Dada zetu kuweni makini na madanga mnayopata sehemu za starehe

Dada zetu kuweni makini na madanga mnayopata sehemu za starehe

Kuna demu nilimpa offer mahala, akapiga mtungi katumia hela zangu (siri yangu) halafu ananiambia ana njaa, nikamwambia aagize msosi akaagiza kuku mzima....at the end kapotea, sasa kama huyu siku siunajilengesha kwake unampiga mtungi kidogo na nusu kaputi kidogo akizima tu, unawapelekea jamaa kujilipa gharama zako..... "If somebody did a good thing for you, its better doing the same..." umenunuliwa mipombe na kula minyama ya bure baada ya wewe nawe kwenda kutoa burudani unakimbia, siku nyingine ukitolewa figo utamlaumu nani?
[emoji1][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji2][emoji1][emoji1][emoji1][emoji28]pole
 
Waende muhimbili wafatilie wagonjwa walio badilishwa figo ndani ya masaa 72 kutokea siku ya tukio..

Kwenye hao wagonjwa wote wanatakiwa waseme walipotoa hizo figo walizowekewa.
Maadili ya kazi ya utabibu hayaruhusu kumwekea mgonjwa figo isiyojulikana ilikotoka, kimsingi huwezi kumwekea mtu figo yoyote kutoka kwa binadam yeyote, mpaka binadam huyo (donor) afanyiwe vipimo kadha wa kadha vya kuonesha kuwa mwili wake na mwili wa mpokeaji wa figo hiyo (receipient) inaendana (compatible). Jambo la kuchunguza hapa ni uwezekano wa kuwepo kwa "biashara ya viungo vya binadam" hapa nchini, ambapo baadhi ya wataalamu wa afya wasiokua na maadili wanaweza kushirikiana na wafanyabiashara wa viungo hivyo ndani na nje ya nchi kufanya biashara hiyo haramu.
 
Figo labda ya kwenda kutambikia. Figo ya kwenda kumwekea mtu mwingine haitolewi hivyo. Inatolewa hospital kwenye chumba cha upasuaji na madaktari bingwa chini ya mazingira maalum ile isipoteze function (isife kabla ya kumwekea mtu mwingine). Na inachukuwa saa kadhaa kumaliza hilo zoezi.
mkuu kuna hospital kubwa tu hapa town wanafanya hii michezo ila legally ila sio legal kiviiiile yani wanawanunua watu wanaotaka kuuza figo usikute daktari kapewa mtonyo kaifanya ishu kitaalam kabisa
 
Mechanism ya kuhifadhi IPO linaweza kaa nnje ya mwili mpaka masaa 72 lakini ndani storage media.

View attachment 2088970
Hiyo Preservation ndo mazingira kama hayo yanahitajika na Proffesional people sio tu kuchana na kungofoa Figo.. Na process hiyo Kupata wataalamu wenye uwezo sio wahuni wakuteka watu na kufanya hayaaa..!! So hizi figo hakuna namna zimeenda kupandikizwa
 
mkuu kuna hospital kubwa tu hapa town wanafanya hii michezo ila legally ila sio legal kiviiiile yani wanawanunua watu wanaotaka kuuza figo usikute daktari kapewa mtonyo kaifanya ishu kitaalam kabisa
Duuh kupandikiza figo wanafanya Muhimbili mkuu
 
Nashukuru sana kwa maelezo yaliyonyooka. Kama nimukuelewa vizuri ni kuwa lazima wataalamu tena mahiri kwenye hiyo fani wahusike na kwa kiasi kikubwa kwenye nchi za kwetu huwezi tu kutolewa figo akapandikizwa mtu mwingine sehemu yoyote zaidi ya hospitali. Sasa hizi stori sijui dada alikuwa baa na mzee mmoja akamlewesha akaenda kutoa figo zinaonekana kabisa zitakuwa uwongo uwongo tu.

