GEMBESON
JF-Expert Member
- Apr 15, 2012
- 1,463
- 3,193
Moyo wako tayari umeshaachia na kukubali kupoteza. Hii ni hatua nzuri ya wewe kusonga mbele na maisha mengine kuendelea.Mercy haniendeshi kama zamani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Moyo wako tayari umeshaachia na kukubali kupoteza. Hii ni hatua nzuri ya wewe kusonga mbele na maisha mengine kuendelea.Mercy haniendeshi kama zamani
Kila siku asubuhi ananisalimia na jioni ananipa pole ya kazi lakin mimi sina tena ratiba nayeMoyo wako tayari umeshaachia na kukubali kupoteza. Hii ni hatua nzuri ya wewe kusonga mbele na maisha mengine kuendelea.
Unakatwa mwenyeweUnakatwa na pididy!! We kijana amekuchapia demu na mtoto wake utalea
Hii ni kweli mzeeKitu ambacho wanaume wenzangu wengi hawakijui, hasa hawa wa kisasa, ni kuwa: mwanamke atakusamehe makosa yote isipokuwa la kuwa dhaifu. Ukionesha udhaifu tu, umekwisha. Atakuadhibu squarely, hautakuja kumsahau.
Pole sana mzeeTuendeleee.......
Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".
Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.
DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.
Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.
Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.
SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.
Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.
Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.
Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.
Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.
Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.
Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.
Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.
Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.
Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.
NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.
Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.
AHSANTENI 🫶🫶🫶.
😂😂dah ila we jamaa bhanaAmuweke mercy bench asimuache, kwasisi tulioa tunaelewa umuhimu wa kiwa na reserve, sometimes ndani kuna wakati hapakaliki au kuna wakati unakuta huyo mwanamke anataka kuolewa kwa hali na mali, kwa hiyo akifika ndani anabadilika.. so ukiwa na reserve hata ukimpiga chini uliyemuoa ukirudi kwenye ubachelor unakuwa na pa kuanzia
Hebu acha wivu wako mtoto tulia uendelee na chai licha ya kuwa inaumaNa mi imeniuma hata ni mwanamke mwenzetu karudiwa ila alikurupuka sana kwa huyo dokta, natamani nimrukie kichwa 😂😂😂
Na hutawamaliza kila mmoja ana mapungufu yake stiki kwa mzimu wako mmoja uzimue😂😂😂😂 Matukio sinaga nikiona mwanaume haeleweki chap namuacha sitaki hekaheka mie
Nashukuru kwa kututambua hivyoMpo vizuri sana 😂😂😂
inachanganya bali wewe ni kimeo kimeo kabisaHizi ni meseji Mercy alinilazimisha niende kwao leo nirudi kesho kutwa. View attachment 2959998
Kesho nitaleta muendelezo wa maelezo muone jinsi dunia inachanganya haieleweki.
Una wivu sana tena wa kitoto🤣🤣🤣🤣 vibaka wa sabasaba na chamwino sio mchezo mchezo..!!! Moro napamiss sana!!
Halafu ndio kipindi game limeanza kumkataa wakaona nao wamalizie kumpotezea kabisaaa!!
Kuna nyingine hiyo nilitoroka hostel nikaenda club nipo na shosti yangu na bwana ake manager wa kampuni moja ya mtandao wa simu, ndio alitusponsor basi nimevaa high heels zangu najiachia mwenyewe kwa stage huku nimekunywa reds zangu nimewaka…!!
Mara nikamkanyaga mdada walikuwa wanacheza na mpenzi wake pembeni yangu..!!!
Yule dada akapanic akanisukuma weeee na zile heels nusu ning’oe meno 🤣🤣🤣🤣
Nikadondoka kile kisketi kikapanda juu chini kote kunaonekana, niliinuka kwa hasira nikavua konkonko nikamfata yule dada nimtwange navyo hapo reds ndio zinaongea, nimemkaribia nikashangaa jamaa yake kanidaka na bonge la mtama 🤣🤣🤣🤣
Nikaanza kutukana akaja rafiki yangu naye akanunua ugomvi. Lakini nikawa namshangaa mbona haonyeshi cheche!! Kumbe kuna kitu alikutana nacho. Akapigwa butwaa
Nikaona ujinga ngoja nikapambane mwenyewe, nikabeba chupa sasa liwalo na liwe kwenda kumchoma nayo yule dada aiseee!! Hapo kwanza ncheke 🤣🤣🤣
Kumbe yule mdada ni dada yangu naye alitoroka home akaja na bwana club. Hasira zilizidi mara mbili nimeshindwa kukamilisha kisasi changu. Akaanza kunipoza na kunigombeza kwann sisomi nahangaika kwenye maclub usiku…! Hapo kiuno kinauma balaa na ule mtama wa yule bwanaake😏😏
Yule bwana ake baadae nilimfanyia figisu moja hiyo mpk wakaachana ila hakujua km ni mimi nilitengeneza ule mchezo mpk leo.
Ila bado kinaniuma mpk kesho.
Dogo mpe namba yako mage yake ichukue ayamalize kwanza hayaTuendeleee..........
Kwanza kabisa kuna kitu ni kama ninakihisi, ni kwamba ninahisi Mercy aliwambia kwao kwamba mwanaume mwenye mtoto ni mimi na siyo Dokta.
