Dah, Maisha ya kuridhika ni mazuri sana!

Umeiweka vizuri sana!!
 
Kwa nini hamuelewi!! Kuridhika haina maana usisonge mbele! Kinyume chake kuridhika kunakupa nguvu ya kusonga mbele bila kujiona ni mnyonge!!
Ukiridhika na umaskini utapataje nguvu ya kuendelea mbele??

Definition uliyo toa kuhusu "kuridhika" sijui umeitolea wapi au umekurupuka?

Ukiridhika maana yake umetosheka na ulicho nacho wala huitaji Zaidi ya ulicho nacho...

Sasa kama mtu ni maskini aridhike na umaskini wake kweli???

Kuridhika ni hoja dhaifu sana na ya kijinga.

Mnachojaribu kufanya ninyi ni kuleta maana (Definition) za kuipamba na kuisifu hii maana ya "kuridhika" ionekane ina mashiko kumbe ni Nonsense!!!
 
Kutokupata bahati ya kuwa kama mtu fulani sio kigezo cha kuridhika na hali yako na kuendelea kubaki hivyo hivyo ulivyo..

Halafu kuto kuridhika sio kuwa na stress au wivu.

Kuto kuridhika ni kutokubali kushindwa na kuto kukata tamaa kwenye jambo unalo pambania... Ukiridhika ina maanisha umetosheka na ulicho kipata wala huitaji zaidi ya hapo.
 
Kuridhika maana yake umetosheka na ulicho nacho..

Sasa wewe uwe maskini halafu utosheke na umaskini wako???

Tafsiri zenu kuhusu "kuridhika" ndizo potofu.

Kuridhika maana yake umetosheka na hali yako na umekubali jinsi ilivyo hata kama ni mbaya, Hivyo kuridhika ni hoja dhaifu.
 
Unatangaza ujinga na umaskini wako siyo?
 
K
Kuridhika ni hoja dhaifu ya kujitetea na kujifariji na Umaskini....

Work hard.. tafuta hela...
li
Kuridhika ni hoja dhaifu ya kujitetea na kujifariji na Umaskini....

Kuridhika ni hoja dhaifu ya kujitetea na kujifariji na Umaskini....

Work hard.. tafuta hela...
This an existential issue. What makes one happy remains individual. Definition ya umaskini ni broad. Money is very important lakini ukiingia kwenye mageiti na mafensi ya washua ni insecurity na depression. Usiitumie capitalism kujudge excellence. Sometimes watu tunaodhani ni maskini they are the richest. That is only if we stop imposing our own standards on others.
 
Unaponzwa na ujinga wako wa kutojua umaskini Ni nini.
Au unaponzwa na propaganda za motivational speakers!

Umaskini kwa mujibu wa hoja yetu, Ni ukosefu wa hitaji la msingi la maisha yako!

Chakula, mavazi, malazi, burudani, tiba, usafiri na mawasiliano!

Kwa mfano ukikosa kimoja wapo hapo juu wewe Ni maskini!
Umaskini unatafsiriwa kwa ukosefu na sio kiwango ulichonacho,
Bali utajiri hutafsiriwa kwa kiwango ulichonacho

Kwa mantiki hiyo, mtu anaishi kwa chai chapati, ugali dagaa huyu si maskini bila kujali watu wengine wanakula kwa viwango vikubwa zaidi!
Hapo hitaji la chakula amelitekeleza kwa 100%

Mtu mwenye nyumba moja ndogo si maskini japo wengine Wana nyumba kubwa Tena ni zaidi ya moja
Hitaji la malazi limekamilika

Mtu ana nguo 3 si maskini
Hitaji la mavazi limekamilika

Mwenye kusafiri na daladala si maskini, hitaji la usafiri limekamilika

Mwenye simu ndogo si maskini, hitaji la mawasiliano limekamilika

Anayetibiwa muhimbili si maskini japo mwingine atatibiwa Uingereza! Hitaji la tiba limekamilika

Anayetazama soka kwenye TV si maskini japo mwingine yupo uwanjani V.I.P
Hitaji la burudani limekamilika

Kwa tafsiri hii, mtu yoyote yupo huru kuamua kuridhika na alichonacho na huna haki kumnyanyasa kwa uamuzi wake huo uliotukuka!

Hakuna mtu anayeridhika kuwa maskini, kwa sababu umaskini si maisha yanayopasa!
Umaskini maana yake huna chakula, huna pakulala, huwezi kutibiwa, huwezi kusafiri Wala kuwasiliana!
Hata Mungu alisema tuwasaidie maskini!

Tafsiri ya umaskini uliyo nayo, ambayo inakufanya kupinga watu kuridhika na maisha sio sahihi!
Kwa tafsiri yako maana yake duniani wote Ni maskini na hatatokea atakaye jikwamua na umaskini, yaani alichonacho anapaswa awe na zaidi! Asiridhike!

Nakushauri panga mipango yako ya achievement, ukitoboa ridhika!
Ukiridhika na hicho ulichoachieve haikuachishi kuamua kupanga mipango mingine!

Kumbuka Yesu, alisema mwenye kanzu mbili, ampatie moja yule asiyenaye!
Asiye na kanzu Ni maskini na akipewa kanzu moja si maskini Tena, maana hitaji la mavazi atakuwa amelikamilisha kwa 100%

Hoja ya shetani Ni kupromoti utajiri duniani, kwa kupandikiza roho za kutoridhika!
Roho hizi zinapelekea watu kutosaidiana! Watu wengi wanakufa hospitalini kwa kukosa dawa, wakati watu wapo wenye utajiri






Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…