Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Huyu dogo atakua alimfata Dr kibabe, kwamba achana na kumfatilia demu wangu, huwezi kumpata, demu ananizimia sana Mimi, utapoteza tu muda wako ila angeenda Kwa adabu. Akamwambia bro najua wewe una Hela na unaweza kufanya lolote Kwa Mercy ila mdogo wako nampenda Mercy na Nina mpango wa kumuoa, naomba niachie bro. Angemuelewa Kwan sisi wanaume ni waelewa sana hasa kama ndo unaanza tu kumfatilia demu Bado hujapiga. Naamini approach yake Kwa Dr haikua Nzuri na ndio maana Dr alipofanikiwa akaanza kumtumia sms za dharau maana alitaka kumuonesha dogo hakuna kinachoshindikana
Dogo wa Mecy wangu(Immaculate) alinifuata kwa style hio, actual alinifuata kazini nikamuomba anisubirie till lunch break tukaenda nae steers makumbusho tukagonga lunch tukamaliza, dogo akaongaea kwa uchungu mkubwa kama mwanaume nikamuelewa as pia nilikua na recover toka kwenye machungu divorce. Dogo tuka shake hand na akapromise hata nisumbua au kunitafuta tena. Na nikweli tangu 2012 sijawah muona au msikia tena kipindi hicho wapo 2nd year Mzumbe. Mecy wangu once in a while huwa tunasalimiana
 
Dogo wa Mecy wangu(Immaculate) alinifuata kwa style hio, actual alinifuata kazini nikamuomba anisubirie till lunch break tukaenda nae steers makumbusho tukagonga lunch tukamaliza, dogo akaongaea kwa uchungu mkubwa kama mwanaume nikamuelewa as pia nilikua na recover toka kwenye machungu divorce. Dogo tuka shake hand na akapromise hata nisumbua au kunitafuta tena. Na nikweli tangu 2012 sijawah muona au msikia tena kipindi hicho wapo 2nd year Mzumbe. Mecy wangu once in a while huwa tunasalimiana
You did as a bro
 
Hivi wewe DeMostAdmired na huyo dakatari mnapata wapi nguvu ya kugombania mwanamke mmoja, yaan mimi ni huu uvivu wangu wa kutongoza wanawake, nianze kugombania mwanamke mmoja aisee naona kama ni kazi ngumu kupita maelezo.
Kutongoza tuu mwanamke nahic kama ni tiresome process, sembuse kugombania.

Kwanza nikiona tuu mwanamke ana mtu mwingine interest yote inapotea, pia nikiona mwanamke niliyokuwa nae ana interest na wanaume wengine interest huondoka(hapa nazungumzia ku-reply message za wanaume ambao anajua kabisa wanamtaka), sasa nyie wanang mkoje????

Ningekuwa wewe baada ya kupata ushahidi wa usaliti, ningeenda kwake kiroho safi tuu, ningechukua vitu vyangu vyote, ningehakikisha na yeye hajaacha kitu kwangu, then ningekata mawasiliano, sio kum-block wala sio kutopokea simu zake, ni kukaa tuu kimya, simpigii na sijibu text zake, akipiga napokea namsikiliza, akituma message sijibu, akiniuliza shida nn namjibu "Niko sawa".

Najua inauma lakini if a woman doesn't want to be what you want her to be, don't force or cry about it, just move on, yes it's going to hurt but that's life, life is not supposed to be easy, especially when dealing with emotions, kuna muda ndio utam-miss na uta tamani umpigie lakini utakapo fanya hivo utashusha dhamani yako, wanaume tuelewe kwamba mwanamke aliyekusaliti ukamsamehe hatakuona una upendo au mvumilivu atakuona mpumbavu na huna uanaume kwasababu mwanaume wa kweli hasamei usaliti, unapomsamehe au kumchekea au kumkalia kimya mwanamke aliyekusaliti ni kama vile unamwambia "Mimi sio mwanaume" na hio kitu naona wanaume wengi wanafanya.

