Biashara hizi ndogo ndogo zenye mtaji wa chini ya 10M kusavaivu ndani miaka mitatu ni ngumu sana mwaka jana nami nilifunga duka baadaya ya kutoona faida kutokana na gharama kubwa ya uendeshaji kwa mfano
1. Tra 250,000
2. Leseni jiji 200,000(phones and accessories)
3. Kodi jengo (150,000*12)=1,800,000
4. Umeme (10,000*12)=120,000
5. Afu kuna hawa jamaa wa fire niliwakataa
6. Posho ya mfanyakazi (100,000*12)=1,200,000
7.ulinzi (10,000*12) =120,000
8. Usafi na mengineyo=100,000
9. Service levy( hapa niligoma kabsa kutoa) wakatisha kufunga biashara wakanipa control number kwa lazima ila sikulipa
Kwa gharama Hizi kutoboa ni ngumu sana aisee bora niendelee kuajiliwa ila biashara ni big no kabsa