Kuridhika maana yake umetosheka na ulicho nacho..
Sasa wewe uwe maskini halafu utosheke na umaskini wako???
Tafsiri zenu kuhusu "kuridhika" ndizo potofu.
Kuridhika maana yake umetosheka na hali yako na umekubali jinsi ilivyo hata kama ni mbaya, Hivyo kuridhika ni hoja dhaifu.
Unaponzwa na ujinga wako wa kutojua umaskini Ni nini.
Au unaponzwa na propaganda za motivational speakers!
Umaskini kwa mujibu wa hoja yetu, Ni ukosefu wa hitaji la msingi la maisha yako!
Chakula, mavazi, malazi, burudani, tiba, usafiri na mawasiliano!
Kwa mfano ukikosa kimoja wapo hapo juu wewe Ni maskini!
Umaskini unatafsiriwa kwa ukosefu na sio kiwango ulichonacho,
Bali utajiri hutafsiriwa kwa kiwango ulichonacho
Kwa mantiki hiyo, mtu anaishi kwa chai chapati, ugali dagaa huyu si maskini bila kujali watu wengine wanakula kwa viwango vikubwa zaidi!
Hapo hitaji la chakula amelitekeleza kwa 100%
Mtu mwenye nyumba moja ndogo si maskini japo wengine Wana nyumba kubwa Tena ni zaidi ya moja
Hitaji la malazi limekamilika
Mtu ana nguo 3 si maskini
Hitaji la mavazi limekamilika
Mwenye kusafiri na daladala si maskini, hitaji la usafiri limekamilika
Mwenye simu ndogo si maskini, hitaji la mawasiliano limekamilika
Anayetibiwa muhimbili si maskini japo mwingine atatibiwa Uingereza! Hitaji la tiba limekamilika
Anayetazama soka kwenye TV si maskini japo mwingine yupo uwanjani V.I.P
Hitaji la burudani limekamilika
Kwa tafsiri hii, mtu yoyote yupo huru kuamua kuridhika na alichonacho na huna haki kumnyanyasa kwa uamuzi wake huo uliotukuka!
Hakuna mtu anayeridhika kuwa maskini, kwa sababu umaskini si maisha yanayopasa!
Umaskini maana yake huna chakula, huna pakulala, huwezi kutibiwa, huwezi kusafiri Wala kuwasiliana!
Hata Mungu alisema tuwasaidie maskini!
Tafsiri ya umaskini uliyo nayo, ambayo inakufanya kupinga watu kuridhika na maisha sio sahihi!
Kwa tafsiri yako maana yake duniani wote Ni maskini na hatatokea atakaye jikwamua na umaskini, yaani alichonacho anapaswa awe na zaidi! Asiridhike!
Nakushauri panga mipango yako ya achievement, ukitoboa ridhika!
Ukiridhika na hicho ulichoachieve haikuachishi kuamua kupanga mipango mingine!
Kumbuka Yesu, alisema mwenye kanzu mbili, ampatie moja yule asiyenaye!
Asiye na kanzu Ni maskini na akipewa kanzu moja si maskini Tena, maana hitaji la mavazi atakuwa amelikamilisha kwa 100%
Hoja ya shetani Ni kupromoti utajiri duniani, kwa kupandikiza roho za kutoridhika!
Roho hizi zinapelekea watu kutosaidiana! Watu wengi wanakufa hospitalini kwa kukosa dawa, wakati watu wapo wenye utajiri
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app