Daimond Platnumz aonyesha muendelezo wa moja ya Nyumba zake

Hiyo nyumba sio ya diamond mbona? Ni ya kinje ipo tegeta
Nyumba ipi tena mpwa? Una maana ile ambayo Chibu amei-post kwenye instagram page yake, au? Hata kama wanasema Diamond ni mpenda show-off (ingawaje hakuna msanii asiye-post vitu vyake mtandaoni) sidhani kama amefikia hatua ya ku-post nyumba ya mtu halafu ajifanye ya kwake! Mbaya zaidi, kulikuwa na sababu gani afanye hivyo wakati hapajazuka zodozodo zozote za kumzodoa kwamba hana nyumba labda ndo tungesema ame-post nyumba ya Kinje na kujifanya yake kv amezodolewa hana nyumba! By the way, ina maana mpwa unataka kuniambia hiyo picha ni mara yako ya kwanza kuiona? Au imekutisha ile interior design.... bwah!bwah!bwah! Hebu pata picha Dinazarde anakuja ghetto kwako anakuta tiles zimeandikwa warumi, zingine Gossip_warumi... hahaahaaa haaaa, yaani hapo unamgonga begani kwa bahati mbaya, unamkuta mwenyewe taraaaatibu anadondokea kwenye sofa huku anareambua na vijimaneno, nh'nini bwanaa, mi sitaki..!" tumia pesa ikuzoee mpwa!
 
Last edited by a moderator:
Mnavyojishaua kama mmeambiwa mtaishi humo vile, nfyuuu ngoja niwahi zangu airport mie niende zangu jamaica, bongo kazi kusifia uchawi tu
Hebu kwenda huko! Ingekuwa state house ya madam Jide hapa tusingelala... kwani mi sikujui wewe! Au na wewe umepewa servant kota kwa madam Jide kule Kimara?
 
Nyumba yenyewe kimeo, imebomoka, ninefuraijee, Dinazarde umeona nyumba ya boss ukuta umevunjika? Nimefuraije maana siku yangu ilikuwa mbaya toka hasubuhi, sasa naweza kulala kwa amani
Mpwa, ni nyumba ipo tena iliyondoka ukuta? Unamaanisha hii:
Hiyo nyumba sio ya diamond mbona? Ni ya kinje ipo tegeta
Kama ndivyo, mbona simple tu, Kinje atajenga tu huo ukuta... it's not the big deal at all! Tena ukuta wenyewe wa fence, au ni mara yako ya kwanza kuona ukuta unabomoka... Braza Kinje atajenga tu huo ukuta!
 
nyie endeleeni kumpotosha mwenzenu,aendelee kufukuzana na upepo......na km wewe au wenzio wanadhania nina ishu na Diamond,mtajijuuu....siko hapa kuwaconvince tofauti.
Jestina huwa nakusoma, Iknow you ain't among the haters lakini katika hili, ni wapi unaona tatizo? Kwani Diamond kamletea mtu nyodo? Ina matatizo ni hilo la ku-post picha za nyumba yake kwenye instagram page? Ni msanii gani Tanzania hii au hata nje ya nchi hafanyi mambo kama haya? Hata huyo Ali KIba wanaesema sio mtu wa show-off ameshawahi ku-post picha za nyumba yake... so, what's the new hadi tuone katika hili basi Diamond anapaswa kufahamu kuna kupanda na kushuka? Au limekutisha hilo la Gold?

But all in all Jestina, don't forget kwamba kama ni kufuru hizo kufuru kazifanya kwenye nyumba... nadhani unafahamu tofauti kubwa iliyopo kati ya kufuru ya kufanya kwenye nyumba na kufuru ya kufanya kwenye vitu kama gari! Wakati gari usually huwa inashuka thamani with time, nyumba huwa inapanda thamani with time. Hata kesho na kesho kutwa akifirisika, bado atakuwa na asset kubwa sana mikoni mwake! Kwangu mimi ninachoona cha busara ni kumshauri kuwa na bima inayoendana na thamani ya nyumba yenyewe lakini kwa kufuru alizofanya kwenye nyumba, everything adds the value to the whole house!
 
