Dah! Nusu nilizwe Kariakooo

Dah! Nusu nilizwe Kariakooo

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Hellow

Mimi siku zote nilikuwa nikiambiwa watu wanaibiwa simu Kariakoo siamini nasemaga uzembe

Leo sasa yamenikuta mimi na bila yule kijana simu ingesepa bila kujua dah

Mchezo ulikuwa hivi, kaja kijana akaanza nikanyaga kwenye mgu uku anasema kuwa ungekanyagwa wewe namna hii ungejisikiaje sasa nikawa namshangaa na kujiuliza kumbe kuna mwezie kasha ingiza mkono mfukon anachukua simu wala sijui

Katokea kijana akaniita njoo mzee uchukue simu yako nashangaa na kujiuliza haya yametokeaje napewa simu uku mwizi akipigwa makofi nikashukuru basi nikasepa jamaa nampa hela kagoma bado najiuliza yametokeaje haya.

Simu yangu bado mpya hata mwezi haijaisha
 
Back
Top Bottom