Mwanamke aliekusaliti ukaachana nae pamoja na yeye kuomba msamaha hata kutoa machozi yote atabaki anakuheshimu milele, lakini mwanamke aliyekusaliti na ukamsamehe atabaki anakudharau milele.
Sawa bhna
 
NIPO KANISANI LAKINI NIMETOKA KIDOGO NJE NIWAIPANDISHIE EPISODE MOJA.

Tuendeleee.......

Hapo nilianza kumuona Mercy mtu tofauti sana na mwanzo kwasababu sikutarajia kama angefanya ule upuuzi.

Basi nikajikaza tu huku nasikiza mziki, nakumbuka nilikuwa nimeweka playlist ya nyimbo za FireboyDML, (need you, what if I say, energy, gbas gbos, champion, vibration, wait and see n.k).
Kuchek saa ni saa nane na nusu Mercy bado hajanichek nikaona namimi nikaushe tu mpka anitafute. Kichwani zile mesej za Dokta zilikuwa hazipungui muda wote zinajirudia. Nikamkumbuka mpka yule bro wa tanapa japo nikaona hata angekuepo msaada wake isingeweza kumrudisha Mercy kwangu.

Siku ile kusemazaukweli nilipanga niachane na Mercy nijikite katika masomo yangu nitoke na GPA nzuri. Kidogo mara cm yangu ikaita kichek ni Mercy, nikapokea akanambia niende kwake tyr kasharud. Lakini nikamwambia sitakwenda muda ule nitaenda jioni.

Alijistukia akaniuliza vipi kuna shida nikamwambia hakuna tatzo.
Nilipanga nisiende muda ule kwasababu nilikuwa ninahasira sana na Mercy tungejikuta tunagonbana tu hafu ingekuwa jau.
Basi jioni ilipofika nikajikusakusanya kwenda kwa Mercy, nilimkuta anachezea cm yake iphone seven ya gold mpauko. Alikuwa keshapika ilikuwa na wali na samaki, tukavunga kwanza tuvute muda ndo tule.

Nilikiamsha nikamuliza kwanini alikuwa hapatikani na kachelewa sana, akajibu cm ilizima chaj na kwa anko wake kunashida ya umeme kulitokea shot. Nikajikaza kumuelewa lakini nikawa nawaza nimuoneshe zile texts za Dokta ila nikaona haitasaidia ila itabomoa nitamfanya Mercy aniache mazima direct maana nilikuwa cna uhakika kama ile battle ningeiweza na kumfanya Mercy amuache Dokta.

Hapa nikaanza kujiona mimi ni mpenz mtazamaji hata show alikuwa ananipa kuniridhisha tu ndo jinsi nilivokuwa nahisi.
Siku zilisogea semester ikasonga vitimbwi vikaendelea. Hakika Dokta alimteka Mercy kwa kutumia pesa zake, ilifika hatua Mercy akawa ananiomba pesa nyingi ili nishindwe kumpa then aanze complain. Nikaona kama ni kitu cha ajabu maana

Mercy hakuwa anaomba pesa ndefu kias cha kunikomoa. Mwanzo alikuwa anaomba labda pesa ya kusuka alikuwa ananitajia kiasi labda naomba elf15 nikasuke, labda elf10 ya kitu flani, elf20 ya jambo flan na haikuwa mara kwa mara.
Sasa ghafla nikakutana na ombi la laki moja anasema anahitaj kubadir cm auze ile aongezee anunue kubwa zaid. Nikamwambia aniwait kidogo boom likitoka nimpe hiyo pesa aliitikia kwa unyonge sana na kama dizain ya kukomplain kidogo. Nikaona huyu kashaingiwa na tamaa baada ya kuonja utam wa penz la pesa la Dokta. Nikaona kabisa huyu mtu simuwez kwasasa na kifupi sio level zangu.

Nikaanza kupanga mikakat ya kujiondoa kwake taratibu lakini nikawaza nikusanye evidence juu ya mahusiano yake na Dokta ili siku akiona nimejitoa niambatanishe zile evidence ili aone makosa yapo wapi. Nikapanga kumchek Mercy feki ili akikutana tena na Dokta apige picha chats zote then anitumie tsap. Hakuwa na noma yule dem plus alikuwa anahitaj rungu langu mpka kesho bas hakunipinga akaona pia ni fursa maana yalikuwa ni mazingira ya kuandaa kuachana kwetu mimi na Mercy og.

