Daima usimdharau usiyemjua, mwenzenu leo nimekutwa na jambo

Daima usimdharau usiyemjua, mwenzenu leo nimekutwa na jambo

Kuna siku alikuja mzee wa kinyamwezi dukani afla simu yake ikaita simu ya tochi na mlio wa marimba. Jamaa wakacheka sana mzee kumaliza kuongea alikasirika sana alihisi kudharauliwa. Nikampooza pale na kumpa mkono wa salamu, mzee alitumia hela hapo mpaka jamaa wote walibaki kushangaa. Na alikuwa na hela ndefu tu, aliishia na kusema:- sipendi mtu anidharau kama sio huyu kaka ningali ondoka zamani sana. Usidharau kimuonekano wala kimatendo mpe heshima kila mtu
 
Wapemba hao Kuna mzee kipind fulani alikuwa anaenda crdb na kapu kama muuza samaki ndani anaweka pesa, anaenda akiwa kavaa ndala miaka ya 2008 enzi nipo Tanga pale crdb karibu na soko la uzunguni ,sikuamini alikuja na kofia chafu zile wanavaa wauza samaki na nguo chafu nikafiria ametoka deep sea hapo karibu na kapu juu kaweka Yale majani ya mikoko kama wanavyofunikia dagaa akafungua pale ila wanamjua aisee pesa kibao ila mkononi kajaa mapete kibao ...Nikiangalia nywele zake nikajua mpemba jamaa ana pesa ila kingine kutokana na mapete Yale mengi nahisi atakuwa mganga
Hahahahaaaa mpaka nimechekaka ndugu mana hata mimi niliwahi kumuona sana yule mzenji hapo hapo so umenikumbusha mbali sanaa na mishati yake michafu chafu yule tajiri wa maboti ya uvuvi nadhani
 
Hahahahaaaa mpaka nimechekaka ndugu mana hata mimi niliwahi kumuona sana yule mzenji hapo hapo so umenikumbusha mbali sanaa na mishati yake michafu chafu yule tajiri wa maboti ya uvuvi nadhani
Kuna stori nilizisikia!! eti Kuna siku majambazi walimuotea🤣🤣🤣wakampora
 
Fanya zoezi moja dogo tu. Chukua sarafu ya shilingi mia Tano (500/) itupe kwenye tope kisha itoe halafu isafishe.

Thamani yake imebadilika? Thamani ya binadamu haiondolewi na dhambi au muonekano wake.
 
Kuna siku nipo ktk hiace karume kuelekea home. Nimekaa ktk bansen burner. Ile kwanza nyuma ya dereva. Upepo mkali nikafunga kioo. Kuna jamaa alikuwa amekaa mbele yangu aliniuliza swali kuwa nina elimu gani?
Yaani umri wangu ulikuwa mdogo wa sekondari then aliniuliza lile swali.

Nikatafakari sana..kwamba umri huu nilitakiwa kuwa na elimu gani ili niweze kujibu kulingana na matakwa ya huyu ndezi. Kiukweli niliumizwa sana na zile dharau tena jamaa alikuwa mkubwa Sana ki umri. Niliamua kukaa kimya. Ila nilikuwa na hasira sana. Sijasahau ile dharau.
 
Kuna siku nipo ktk hiace karume kuelekea home. Nimekaa ktk bansen burner. Ile kwanza nyuma ya dereva. Upepo mkali nikafunga kioo. Kuna jamaa alikuwa amekaa mbele yangu aliniuliza swali kuwa nina elimu gani?
Yaani umri wangu ulikuwa mdogo wa sekondari then aliniuliza lile swali.

Nikatafakari sana..kwamba umri huu nilitakiwa kuwa na elimu gani ili niweze kujibu kulingana na matakwa ya huyu ndezi. Kiukweli niliumizwa sana na zile dharau tena jamaa alikuwa mkubwa Sana ki umri. Niliamua kukaa kimya. Ila nilikuwa na hasira sana. Sijasahau ile dharau.
Pole mkuu
 
Niko zangu kibandani kwangu, hua nauza nguo kwa jumla na rejareja. Mara ghafula wanatokea watu wawili wachafu, mzee kwa umri zaidi ya miaka sitini akiwa amevalia suruali yenye viraka kila sehemu ila sehemu inayoonekana zaidi ni maeneo ya kwenye zipu ambapo pameshonwa na uzi mweupe wakati suruali ni nyeusi.

