Nature bado mkali, namsifu ameweza kuitunza sauti yake bado anajiamini kutunga nyimbo mpya, ameweza kuhimili vishindo bila kukimbilia kula unga, ameoa anawatoto baba wa familia anaejitambua, safi sana. Ila tukubali ukweli kila zama na watu wake kwa sasa wapo wanao ona Dangote ni zaidi kwa kuwa ni wakati wake, ila wapo wanao ona Kiba ni zaidi kwa kuwa wana mkubali. Mimi bado namkubali Kiroboto kwa kuwa bado anajitambua.