wanawake wengi kuvumilia ndoa za manyanyaso,, vipigo na dharau kisa anaogopa akiachika watu Kama wewe mtoa mada mtamnanga kwa kejeli mtaani bila kufahamu undani wake,, sitoacha kumuomba Mungu anijaaliye mume atakaye kua na kheri na Mimi sababu ndoa Ni ibada na stara kwa wote mwanamke na mwanaume lakini sitokua tayari kujitwika gunia la mavi maana ake mwanaume asiye na busara,, huruma Wala heshima kwa wanawake kwa kuogopea masimango ya wanajamii. hata hao unaowaona wameolewa waliwachagua Waume zao Kati ya wengi waliowafuata wakawaona watawafaa hawakukubali tu Bora liende,,in your next life nakuombea uzaliwe mwanamke,,.
Mimi niliishi na mke wangu miaka mitatu hadi tukaja kuamua wenyewe kuwa sasa tuoane. Tunaenjoy ndoa yetu sana sasa.