Chini kavaa viatu visivyoeleweka na kichwani kabeba sanduku lililochakaa aina ya Omega kubwa haswaa likiwa limejaa vumbi jekundu kama lile la Kigoma(wanaojua vumbi la Kigoma watapata picha).

Mtu wa pili alikua ni mwanamke aliye kwenye umri wa miaka thelathini ya mwanzo akiwa amechoka na maisha haswa kwa muonekano. Amevaa sketi ya pande sita isiyoeleweka, coat la tracksuit ambalo limenyonyoka manyoya haswaa na yuko na nywele chafu hatari.

Kitu kilichoniijia akilini mwangu moja kwa moja wale watu ni omba omba ila wanaanza nichanganya kwa kuulizia bei ya nguo na mimi sikutaka kujichosha nao maana najua ni omba omba ila ndo wameamua kunichosha nikawa nawapa bei ya jumla, nguo ya kwanza shilingi ngapi, nikajibu 37,000,/ akaulizia ya pili, tatu na nne, jibu langu likawa lilelile.

Baadaye yule mwanaume akaomba waonyeshwe sehemu ya kajaribishia, kwa jinsi walivyo nikaona wanaendelea kunizingua nikamwambia tuelewane bei kwanza ndio nguo zijaribishiwe. Akaniuliza kwani izo nguo nne ni kiasi gani jumla, nikamjibu ni 148,000, akaniambia we nionyeshe tuu pakujaribishia bei hatutoshidwana nikaona isiwe tabu wacha nimuonyeshe.

Yule bidada aliyechoka akaingia na kajaribishia nguo, kwa macho yangu hakuna nguo hata moja iliyomkaa vizuri ila tayari sikua nawatilia manani so sikua nikuangaika nao.

Picha linaanza mwanaume, yule mbaba anaomba nimpe usalama ili aweze kutoa pesa nikaona kama ananichanganya nikamwambia mimi sina usalama, mara papu anamwambia yule mwanamke njoo unisaidie kushusha sanduku.

Maana tangu wamefika mwanaume alikua na sanduku kichwani na hakua amelishusha, bidada akaenda, sanduku lilikua zito haswaa kiasi kwamba mwanaume hawezi kuliweka chini mwenyewe.

Mwanaume akaingiza sanduku lake ndani, mwanamke akakaa mbele yake na kumsisitiza atoe pesa za kutosha matumizi yote maana hapa dukani ndio sehemu yenye usalama na hawatopata sehemu nyingine salama.

Mwanaume anafungua kufuli lililokua limefunga zipu za sanduku, sijaamini macho yangu, lile sanduku lilikua limejaa pesa zilizofugwa kwenye mabunda ya milioni milioni. Akatoa kibunda kimoja kisha akafunga sanduku baada ya hapo akahesa noti kumi na tano za elfu kumi kumi yaani laki moja na hamsini, nikakata pesa yangu na kumrudishia shilingi elfu mbili.

Mwanamke akaja akamtwisha mwanaume sanduku wakaondoka zao wakiwa wameniacha mdomo wazi na maswali kibao. Naendelea kujiuliza wametoka wapi na wànakwenda wapi, izo pesa zimetikana na nini, wanazipeleka banki ama wapi sijui?!

Kiukweli sijapata majibu kabisa ila naendelea kuduwaa, staili yao ya uvaaji ni mbinu ya ulinzi kwao ama walikua makapuku ila pesa wameziokota? Sanduku lilikua limejaa vumbi haswa na limechakaa haswa kama vile lilikua kwenye buti ya bus ambalo linapiga masafa marefu kwenye barabara ya vumbi.

Sasa ni kwamba sanduku waliliweka kwenye buti wakati wa safari ama walikaa nalo ndani, sijui, nimebaki na maswali kibao na kujidharu kwa kuwadharau wakati mimi ni kapuku na wao ndo mabosi.

Ndugu zangu wana JF, tuheshimu watu wote tunaokutana nao barabarani maana hatujui walichobeba. Mwenzenu leo nimekutwa na jambo, ila nimeona isiwe tabu nililete kwenu pia maana sisi ni wanafamilia mnaweza kua mmekutana na visanga tofauti tofauti ambavyo vinaweza kua mafundisho kwetu sote.
Hahahaha wamekuachia chuma ulete. Jipange.
 
Hii itakuwa ni hadithi Kama zilivyo hadithi nyingine naona,pesa Ina adabu zake.
 
Back
Top Bottom