Daima mbele nyuma mwiko, huu msemo ubadilishwe mapema.

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
1,846
Reaction score
2,754
Kwa dhati kabisa ninauomba uongozi wa yanga,, ukae chini ubadilishe hii slogan ya daima mbele nyuma mwiko.

Slogan hiyo imekua ikitumika vibaya kututusi wanayanga kwamba tunatembea na mwiko,, kitu ambacho ni tofauti na maana iliyodhamiriwa.

Saivi huku mtaani na mitandaoni tunapata shida sana kwakweli. Kila mara imekua mwiko mwiko.

Napendekeza msemo huu usemao : KWETU USHINDI DAIMA au USHINDI DAIMA. Mambo ya mwiko tumeyachoka
 
Hatuwezi kubadili slogan sababu ya utani wa jadi, mbona yalikuwepo ya yeboyebo, gongo wazi yote yamepita na tumesahau? Hili nalo litapita.

Hii slogan ni motisha hata katika maisha binafsi, ukisonga mbele songa bila kutazama nyuma.
Mwiko katika slogan hauna maana ya mwiko wa kupikia, bali ni katazo la kutokurudi nyuma.
 
Daima mbele,nyuma mwiko umeegeshwa.Jina zuri sana na limewakaa kama lori bovubovu na dereva wake mzeemzee!
 
Hatuwezi kubadili slogan sababu ya utani wa jadi, mbona yalikuwepo ya yeboyebo, gongo wazi yote yamepita na tumesahau? Hili nalo litapita.

Hii slogan ni motisha hata katika maisha binafsi, ukisonga mbele songa bila kutazama nyuma.
Mwiko katika slogan hauna maana ya mwiko wa kupikia, bali ni katazo la kutokurudi nyuma.
Ni kweli mkuu ila sasa katika kizazi hiki cha matusi maana imebadilishwa
 
Upo sahihi kabisa, kuna kauli mbiu nyingine ukiziweka ni rahisi watu kuwakebehi , kuwashalilisha na kuwacheka.

Pia sijua ni kwa nini Yanga haikutafuta nembo yenya maana kubwa. Kiukweli jina la Simba linawabeba sana na lina maana kubwa YA USHUJAA.

Hivi kweli Yanga walikosa jina la maana hadi kujiita Young African/Yanga. Hivi walikosa jina la maana na lenye thamani hata mtu akilisikia haina haja ya kutaka kujua lina maana gani.

Yaani hadi mtu atafsiri maana ya Yanga!!!!.

Mara tunaona vikandambili, unga wa Yanga.

NINA IMANI IPO SIKU WATAKUJA VIONGOZI WENYE UELEWA ZAIDI NA WATAONDOA HUU UJINGA.

JINA SIO MSAAFU KWAMBA HALIBADILIKI.

SIMBA INAJIBEBA YENYEWE BILA HATA YA MATANGAZO. JINA LA SIMBA LINAVUTIA SANA
 
Neno sahihi ni Young Africans, hilo la Yanga limetokana na wabongo wenzetu wa kipindi hicho kushindwa kunyosha kimalkia ipasavyo hivyo badala ya kutamka Young Africans wao wakawa wanaita Yanga. Ni sawa sawa na kule Morogoro wilaya ya Kilombero kuna sehemu inaitwa Signal ila kwavile wazee wetu walilishinda hilo neno kukaitwa Ziginali na hadi leo ndio jina linalotumika hiyo sehemu.
 
Upo sahihi kabisa, kuna kauli mbiu nyingine ukiziweka ni rahisi watu kuwakebehi , kuwashalilisha na kuwacheka.

Pia sijua ni kwa nini Yanga haikutafuta nembo yenya maana kubwa. Kiukweli jina la Simba linawabeba sana na lina maana kubwa YA USHUJAA.

Hivi kweli Yanga walikosa jina la maana hadi kujiita Young African/Yanga. Hivi walikosa jina la maana na lenye thamani hata mtu akilisikia haina haja ya kutaka kujua lina maana gani.

Yaani hadi mtu atafsiri maana ya Yanga!!!!.

Mara tunaona vikandambili, unga wa Yanga.

NINA IMANI IPO SIKU WATAKUJA VIONGOZI WENYE UELEWA ZAIDI NA WATAONDOA HUU UJINGA.

JINA SIO MSAAFU KWAMBA HALIBADILIKI.

SIMBA INAJIBEBA YENYEWE BILA HATA YA MATANGAZO. JINA LA SIMBA LINAVUTIA SANA
Kabisa mkuu ni upuuzi sana, saivi wanatusema kwamba daima mbele nyuma kuna mwiko. Haifai kabisa
 
Binafsi sioni shida na huu msemo. Binadamu na hila zao wanajaribu kupindisha maana ya maneno na kauli ulimwenguni kote. Kwakua kilichomaanishwa sio kinachotafsiriwa basi hakuna sababu ya kubadili huu msemo. Ningekushauri ukaulize maana kabla hujaja kuleta haya maoni yako.
 
Mtu mwenyewe ana kisirani hajui utani.Hapendi mwiko uwe nyuma.
 
Kwenye maisha usi ishi kufarahisha watu hio slogan haina baya lolote hata tukibadili bado watatafta maana yao wanayo ijua
Daima mbele
 
Back
Top Bottom