Dahlia Majid: Kufanyike Uchunguzi huru kuongezeka mauaji yanayohusisha Polisi

Dahlia Majid: Kufanyike Uchunguzi huru kuongezeka mauaji yanayohusisha Polisi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Chama cha ACT-Wazalendo kimetaka uchunguzi wa Kamati ya Kibunge juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na magereza. Kimetaja vitendo vya utekaji, uteswaji wa watuhumiwa na ushirika wa Jeshi la Polisi kwenye matukio ya mauaji ya rai vimerudi kwa kasi zaidi kwa siku za hivi karibuni. Aidha, imeeleza mrundikano wa mahabusu, kuzuiwa kwa haki ya dhamana ya watuhumiwa na kushikiliwa kwa muda mrefu kinyume na sheria ni mambo yanayoendelea kulalamikiwa nchini.

Kauli hiyo ameitoa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Ndg. Dahlia Majid Hassan leo Mei 16, 2024 katika Uchambuzi wa bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani iliyowasilishwa bungeni jana jumatano.

Katika hatua zingine juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ameitaka Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora kufanya ukaguzi katika magereza, vituo vya Polisi na maeneo mengine vya vizuizi ili kuondoa msongamano wa mahabusu na wafungwa. Vile vile, ametaka maafisa wa Jeshi la Polisi wanaotuhumiwa na mauaji kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi.

Aidha, Waziri Kivuli Dahlia ametaka Jeshi la Polisi kufanyiwa mageuzi ya kimuundo na kiundeshaji kutoka kuwa chombo cha kimabavu na kwenda kwenda kwenye mfumo wa huduma. Hii itawezekana kwa kubadili utaratibu wa ukamataji, mfumo wa dhamana kwa kupunguza makosa yasiyo na dhamana, kuboresha mfumo wa upelelezi kwa kuongeza mafunzo zaidi na kutenga bajeti ya kutosha kwa upepelezi. Na Polisi kuondolewa kwenye utaratibu wa kuendesha mashtaka (wasiwe waendesha mshtaka).

Mbali na wito huo Ndugu Dahlia,ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi kuwalipa askari wa Jeshi la Magereza fedha za mazingira magumu ya kazi kiasi cha shilingi bilioni 27.

Kuhusu msongamano wa mahabusu na hali ya usalama katika Magereza Ndugu Dahlia amesema takwimu zinaonyesha mahabusu ni wengi kuliko wafungwa waliohukumiwa Kwa mujibu wa wizara (2020/21) kulikuwa na wafungwa na mahabusu 32,438 katika magereza yote nchini, Kati yao wafungwa ni 14,464 na mahabusu 17,974. Huku uwezo wa magereza ni kuhifadhi wafungwa na mahabusu 29,902 na Kusema ACT Wazalendo inasisitaza matumizi ya adhabu mbadala kama inavyobainishwa katika kifungu 3 (1) cha Sheria: The Community Services Act (Cap. 291 R.E. 2019) ili kupunguza msongamano katika magerezaa mbali mbali nchini.


Katika Mkutano huo pia Ndugu Dahlia amezungumzia Matukio ya uhalifu dhidi ya wanawake, wazee na Watoto na kusema ni vitendo vinavyoongezeka kila kukicha. Amesema kuwa ACT Wazalendo hairidhishwi na hatua za Serikali katika kukabiliana na uhalifu dhidi ya makundi hayo.


Katika hatua nyingine Ndugu Dahlia amezungumzia kero za upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kasi ndogo ya uzalishaji, usmbazaji na kufungamanisha mfumo huo na huduma katika taasisi nyingine. Pia, kuwepo kwa changamoto kwa baadhi ya Mikoa ya pembezoni (Kigoma na Kagera) kupata vitambulisho hivyo.


Amehitimisha uchambuzi wake kwa kusikitishwa na ongezeko kubwa la matukio ya ajali za barabarani zinazochangiwa na ubovu wa Miundombinu na uzembe wa ukaguzi wa ubora wa vyombo vya usafiri.

Ndg. Abdallah Khamis
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano-ScaRo
ACT Wazalendo
Mei 16, 2024
 
Haya mambo wewe acha tu.
Ngoja niishie hapo ndugu wazalendo.
 
Back
Top Bottom