Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Hapa sasa ndo umeanza kutufurahisha wanaume kamili, nashauri tuchangie pesa tukupongeze ule Idd. Mercy mpige chini mazima akaolewe na Dr., Hata akijiua acha afe tu maana mwanamke malaya hana faida hapa Duniani, bora uoe huyo Madam mwenye kipato chake, hata kama kakuzidi miaka miwili poa tu, kuliko kuoa limalaya lililokusaliti tena kwa dharau, siku ulirogwa umuoe mercy, Dr. Ataendelea kukupigia na utapata stress hadi utakufa ukiwa na miaka 30.
MERCY anazingua sana utaona huko mbele
 
PICHA NZIMA YA YANAYOENDELEA YANAANZIA KATIKA HII EPISODE.

Tuendeleee.......

Mwezi wa 10 katika harakati zangu, ilikuwa nampeleka mtoto wa dada skul. Mtoto wa dada yangu wa tatu kuzaliwa, huyu mtoto ni wa kike alikuwa anaishi na mama mkubwa hapo Kilimanjaro moshi. Huyu dogo now yupo form town means mwaka jana alikuwa form one na alihama kutoka hiyo skul ya moshi akaletwa huku Tanga katika skul flan.

Mimi ndo nilipewa jukumu la kumpokea na kumpeleka skul kurepot. Nilipofika skul kama kawaida nikafata taratibu zote na dogo akapokelewa.
Sasa katika harakati za kumripotisha dogo pale skul nikaonana na madam ni second mistress pale skul.

Ni mwanamke mbichi tu japo kanizid kama miaka miwili (inanifanya nisite kumuoa). Huyu binti niliona kama nimemuelewa hivi lakini sikuwahi na uhakika kama ni kweli au ni macho ya kifisi tu kama ya brother INSIDER MAN kwa akina Asmah, Lucy, Marry na Vicky.

Nilifanikiwa kumuomba namba na alinipa bila ajizi, nikaanza kuwa namtafuta nayeye anarespond. Mwanzo nilikuwa namtafuta kumuuliza maendeleo ya anko wangu dogo anaitwa Gisela.
Nikawa nauliza maendeleo ya Gisela anasema dogo yupo poa na anaonekana kuwa smart na mtu makini (of course yupo poa kichwani). Hii skul ni ya private ada imechangamka kimtindo.

Mawasiliano na huyu madam (nimuite Mage, fake name), tulizidi kuzoeana na mpka ikafikia hatua nikaanza kutupa nyavu. Kifupi nilipambana sana mwisho wa siku madam akajaa na nikaanza rasmi kudate naye.

Huyu Madam Mage yupo smart sana nafikiri ndiyo maana hata kapewa u second mistress akiwa na umri mdogo tu ingali wakubwa kumzidi wapo pale skul.

Huyu Madam Mage tumpe maua yake kabla hata sijaanza kuelezea ni mambo gani special ameyafanya na anaendelea kuyafanya hasa katika hili sekeseke langu na Mercy kwasababu Mercy bado haelewi namimi kuna muda nashindwa kufanya uamuzi sahihi japo Madam Mage shemej yenu na wifi yenu wa faida anaplay part yake vilivyo kabisa.

Nimewawekea picha ya mesej za Mercy alinilazimisha niende kumuona kwao huku akidai kuna mipango madhubuti kama familia wameiweka ili kuhakikisha tunaoana mimi na Mercy na tunaishi maisha bora.
Kwahyo saivi hii vita siyo yangu dhidi Mercy tu bali ni yangu na familia ya Mercy kiujumla.

Mercy amekuwa haelewi japo nimemwambia tayari kwamba nipo na mchumba wangu na tuna mipango ya kuoana. Baada ya kukwambia hiki kitu ndo ni kama nimechochea moto kwasababu anaomba nimpe namba ya huyo mchumba wangu Mage amuombe kistarabu kama mwanamke mwenzake aniache mimi ili nimuoe yeye Mercy akidai kwamba yeye ndo wa kwanza kuingia katika uchumba namimi ila kwa bahati mbaya mambo yakavurugika (siku hii nilicheka sana).

Kuna wakati nawambia Mercy ni kama kachanganyikiwa kwasababu kafikia hatua mbaya eti mimi nitoe namba ya Madam Mage (mchumba wangu) nimpe yeye ili avuruge mahusiano yangu. Hii kwa akili ya kawaida tu ni kitu ambayo ni ngumu na haiwezekani mimi nimpe Mercy namba ya Madam Mage ni hakuna.

Upande wangu mchumba wangu Mage nishamueleza kuhusu Mercy na anaelewa na nimuelewa kwahiyo huwa hata Mercy akituma sms, alipiga cm Mage huwa hamind kwasababu anajua kinachoendelea. Ila cha zaid tu huwa ananisihi nifanye maamuzi sahihi kwani maisha yanahitaj utulivu sana na sio kila kitu kinahitaji uzingatie hisia bali uhalisia.

Mpka saivi mzani umezidi sana kwa Madam Mage kwani nimenotice vitu flan vya msingi sana ambavyo mage anavyo ila Mercy anazingu.
Mfano: Mage anahali flani ya kujishusha sana akikosea au tukigombana huwa anajishusha kitu ambacho Mercy pia anacho ila anazidiwa na mage (Magnitude).

Kuna siku nilikuwa kazini kuna kazi flani ni ya kutumia nguvu ila akili zaidi. Siku hiyo Mage alikuwa kaniomba nimuwekee tsh 50k alikuwa anaongezea anunua cm mpya maana cm yake iliibiwa siku hiyo alikuwa anaenda kununua Samsung note 10 plus gb256 ni hizi used from abroad.

