Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Mkuu huo mzigo wa 3.8m unauza mwaka mzima??..kama hutojali tuambie ni bidhaa gan hzo tukushauri...maana wengne huo mzigo wanauza ndani ya mwezi tu
 
Pia Mzunguko wa hela kule ni mdogo tofauti na huku town.

Imagine DSM hapa fedha inayozunguka Kwa Siku ni zaidi ya 35B Kwa mujibu wa ripoti ya BoT ya Mwaka 2017 so hopefully kwasasa Mzunguko unaweza kufikia 200B na zaidi
Kijijini kwa biashara hapafai. Labda uende sehemu za machimboni au vijiji maarufu kwa kilimo cha mazao ya biashara. Ila hivi vijiji vya kawaida watu wanajilimia kwa ajili ya msosi ni pagumu sana.
 
Mkuu hili jukwaa la biashara sio jukwaa la lugha, kuna wadau wanakosea vitu vidogo vidogo kwenye kuandika ila huwa wanaleta madini safi sana humu,
Nadhani wewe unge-focus kwenye comments zingine. Ukiwa mtu wa kuhamishwa kimawazo kirahisi biashara hutaweza mkuu.
 
Inamaana Kwa mwaka umeuza mzigo wa milion 8

Milion 8 gawa Kwa 12 inamaana Kwa mwezi umeuza mzigo wa less than Laki 7.5

Kwa siku Laki 7.5 gawa Kwa 25 inamaana uliuza mzigo wa less than elfu 25.

Biashara gan hii au malimao?

Usitishe watu mkuu. Biashara ni hesabu zako .
 
Kwa hayo mahesabu unakubalije kuwalipa tra 250000. Tra unawalipa kutokana na biashara ilivyo. Mambo ya msiba usiyaingize kwenye biashara.
Mimi niliandikiwa na tra kulipa 100k kwa mwaka yaani biashara nilipoianza Tu, sijui hata itakuwa na uchangamfu UPI kwakweli nilijieleza kuwa ndo naanza na eneo nililokuwapo halina mzunguko wa watu kwa Aina ya biashara Ile niliishia kukosa fedha za Kodi kulipa tra kwa miaka mitatu.


Sasa nalipia nini tra wakati biashara unakaa ofsini unasubiri wateja hata mwezi mzima huoni mteja?!, mwezi unaofata unapata mteja mmoja au wawili haupati tena yaani nikifunga hesabu ya mwaka mzima nimeambulia chini ya laki moja kwa mwaka.

Nasema uhalisia lakini tra hawajui biashara wao ni kupanga Tu ovyo. Kilichonifanya nianzie tra ni kwamba niliwahi ifanyia hiyo biashara mkoa mwingine na ilikuwa vyema ila niliicha baadae na kufanya mambo mengine sasa Hali ilivyokuwa ngumu nilizama tena kwenye hiyo biashara mkoa mwingine sikuwa na mtaji Wa kuiiweka mjini ila ndo hivyo.


Bado sijaripoti tra sijui nitawaelezaje ushauri 😀
 
Kuna Kitu kinamiss kwenye Hesabu zako.Rudia Tena maelezo.Huo Mzigo wa Milion 3.8 ni manunuzi uliyofanya jumla mwaka mzima?na Je Hiyo Milioni 8.2 ni mauzo uliyofanya Jumla Mwaka mzima?
 
Kwani ww unataka uwalipe hao TRA kiasi gn?
 
Biashara inataka bidhaa inayoisha dukani,irudishwe hapo,Kwa Maelezo Yako inaonekana ulikuwa unauza TU,mpaka mwaka ukaisha bila kuongeza na kurudisha bishaa iliyoisha,Kwa mfano umeuza maji dukani yakaisha,inakubidi ukaongeze hayo maji yaliyopungua dukani ,usisubiri mpaka uuze bidhaa nyingi ndio ukaongeze bidhaa,maana ukisubiri uuze bidhaa nyingine ndio ukaongeze bidhaa ,Kuna wateja unawapoteza wanaohitaji bidhaa ambazo tayari zimeisha dukani. jitahidi bidhaa inayoisha dukani iagizwe ili kuzungusha mtaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ww unataka uwalipe hao TRA kiasi gn?
Nataka kuwalipa kulingana na ninchopata yaani walau kuwepo percent flani sio kukadiria pesa ambayo hautopata utawala nini?

Unaniambia nilipe laki moja yaani 25k kila baada ya miezi mitatu Mimi napata 20k katika miezi hiyo nikupe yote ?
 
Mkuu mnafanyaje tathmini Bila kuingia kwenye biashara yaani nadharia au hisia embu nifafanulie maana Niko kwa njia panda
Tathmini inafanyika Kwa kuingia sokoni na kuangalia ni biashara ipi ina wateja na inaweza kutoka Kwa urahisi.

Unaweza kujifunza kupitia biashara za wenzako zinazofanana na yako

Mara nyingi tathmini huusisha hali ya Soko, wapi unapopata bidhaa zako iwapo zitaisha, aina ya biashara unayotaka kuifanya, aina ya delivery utakayotumia kuwafikia wateja wako n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…