Endelea..................
Nilipomuliza kuhusu Dokta niliona kama Mercy amestuka kidogo lakini akakaa sawa akanambia Dokta toka siku ile apige tupo wote ukakata hajapiga wala kutuma text tena.
Nilikubali nikamwambia sawa haina shida, basi tukaendelea na stor zingine.
Baadae nikiwa magetoni kwangu nikajua kabisa kwa Mercy kustuka vile basi Dokta kashatuma pesa na Mercy kaisigina. Na kama Mercy kaamua kula buyu basi tayar hapa sina changu.
Magetoni nilikuwa na kisabufa changu na kama nilivowambia napenda kuimba na napenda muziki. Basi nikafungulia sabufa sauti ya chini nakumbuka niliweka wimbo wa Alikiba "Dodo" naupenda sana huu wimbo.
Baadae usingizi ulinipitia nilikuja kuamshwa na cm ya brother alinichek tukaongea tulipomaliza nikaona kulikuwa na text ya Mercy alinitumia "baby mambo" ilikuwa kama saa tatu usiku, nilimpigia tukaongea then tukaagana maana nilimwambia toka mapema kwamba sitakula jioni najihisi kushiba.
Ijumaa ile hatukuwa na mtihani kwahiyo tulikuwa na time kubwa kujiandaa na papers zilizokuwa zimebaki. Mimi na Mercy tulikuwa na jumla ya masomo 8 semester ile na wiki ya kwanza tulifanya mitihani mi5 ikawa imebak 3.
Sambamba na haya tulikuwa pia tunafanya research kumbuka mwaka wa 3 pale chuoni kulikuwa na research na ni compulsory.
Kwahiyo hiyo ijumaa tulijikiza sana katika kuedit edit researches zetu.
Ndugu zangu Mercy ni binti niliyempenda sana kuna watu wanasema mimi ni mshamba wa mapenzi ila najua hawajawahi kukutana na mtu wakampenda vilivyo.
Mercy ni binti mstaarabu, mzuri na hakuwa na mambo mengi ndio maana Uzi unasomeka "DAKTARI ALIFANYA NIKAMPOTEZA MCHUMBA WANGU MERCY".
Ijumaa ile mchana kutwa nilikuwa na Mercy kwangu maana nilimuita ili pia anisaidie saidie usaf magetoni kwangu.
Kumbuka Mercy kashakataa kwamba Dokta hamtafuti tena. Nikawa sina jinsi na nikaona hili ndo gap la kumuacha Mercy aamue anachotaka kuhusu Dokta maana nilikuwa na uhakika kabisa bado anamawasiliano na Dokta.
Weekend ile Mercy alinambia anahitaji kunitoa out. Sikushangaa sana kwasabb tulikuwa tunatoka toka sana out hasa weekend nilikuwa napenda kumpeleka mahali tunapata vinywaji na nyama kimtindo then tunarud geto.
Siku hiyo Mercy kanambia anataka kunitoa out lakini nikawaza Mercy hii pesa isije ikawa ndo ya Dokta yani anataka hela ya sponsor anitolee mimi out.
Nikawaza kumuliza pesa kapata wapi ila nikaona kama nitazingua ikabid nile buyu tu niugulie ndani.
Ilikuwa j moc saa mbili usiku tulienda town kwenye ilikuwa ni lounge x pale town, kulikuwa na watu wengi tu.
Baada ya kufika pale tulikaa sehem tukiwa wawili then kwa mbele yangu ila nyuma ya Mercy kulikuwa na watu wawili ke na me kuangalia vizuri namuona mtu kama Mercy fek.
Kumtazama vizur alikuwa ni yeye na nilipomuangalia yule alokuwa naye sikumtambua lakini inaokana kabisa yule alikuwa ni mpenz au danga lake.
Hapo hapo nikapata chance ya kumuaminisha Mercy kwamba yule hakuwa mpenzi wangu bali ni binamu yangu ila anamazoea ya kijinga na sikuwahi kushiriki naye tendo.
Nilimsogelea Mercy nikamwambia geukq unamuona yule bint nyuma yako, akaitika kamuona nikamwambia ndo yule alotuma ile text na huyo unayenuona naye ni mpenz wake wana miaka mingi sana kwenye mahusiano kwahyo ulivokuwa unadai kwamba ni mpenz wangu ulikuwa unakosea. Na kama hauamini twende wote mpk pale walipo tukawasalimie, Mercy akasema haina shida tufanye yetu tu niwe huru na niwe na amani.
Tuliagiza tukatumia, tulikaa kama masaa mawili ilipofika saa 4 na nusu usiku tukapanda boda tukarudi. Tulipitisha Mercy kwake then akanipeleka kwangu.
Nilovofika kwangu nikakumbuka kesho ni j pili kwahyo nikaamua nimpigie Mercy nimulize kama ataenda church au vipi.
Nilipompigia cm yake ilikuwa inatumika kuchek saa saa5 na madakika usiku.
Duh nikashusha pumzi, Mercy muda huu anawasiliana na nani. Nikampigia tena bado busy nikazidi kupatwa na wasiwasi mixer hasira. Baada ya muda nikaona cm inaita alikuwa ni Mercy anapiga nikapokea, sikumuliza alikuwa anaongea na nani nikakaza tu, akajiongeza akasema alikuwa anaongea na rafkiake walisoma wote advance nikasema haina shida.
Kiukweli nilikuwa nishaanza kuvaa ujasiri ya uvumilivu nikawa nimepunguza kumchunguza Mercy nikawa bize na mambo mengine kabisa.
Kesho yake tukaenda church, ilivofika saa7 mchana tulikuwa tushatoka wote nikaamua kwenda kwa Mercy ili tufanye mpango wa msosi.
Alipika tukala then tukaanza kupitia researches zetu na past papers za mtihan wa j3 kwasabb kulikuwa na paper moja Moja mpka mwsho wa UE na yalikuwa yamebak masomo ma3.
See you..............