Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy


Turejee maelezo yake hayo aliyoeleza.

Alisema alishindwa kutembea sababuvya upande wa kushoto wa mwili kutokuwa sawa, japo hatuwezi kuthibitisha kwa kuhadithiwa kama hivi ila hapo upande mmoja kuzingua ni inaelekea kama stroke.
Hapo ndipo ninapohisi sababu ya kupewa Artane.

Kwako Dokta uliyetibua mchumba wa mtu...😂😂😂
 
Nipo upande wa Dokta aliyesema ni atenolol maana effects alizozitaja ndo zilinipata. Nilikuwa nachangamka sana na napata ham ya kuongea sana, nilikuwa nahisi ka-raha flani hvi kama nimepiga tungi
 
Mi sijakataa..
Ila Artane haitumiki kwa ajili ya kuprevent stroke chief..
Artane mara nyingi Sana ni kwa Parkinson na hata wale wanaopata Repateated Fits au hata wenye Epilepsy .

Kwa sababu Artane Ni Group la dawa linaloitwa antidyskinetics..

Kama umesoma Pharmacology utanielewa vizuri..
 
Upo mbali sana na central target 🎯
 

We upo nondo yani unaelezea vizur na maelezo yako yanamashiko
 
DeMostAdmired, ninakushukuru kwa kutushirikisha uzoefu wa maisha ya kimapenzi uliyoyapitia. NIMEJIFUNZA MENGI. umepambana na moyo, roho na mwili juu ya mwanamke. Ulidhalilishwa kwa uwazi na watu waliona. Acha roho yako ipumzike na ifikirie project mpya; acha moyo uburudike na penzi jipya la kidigo na acha mwili unawiri kwa supu ya pweza na ngisi kwa kuachana na Messi for good. Bila ya kuachana naye utateseka sana siku za usoni. Hata hivyo, endelea kuwa na tahadhari kubwa maana, kwa mujibu wa uzi Umalaya na Ukahaba wa Kishua; utamaduni wa watu wa Tanga na hasa wa Wadigo, hauna wivu katika mapenzi. Mahusiano na mtoto wa ki Digo yanaweza kupelekea ndoa au mtoto, angalia usije ukazimia au kufa kabisa siku utakayogundua mpenzi wako analiwa na Kaka au baba, babu, mjomba wake. Achana na mtindo wa kujaribu mapenzi, nenda Kijijini kwenu ukaowe binamu yako maana anaweza kukuhurumia na kukuheshimu kwa dhati kabisa. Matatizo ya moyo yaliyokukumba ni makubwa na hapo ulipo usijidhanie umepona kabisa. Ni suala la muda tu na Volcano ya Nyiragongo au OldonyoLengai italipuka. Inahitaji kiasi kidogo tu cha stress kukulaza chali. ZINGATIA HILI.

Aidha, zingatia ushauri wa wadau mbalimbali waliokupatia hapa jamvini.

Kwa sasa unayo kazi inayokuingizia kipato, jitahidi ku maintain low profile life style ili afya yako idumu. Acha kufikiria tena mapenzi na Messi afe kabisa rohoni mwako.
 
MADAKTARI walinipa huu ushaur niache kuwaza sana mambo yasiyo na faida at this moment.
Dem niliyenaye naona tupo sawa tu hana shida na sitaki kabisa kumchunguza chunguza movements zake coz najihisi bado kuna vishida kidogo katika afya

Hasira bado nakuwa nazo zile za ghafla ghafla. Japo hazidum

Nakuwa na mood swing

Hizo ni baadhi ya vishida ambavyo bado vipo lakini vinaisha kadr siku zinavozd kwenda
 
Asante kwa hadithi yako ,imetoa funzo,
Angalizo, usimuoe huyo Binti labda awe bi mdogo wa tatu, vingnevyo utakufa mapema sana, jifunze kusema inatosha! Chukua namba zake ziblock halafu zifute jipe siku kadhaa kumwambia Mungu kitu!, additional point, in transition period, tafuta pisi Kali hata mbili kwa afya ya moyo wako!
 
Nimeuchukua ushaur nashukuru
 
Shida nyingi inayowapata wanaoshindwa ku-move on ni zile hisia za kuwa huyo uliye naye ni wa kipekee sana, hauwezi kupata mwingine kama yeye.

Mambo ni tofauti kwa ground; kuna watu wengi tu ambao ni wema na bora kumzidi huyo. Epuka ukosefu wa exposure, jichanganye, ufungue moyo uangalie na wengine.

Ulikuwa unaishi vizuri kabla hajaja kwenye maisha yako, unaweza ukaishi vizuri zaidi hata akitoka kwenye maisha yako. Although it's hard; life has to, and MUST, go on.
 
Thanxxx
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…