Dah, vijana mnanunua magari ya Bilioni 1, mnasema ni forex tu, haya bwana!

Tochuku

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
5,322
Reaction score
8,412
Tena hata sio milioni 700, ni Bilioni Moja hio gari.

Na hapo dogo naona anataka kuanza kukodi private jet, itakayokua inampeleka katika safari zake.

Eti ni forex tu. Naandika ujumbe huu machozi yakinilenga na naitazama hii baiskeli yangu ya mifupa hapa imepaki juani.

Hamna shida bwana. Nchi Ina hela watu wanaogelea kwenye mahela.
 
Watu mnalizwa kiaina

Hizo ni schemes ya kufua pesa na deep state don 2 don manipulation.

Alafu wakienda kwenye podcast huko wanajiifanya kuwa ni juhudi pekee

LC300 zimetapakaa kama maji ila wewe hadi hapo mchana ndio una plan ya kupasha ukoko wa jana.
 
Sasa kama mnaambiwa ni forex, na unabisha. Nawe jaribu kufanya katika kile unacho hisi inapatika hiyo hela.. 😅
 
ni muhimu zaidi kufanya kazi kwa bidii bila kukerwa au kukatishwa tamaa na mafanikio ya wengine,
na itapendeza zaidi ndugu zangu
 
Huja msema hiyo mtu, ungetuonesha huenda tunajua mbili tatu tukakupasha ili upinhuze stress mkuu usije ukajipiga kitanzi bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…