Chezeya ma haters maninaaaaaaaaaaaaaaa nfyuuuuu, ukuta kule, na bado mpaka nyumba yote ijae mafuriko maninaaa, nilitaka nishangae jamani yani leo siku nzima napata maumivu, atleast nimefarijika, kwikwiiiiiiiiiiikk

Ila binamu ingawa domo simkubali kabisa ila hapa Ametisha! Kanifurahisha sana kwa kweli....anakula matunda ya kazi yake.Kumbe mziki unalipa sana ee, sasa crew yote ile inalipwaje? Mhuuu
 
Mnavyojishaua kama mmeambiwa mtaishi humo vile, nfyuuu ngoja niwahi zangu airport mie niende zangu jamaica, bongo kazi kusifia uchawi tu

Binamu una undugu na Dougie Mchawi! Mfyuuu zake amekosa hata la kuongea anabaki kujijambia jambia tu.Alie na mola wake hana maisha wala kipaji anabaki kutukana watu wenye maisha yao when she has a misarable life....
 
Ila binamu ingawa domo simkubali kabisa ila hapa Ametisha! Kanifurahisha sana kwa kweli....anakula matunda ya kazi yake.Kumbe mziki unalipa sana ee, sasa crew yote ile inalipwaje? Mhuuu
Tufanye kolabo basi mimi na wewe...
 
Kwani kuna tatizo kua na nyumba na bado ukapanga..?? ni maamuzi tu ya mtu...
Nashangaa... ndo maana kuna mtu nikamweleza usidhani kila anayepanga hana nyumba! Mtu ananunua coaster anafanya daladala na yeye akienda town anapanda daladala wakati pesa aliyonunulia coaster ingetosha kununulia angalau vitz akawa anatembelea instead!
 
Sioni kufuru aliyofanya Chibu hapa zaidi ya kua kafanya kutokana na uwezo wake. kwa wewe usie na uwezo unaona kufuru. Umesahau kua unajikuna unapofikia. Huwezi kuingiza shs. Million 100 kwa mwezi halafu ukajenga nyumba ya mil 50, ni kujitukanisha, na huwezi kuingiza elfu 50 kwa mwezi ukataka kujenga nyumba ya dhahabu, utakua mwizi. kuanguka ni mambo mengine kwa sasa maana anazidi kupanda. Acheni wivu na msifikirie negative tu kuwa ataanguka. nyie ndio mlikua mstari wa mbele kumsema hana nyumba, leo kawaonyesha ya dhahabu, roho zinawatoka... Watanzania mna shida sana... big up Chibu....
mnh sijui ni kweli au uongo,ila Diamond careful kuna kesho,wengi tu maisha yanawabadilikia inabaki kukumbuka zamani...acha kufuru mkuu
 
Hii nyumba ipo tegeta kontena inatazamana na mwenyekiti wa serokali ya mtaa wetu.Ni ya kawaida sana na iko bondeni.Hizo nyumba nyingine hakuna kwa sbb ni hii onayo tangazwa mara zote.
 
Mkuu umesahau neno moja ambalo linaleta maana kamili,"pure gold plated"
Sawa Mkuu, kumbe unafanya plating bado ulitarajia ufanye plating na fake metal? Mara kumi angesema gold-filled, ingekuwa ni questionable lakini amesema wazi kwamba ni gold plated material unless kama watu wanashindwa kutofautisha! Na hata angesema ni gold filled no one would be able kutofautisha, coz' gold filled and gold plated completely looks the same na huwezi kutofautisha kwa macho never ever lakini pamoja na yote hayo, amekuwa fair enough kusema ni gold plated na wala sio masinki ya gold au gold filled sinks!
 
Ukuta chini!!!au mchanga ulikuwa mwingi?
 

Attachments

  • 1427089632094.jpg
    61.7 KB · Views: 331
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…