Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Ok hapo alipotaka kutoa mimba ili muanze Tena upya hapo kwangu mwanamke huyo napiga chini hapo hapo......

Sipendi na huwa simkubali mwanamke anayetoa mimba.... Labda kuwe na biological factor! Nje ya hapo ni mwiko kwangu!

Pole kwa yaliyokukuta! Jitahidi kufuata ushauri wa watu humu..... Utakusaidia kwenye penzi jingine na kuilinda manhood yako kwa ujumla!

Nikutakie kila la khery! Brother
 
Pamoja
 
mkuu funguka kwanza hapa kuhusu malez ya kiumen/toa codes kwamba alizngua wap au information gan muhmu ktoka kwa ding yake alizikosa. wahanga hapa niwengi. karibu.
 
mkuu funguka kwanza hapa kuhusu malez ya kiumen/toa codes kwamba alizngua wap au information gan muhmu ktoka kwa ding yake alizikosa. wahanga hapa niwengi. karibu.
Ni ngumu kidogo kuweka kwenye maneno,

Malezi ya DINGI au mlezi wa kiume humfundisha kijana kujitambua, kujipa kipaumbele, kuwa na uthubutu, na kusimama imara katika nafasi yake kama mwanaume. Pia, yanajenga ujasiri wa kufanya maamuzi magumu inapobidi, hata kama maamuzi hayo yanaweza kuathiri wengine. Baba mara nyingi hufundisha nidhamu ya kiakili, ikiwemo kudhibiti hasira, kuwajibika kwa matendo yako, kushinda hofu, na kusimamia hisia katika hali ngumu. (Mwamba alikuwa anaendeshwa na hisia mwanzo mwisho)

Kwa upande mwingine, mama au mlezi wa kike hufundisha jinsi ya kujenga na kudumisha uhusiano wa karibu wa kihisia. Mama huchochea huruma, kujali jamii inayokuzunguka, na mshikamano wa kifamilia. Pia, husaidia mtu kuelewa na kuthamini mahitaji ya kihisia ya wengine, jambo ambalo ni msingi wa mahusiano mazuri

ukibahatika kupata malezi ya pande zote mbili kuna chances za mtu kuwa mtu bora,mwenye uwiano wa kiakili na kihisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…