Nahisi pia kawadanganya kwamba nimekengeuka sitaki kumuoa mtoto wao kwasababu sasahivi hili sekeseke hadi wao wazaz wa Mercy wameingilia kati. Na bila shaka kama Mercy angekuwa kawambia ukweli kwamba yule mtoto sio wangu ni wa Dokta basi wazazi wangedili na Dokta na siyo mimi.
Mercy namuona ni kama anatumiwa na shetani kunivurugia mambo yangu.
Mercy amepanga mipango ya kuhamia Tanga mahali nilipo ili awe karibu na mimi. Nilijaribu sana kumpiga biti nyingi za makatazo juu ya mpango wake kwani ataniharibia mipango yangu na Mage na ukizingatia Mage tayari tupo naye vizuri sana yani mapenzi ni moto sana saivi.
Mage ni mwanamke mzuri na mpka sasa siamini ni kwanini nilimkuta Mage akiwa single Hana mtu najiuliza je alikuwa anawakataa watu au alikuwa hatongozwi maana Mage ni wife material haswa. Ila nachokiamini Mage hakuwa single ila kaamua kuweka utoto pembeni na kuwa na mimi 100%.
Nahisi pia ni mpango wa Mungu Mage kuwa namimi kwasababu amekuja wakati sahihi wakati ambao nilikuwa nahitaji sana mtu wa karibu ambaye ataridhia kuwa namimi no matter what.
Yale matatizo ya moyo niliyoyapataga
nahisi bado kwa kiasi kidogo yapo bado japo kadri siku zinavokwenda yanazidi kupotea na nazido kuimarika.
Kuna muda nahisi hasira kwa vitu vidogo vidogo, pia kuna muda nadhoofika moyo unakuwa unapiga kwa nguvu mpka nikiweka kiganja juu juu tu katika sehem ya moyo nakuwa nafeel moyo unavopiga kwa nguvu Sasa hii hali inanifanyaga nidhoofike na pia nakuwa na shorten breath.
Mage tayari anafaham hali yangu halisi na ananipa kampani ya dhati sana mpka naona kama vile ni special from God.
Kuna siku nipo na Mage nakumbuka ilikuwa siku ya j pili weekend maana Mage anakuwaga na nafasi ya kuja kunitembelea siku za weekend.
Siku hiyo tupo bed tunapiga stors meseji ya Mercy ikaingia "DeMostAdmired mimi nawewe tulipanga mengi makubwa, kilichotokea mimi kukusaliti mpka kuzaa na Dokta ni kama ajali tu na sikufanya kwa kukusudia naomba unielewe. Dokta nimeshampiga marufuku hanitafuti tena na Hana kabisa mazoea na mimi. Nisamehe kila siku nakuomba msamaha siyo kwamba sitongozwi natongozwa ila nahitaji kuolewa nawewe niambie nini nifanye ili urudishe moyo wako kwangu mimi nipo tayari".
Hii mesej hata Mage ilimpa mashaka japo tayari ameshamzoea Mercy na vimbwanga vyake lakini siku hii Mage alisimama akanambia " baby huyu mwanamke sasa naona anavuka mipaka, mimi sipo tayari kuona unatumiwa mamesej ya kubembelezwa namna hii na wewe ni binadamu kuna kipindi kitafika utaanza kuregea na kuanza kumpenda huyu Mercy"
Mage alinambia either tubadirishane laini yeye atumie yangu namimi nitumie yake au lah basi nivunje hii yangu nisajili nyengine ili Mercy asinipate tena.
Niliona option ambayo kidogo ni nzuri ni hii Option ya pili japo niliwahi kubadirisha laini lakini alipata namba yangu kupitia watu tulomaliza nao chuo ndo walimpa namba yangu na wembe ukawa ni uleule.
Nilimuahidi kwamba atulie mimi ni mwanamume ninaakiki timamu nafahamu Mercy siyo mtu mzuri kwahiyo asiwe na wasiwasi kabisa.
Alikubali japo kwa shingo upande
Siku hii Mage aliwaka sana mpka nikaona kama vile Mercy anaenda kuniharibia mipango yangu na Mage kwasababu mage tayari ameridhia tuanze taratibu za kutambulishana ili tuanze kuishi pamoja kama mume na mke na hapo baadae tufunge ndoa. Hii kitu bado naona ni mapema kwasababu ndo kwanza hata mwaka hatujamaliza.
See you........
Id yako ya mwanzo ipi? 😂😂😂Hebu acha wivu wako mtoto tulia uendelee na chai licha ya kuwa inauma
Wivu wa nini mahi?Una wivu sana tena wa kitoto
Chai gani? Watu wa JF mnashangaza sana haya nambie unataka nifanyej ili uamini hii sio chai?Hebu acha wivu wako mtoto tulia uendelee na chai licha ya kuwa inauma
Mercy kashashindwa Hana tena nafas kwangu. Na naona kama vile nilichelewa kumpata Mage au mtu kama MageDogo mpe namba yako mage yake ichukue ayamalize kwanza haya
Baadaye yakiisha utakuwa vzr, usidhani kuwa mage naye hatongozwi atakuja achoke na skendo zenu aingie kwa mtu mwingine akuache