Bajet yake ilikuwa kama 550k hiyo ni Bei ya used sijajua brand new Bei yake ni ngap. Kwahyo aliniomba nimuongezee kama 50k tu nyengine anayo. Nikasema sawa, sas muda huo mimi nilikuwa bize kuifanya ile kazi hafu na Mage katoka ckul anaenda mjini ili kuifata ile cm kwahyo akawa anaharaka sana nimuwekee katika cm yake mpesa. Muda huo namimi nakimbizana na muda niimalize kazi niwasilishe.

Mage alipiga sim na kutuma texts mimi sikuwa na time na cm na nilikuwa dizaini kma nimesahau kama nilitakiwa kumuwekea pesa Mage.
Mage alikasirika akatuma text "DeMostAdmired mbona kama unafanya mambo ya kitoto acha upuuzi". Ile text nilikuja kuiona baadae na nilipoiona nilikasirika sana. Kwasabb nilikuwa nina hasira sikutaka kumjibu chochote kwasababu najua ningemjibu vbaya sana nikamkwaza.

Niliamua kuanza transaction ya kumuwekea ile 50k lakini kabla sijaingia kwenye menu ya mpesa niliona text inaingia ya Mage inasema "am very sorry my love DeMostAdmired najua nimekukwaza ila nisamehe zilikuwa hasira na usiwaze pesa nishaikamilisha na cm nishanunua".

Haya maneno ya Mage yalinifanya nipate furaha isiyo kifani na ndo aina ya wanawake naowapenda yani kakosea, kajua kosa lake na akajiongeza kuomba msamaha kabla sijacomplain. Namimi nilijiongeza nikamtumia 80k badala ya 50k, akanitumia mesej " honey nilikuwa nishakamilisha na cm tayar ninayo hata hivo nakushukuru na nakuomba unisamehe sana kwa yale maneno". Nikamjibu usiwaze I understand and love you so much.

Sasa Mercy kitu hiki hana. Mercy alikuwa nikimuudhi kama nipo kwake alikuwa ananifukuza Sasa hii ni ishara ya dharau, na vijitabia vingine vingi vingi vya ajabu alikuwa navyo japo nayeye anamazuri yake mengi ndomana hata nilimpenda sana.

See you........
Mahusiano yakiwa ya kuombana misamaha sana, hayanogi... Ila pia huenda anakuwa hivyo kwa sababu anahitaji ndoa.. labda utuambie huyo madam ana miaka mingapi
 
Tuendeleee.......

Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".

Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.

DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.

Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.

Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.

SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.

Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.

Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.

Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.

Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.

Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.

Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.

Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.

Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.

Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.

NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.

Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

AHSANTENI 🫶🫶🫶.
Mission complete tunaashukuru kwa Somo zuri....
 
Kuna muendelezo endelea ku scroll chin utazipata episoiji des
Naendelea kuscroll kwenye ushauri Kuna inshu Moja sijaona hapa imezungumzwa

•Nakushauri umtangulize Mungu katika safari yako ....Nikisema umtangulize sio kwenda kanisani yaani katika maombi yako omba Sana kukutana watu sahihi wa kukusukuma au kukuinua n.k

•Mercy kwa kwl Yuko very depressed kwa sasa yaani kama ulivoteseka kipindi anakufanyia maidoido chuo kila rangi haachi kuiona sasa mtaani hii iwe kama alert kwako unapofanya jambo litakaloleta au changia maisha yako tumia akili zaidi na rudia pointi ya kwanza .

•Mwisho,maisha ni fumbo kubwa hauwezi kufanikiwa kirahisi rahisi lazima usote au watu kadhaa wasote Ili upate kilicho bora .Umeaswa mengi na bado utaaswa Ili kufikia kilele chako cha mafanikio maishani,jijenge kwa sasa uwe na kesho ilio bora

Good luck!!!
 
Nilitaka nikustue nikakumbuka husomagi story 🤣🤣🤣🤣🤣kwenye baiskeli nililia sana
Ya huyu Mr lava lava imenifanya nitake kujua alivyo mjinga…!!! 😂😂😂

Eti wanawake tunapenda baiskeli khaaa!! Labda huyo wake na Anitha wa Matonya 😂😂😂
Wengine asitusingizie hatupendi phonex wala mkangafu
 
Ya huyu Mr lava lava imenifanya nitake kujua alivyo mjinga…!!! 😂😂😂

Eti wanawake tunapenda baiskeli khaaa!! Labda huyo wake na Anitha wa Matonya 😂😂😂
Wengine asitusingizie hatupendi phonex wala mkangafu
Mahaba ya mkoani haya baiskeli wanaiona kama rangeee ya Mobeto🤣🤣
 
Ya huyu Mr lava lava imenifanya nitake kujua alivyo mjinga…!!! 😂😂😂

Eti wanawake tunapenda baiskeli khaaa!! Labda huyo wake na Anitha wa Matonya 😂😂😂
Wengine asitusingizie hatupendi phonex wala mkangafu
🤣🤣🤣Eti Anitha una kumbuka vitu vya kijinga sana
 
Natania bana kuchangamsha genge wala sio kweli, kutoa mbusus unafikiri mchezo mchezo 🤣🤣🤣🤣
Kutoa si unatoa tu kwani naondoka nayo, yaani kitumbua nacho ni kitu cha kumnyima mtu kweli, nahuku raha tunapata wote, tena mwanamke ndo anapata raha zaidi ya mwanaume. Halafu PM yako umeifunga dah
 
Back
Top Bottom