Dah, Maisha ya kuridhika ni mazuri sana!

Dah, Maisha ya kuridhika ni mazuri sana!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Nimeamka sina kifungua kinywa, ilipofika saa 5 hivi nikakoroga uji kwa kutumia maziwa yaliyokuwepo kama nusu lita hivi!! Nilikunywa huo uji mtamu na moyo ukaridhika kuwa hayo ndiyo maisha mazuri. Nikiwa mitaani hakuna anayeweza kuhisi kuwa nimeshindia uji.

Kwa kweli kuridhika ni faida kubwa! Alisikika mtu mmoja akiwaeleza rafiki zake huku akiwa na uso wa furaha utadhani anamiliki mamilioni ya fedha!
 
Nimeamka sina kifungua kinywa, ilipofika saa 5 hivi nikakoroga uji kwa kutumia maziwa yaliyokuwepo kama nusu lita hivi!! Nilikunywa huo uji mtamu na moyo ukaridhika kuwa hayo ndiyo maisha mazuri. Nikiwa mitaani hakuna anayeweza kuhisi kuwa nimeshindia uji. Kwa kweli kuridhika ni faida kubwa!! Alisikika mtu mmoja akiwaeleza rafiki zake huku akiwa na uso wa furaha utadhani anamiliki mamilioni ya fedha!
Kuridhika ndo kila kitu mkuu.
 
Kuridhika ni hoja dhaifu ya kujitetea na kujifariji na Umaskini....

Work hard.. tafuta hela...
 
Kuridhika ni hoja dhaifu ya kujitetea na kujifariji na Umaskini....

Work hard.. tafuta hela...
Hujaelewa! Kuridhika haina maana kuwa uache kupambana na kusonga mbele katika maisha bali kuridhika kunakufanya usijione mnyonge, usimwone mwingine kuwa ni bora zaidi kwa kuwa ana kitu ambacho wewe huna! Kuridhika kunatunza nafsi ya mtu na kumpa ujasiri!!
 
Ni mentality tu, uji au wali ukifika tumboni hauna tofauti🤷🏻‍♂️
Dah!! Una akili kubwa sana!! Umenikumbusha mtu mmoja alienda kununua mchele dukani. Akakuta kuna sampuli mbali mbali za mchele. Ule ambao hauna changa ni sh 3,000/= kwa kilo. Chenga za mchele ni sh 800/= kwa kilo. Yeye akanunua chenga!! Halafu akatamba akisema, hamuwezi kunifanya mjinga nikanunua mchele kwa sh 3,000/= eti tu kwa kuwa haujakatikakatika wakati ninajua kuwa wakati naula utakatikakatika tu maana nitautafuna!! Huko mdomoni hakuna tofauti ya wali chenga na wali ulionyoka bila kukatikakatika!! Halafu akasema waibieni wajinga wasiokumbuka kuwa wakati wa kula watatafuna, kwangu hamuwezi kuwahi!!
 
maisha ni matamu sana kama utalidhika na ukipatacho, na Vile unaishi
 
This is it..! kuridhika ni kukiri ya kuwa umeshindwa, hauna mbinu tena za kujikwamua kiuchumi.
Hiyo ni tafsiri yako potofu ya kuridhika! Kwa tafsiri hiyo hutakaa uridhike na ufurahie maisha duniani!!! Kuridhika hakumfanyi mtu kutokusonga mbele katika maisha, bali kutamsaidia kusonga mbele bila presha akiwa na utulivu wa hali ya juu na kwa kujiamini bila kujiona kuwa ni mnyonge kuliko wengine!!
 
Lionel Messi angeridhika na mafanikio aliyoyapata kwenye soka Asinge pambana kufa na kupona kutwaa kombe la dunia..

Kuridhika ni hoja dhaifu sana....
 
Dah!! Una akili kubwa sana!! Umenikumbusha mtu mmoja alienda kununua mchele dukani. Akakuta kuna sampuli mbali mbali za mchele. Ule ambao hauna changa ni sh 3,000/= kwa kilo. Chenga za mchele ni sh 800/= kwa kilo. Yeye akanunua chenga!! Halafu akatamba akisema, hamuwezi kunifanya mjinga nikanunua mchele kwa sh 3,000/= eti tu kwa kuwa haujakatikakatika wakati ninajua kuwa wakati naula utakatikakatika tu maana nitautafuna!! Huko mdomoni hakuna tofauti ya wali chenga na wali uliokatikakatika!! Halafu akasema waibieni wajinga wasiokumbuka kuwa wakati wa kula watatafuna, kwangu hamuwezi kuwahi!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka mkuu ila naongezea tu. Kuridhika kunakufanya uonekane una hela pia uko matawi ya juu Kumbe Kapuku mmoja
 
Lionel Messi angeridhika na mafanikio aliyoyapata kwenye soka Asinge pambana kufa na kupona kutwaa kombe la dunia..

Kuridhika ni hoja dhaifu sana....
Kwa nini hamuelewi!! Kuridhika haina maana usisonge mbele! Kinyume chake kuridhika kunakupa nguvu ya kusonga mbele bila kujiona ni mnyonge!!
 
Maisha ni jinsi unavyoyapangilia na maisha ni meza inayozunguka wala mtu asikuambie kitu! Hakuna kukata tamaa na hakuna kujiona mnyonge na kujua mafanikio ni suala la muda tu! Ufahamu huu utakupa kuridhika na kila hatua ya maisha huku ukisonga mbele!! Maisa ni meza inayozunguka na usipokata tamaa mafanikio ni lazima, maana wote tunapewa ridhiki na Mungu hatua kwa hatua!
 
stay out of your comfort zone
True, but the previous comfort zone gives you the strength for the leap forward, it is the base for positive meditation and further planning!!! It is an important step in life, although it is not the final one!!!
 
Lionel Messi angeridhika na mafanikio aliyoyapata kwenye soka Asinge pambana kufa na kupona kutwaa kombe la dunia..

Kuridhika ni hoja dhaifu sana....
Kwahio wengine wote duniani ambao hawajapata bahati ya Kuwa Messi wasiridhike, wawe na stress, wawe na wivu kwa Messi hadi wanaingia kaburini!

Kuto ridhika kumeleta chuki, migogoro na Vita vingi duniani!

Mitume na Manabii hawakuwa wajinga kuwaasa watu wawe na mioyo ya kuridhika!

Kinyume Cha kuridhika Ni tamaa!
Kufanikiwa Jambo moja ukaridhika haiachishi kuanza kutafuta jambo lingine!
Maisha Ni mapambano ya daima

Mkulima akivuna gunia 10 akaridhika, haimuachishi kuendelea kulima msimu mwingine

Kuridhika Ni kupokea Jambo kwa Amani ya moyo bila chuki, lawama na manung'uniko

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom