Tuendeleee..........
Nianze na upande wa MERCY.
MERCY alikuwa anasisitiza sana anataka kuja nilipo (Tanga) ili awe karibu na mimi lakini mimi nilikuwa namkataa na kumsisitizia kuwa sina mipango naye hata kidogo na Nina mchumba wangu tayari.
Baadae ni kama juhudi zake zilionekana kufifia na nikaona ni kama ameridhia na hali. Mimi huku na Mage mambo yakawa shwari tu na mipango ikawa ni ile ile mwez wa saba ambao ndo huu tunaanza kuishi pamoja rasmi kama mume na mke.
Ilipita miezi kama miwili toka Mercy akae kimya then akaja kunitafutaa tena.
Aliponitafuta akaja na malalamiko mengi sana mara oooh wewe bado haujanisamehe unakinyongo na mm.
Nikamuliza kwanini unasema hivo? Kajibu yani mambo yangu hayaendi.
Nikamuliza mambo kama yapi? Akasema ngoja nikwambie ukweli, baada ya kuona wewe haueleweki nikaamua kurudi kwa Dokta na tayar nina ujauzito wake mwingine. Nilishusha pumzi nikamshukuru Mungu kwakuwa hakuuruhusu moyo wangu umkubali Mercy na kumuoa awe mke wangu kwasababu ni dhahiri ningekuwa nimepoteza dira katika maisha yangu.
Nikamuliza sasa lawama unazozielekeza kwangu zinakuja vipi? Akanijibu kwamba anahisi bado ninakinyongo na ninamsemea vibaya sana ndomana hana hali nzuri katika maisha yake upande wa mahusiano.
Akanambia kwamba yeye na Dokta wamevurugana vibaya na ni ugomvi kila siku japo hawakuwa na mahusiano rasmi ila kaumia sana kuona hana furaha katika maisha yake.
Akaniomba kwamba anajua kabisa siwez kumuoa ukizingatia tayar anaujauzito wapili kutoka kwa Dokta, akaniomba nimsamehe na niachilie nisimseme vibaya ili aishi kwa furaha.
Hapa nilikuja kugundua Mercy kachanganyikiwa na maisha yamemchosha kwasababu maneno alokuwa anaongea ni dhahiri niliona tayari kachanganyikiwa.
Of course kuna siku katika mawasiliano na Mercy nilimtumia text "what goes around comes around" akanambia siyo vizur hayo maneno ni kama laana kwake.
Sasa ni kama alishikilia hayo maneno na anadhani yale maneno yanahusiana na mikanganyiko inayoendekea kati yake na Dokta wake.
Honestly sikutarajia kama Mercy atarudiana tena na Dokta na ni dhahiri sasa nimeamini mwanamke ni mtu wa kuishi naye kwa akili sana maana haeleweki kabisa.
Nashukuru sikuchukua maamuzi ya kumuoa, nawashukuru pia my best friend Mbwambo kama mnamkumbuka alinisisitizia sana nisimrudie Mercy lakini pia Merry kama mnamkumbuka kipindi Mercy karudi kwangu na mm kuamua kumuacha Merry na kurudi kwa Mercy, Merry alinitahadharisha nisije kufanya makosa nikamuoa Mercy nitajuta.
See you ........