Hapa ndio naona umuhimu wa serikali kuingilia kati haraka kwani hizi stori za uwongo uwongo zimekuwa nyingi sana kwenye magroup ya whatasapp. Ni stori ambazo zinaleta taharuki sana kwenye jamii bila sababu ya msingi. Wote tunajua serikali kupitia TCRA inaweza kabisa kuwapata hawa wasambaza taarifa ili waweze kuthibitisha taarifa zao. Na ni wajibu wa serikali kutoa taarifa sahihi kwenye vyombo vya habari kuliko kuendelea kuacha habari tata kama hizi zisambae kwa kiasi kukbwa kwenye vyombo vya habari kwani kwanza zilianzia kwenye whatsapp sasa hivi zipo JF hatujui kesho zitafika wapi hasa ukizingatia baadhi ya waandishi huwa wanaokoteza habari badala ya kutatfuta na kufuatilia habari kiundani.
Wewe mtu wa kale kweli ndugu yangu,waru siku hizi huduma za hospitali wanazo km theatres majumbani kwao. Wana kila facilities km za hospitali plus proffessional doctors
 
Nasikia alikutwa geust house,, lazima jamaa alikojowa Kwanza kabla ya mauaji.

RIP mrembo,,Mungu atakulipia kwa wote waliohusika kwa unyama huu.
Wadada tena wanavyopenda hela na bata
Utafikiria tiaraei vile
Kwa mfumo huu watangolewa sana viungo
Inabdi wabadilike sasa

Ova
 
Waende muhimbili wafatilie wagonjwa walio badilishwa figo ndani ya masaa 72 kutokea siku ya tukio..

Kwenye hao wagonjwa wote wanatakiwa waseme walipotoa hizo figo walizowekewa.
kuna utaratibu mzuri sana tena wa wazi kabla ya kufikia hatua ya mwisho ya kutoa figo.
labda kama kua taasisi ya siri ambayo ipo kusikojulikana inayofanya huo uhalifu.
 
Huu mji ifike mda police waanze kufanya vetting ya vijana wanachofanya to survive maana kumekuwa na watu wa ovyo wanaoshinda mabar na club bila kujulikana source ya income especially mbezi beach,sinza na tabata.

naunga mkono hoja
 
Maadili ya kazi ya utabibu hayaruhusu kumwekea mgonjwa figo isiyojulikana ilikotoka, kimsingi huwezi kumwekea mtu figo yoyote kutoka kwa binadam yeyote, mpaka binadam huyo (donor) afanyiwe vipimo kadha wa kadha vya kuonesha kuwa mwili wake na mwili wa mpokeaji wa figo hiyo (receipient) inaendana (compatible). Jambo la kuchunguza hapa ni uwezekano wa kuwepo kwa "biashara ya viungo vya binadam" hapa nchini, ambapo baadhi ya wataalamu wa afya wasiokua na maadili wanaweza kushirikiana na wafanyabiashara wa viungo hivyo ndani na nje ya nchi kufanya biashara hiyo haramu.
Yani tunajua fika ikiwa hivyo lazima kunawatu watawajibishwa hapo hospital ya taifa.. kwasababu ndio hospitali pekee inaweza fanya hiyo transplant ukiachana na Ile ya Dodoma.. kama wapo matabibu wanao toa mimba kinyume na maadili ya utumishi hata kuvunja hiyo miiko hawashundwi mkuu ukizingatia pesa ya figo ni kubwa zaidi
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hiyo Preservation ndo mazingira kama hayo yanahitajika na Proffesional people sio tu kuchana na kungofoa Figo.. Na process hiyo Kupata wataalamu wenye uwezo sio wahuni wakuteka watu na kufanya hayaaa..!! So hizi figo hakuna namna zimeenda kupandikizwa
Kwani ulikuwepo akitolewa figo ukaona waliotoa hawakuwa professional?..
 
Back
Top Bottom