Dada zetu siku hizi wamekua wazungu wa bandia

Dada zetu siku hizi wamekua wazungu wa bandia

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,085
Habari za Leo wakubwa,
poleni na mihangaiko jamani,

Basi leo nimejikuta nawaza mbali sana baada ya kukutana na dada mmoja ana mikucha mirefu balaa mara pap nikakumbuka movie ya shumileta, walati nakumbuka picha ya msyuka ikanijia nikaogopa. Nadhani uliwahi angalia movie ya msyuka jinsi inavyotisha.

Kwa kifupi hawa dada zetu wamekuwa WAZUNGU BANDIA mpaka wanatutisha eti.

Kope za bandia, nywele za bandia, kucha za bandia, makalio ya bandia, nyusi za bandia, sura ya bandia.

Halafu anakwambia anataka kuolewa na mwanaume mwenye DINI yaani yeye ajiweke kama JINI halafu atake mwanaume mwenye DINI. Dada yangu hapo lazima utapata mwenye MAJINI.
 
Huyo uliyekutana naye amekwambia anataka kuolewa au ni hisia zako?
 
Wanauza picha zao za uchi pia ama kweli dunia iko kasi sanaa au uongo ndugu zangu ?
 
Mkuu mbna kama una hasira sana .....au umenyimwa.....kimasihara😂😂
 
akitekcha niaje ?

vipi napata floor plan ya vyumba vitatu na public toi ?
 
Embu tuache bwana.


Ila hata mwenyewe nakerwa na wanawake wenzangu wanaobandika makucha marefu na makope ..loh!!
 
Wapumzisheni Dada zetu,Kuna watu wanaopenda madada ambao wapo kama MAJINI wengine wanapenda wanawake waliokaa KISHANGAZI yaani full vilemba na magauni kama ya mifuko ya mashineni.
Kweli kabisa! Ila huo mwonekano wa kishangazi dah! Hivi hata atapelekwa out kweli na lemba lake😀😀
 
Back
Top Bottom