Huku mimi nikaanza kumkataa Mercy taratibu, nikawa sometimes nampitia na baiki siku nyingne simpitiii, somedays naenda kula kwake siku nyingine siendi yani nikawa nafanya vile ili siku tukiachana niwe nishazoea.
Siku zilienda tukawa tunaishi hvohvo kwa kuforce ilifika muda mawasiliano yakapungua kwa kiasi kikubwa. Mercy alikuwa anamuliza shida nini namimi namjibu hapana nipo sawa kabisa asiwaze. Lakini nikawa namuona kama mnafiki kuuliza kitu anachokijua.

Siku moja Mercy alinitumia ujumbe kwamba anaenda kwa anko wake na atalala hukohuko maana mamaake mzaz kaja kwahyo Hana uhakika kama atarudi siku ileile. Nikakubali lakini kinawa najua kabisa Mercy kanidanganya ila anaenda kuliwa.

Nakumbuka ilikuwa ni weekend, nikapata wazo nimwambia Mercy fek amchek Dokta aombe mtoko siku ile. Nilipomchek akanijibu alikuwa na mpango huo yeye binafs kabla hata ya mimi kuwaza hilo na alikuwa ashamuomba watoke na Dokta kamjibu siku hiyo atakuwa yupo bize sana na hatokuwa na muda, tayari nikahitimisha Mercy anaenda kwa Dokta. Nikarelax nikaona Haina haja ya kuendelea kuumia nikawa nafanya mambo yangu tu.

Ndugu yangu hakuna kitu nilikuwa nacho makini kama kusoma, Mercy aliniumiza sana lakini sikuwahi kufeli hili ndo naloshukuru mpka Mercy mwenyewe na marafiki zake wakawa wananiita mimi mchawi wa masomo. Kwasabb sikuruhusu mambo yangu yaingiliane na masomo yangu.

Asee siku Ile Dokta alituma tena mesej "dogo vipi umeshindwa kumdhibiti Mercy". Nikaona Dokta sasa hata kama ni ROHO mbaya kazidisha na hiyo sas ni arrogance. Nikamjibu kistarabu tu "tumia muda wako vizur enjoy" then nikakaa zangu kimya.

Seeee you.......
dokta alipokutumia hio meseji ungemjibu '"nina ubao hatari, fanya kutuma 50 hapo nikapige mdudu......."

mtu anakuchukulia demu wako alafu unaendelea kumwonyesha umekua mnyonge?
 
"NDUGU ZANGU NIMEPIKA CHAKULA NI KITAMU SANA HAPA KARIBU LUNCH"


Tuendeleee....

Hii ni experience ambayo sidhani kama nitakuja kukutana nayo tena katika maisha yangu maana nilijikuta kama nipo dunia nyingine kabisa ilojaa kila aina ya tabu na mateso. Na nilijifunza mengi na ilinifanya niwe makini lakini pia mvumilivu katika ulimwengu wa mapenz na vibweka vyake

Kuna muda nilikuwa napatwa na mawazo ya kijinga nikawaza nimuwinde Dokta nimpige hata na mawe lakini nikawa narelax nakuyapotezea hayo mawazo ya kijinga na kitoto.

Mercy alinichek ilikuwa ni mida ya sa12 jioni akanambia hatoweza kuja atalal hukohuko, ilikuwa ni kwa mesej nikamjibu short "poa" naye akatuma mguno "mh" sikumjihu nikapotezea.

Sikumtafuta tena mpka kesho ikafika, ilikuwa ni j3 niliamka nikajiandaa kwenda chuo, chakushangaza nilipofika chuo nikamkuta Mercy tayar kashafika chuo. Nikamsalimia basi tukaendelea na pindi.

Sasa kuna mshikaji wangu huyo alikuwa anapenda kunipasua sana kuhusu Mercy anasema Mercy nawewe hamuendani na atakuumiza tu. Huyu jamaa alikuwa ni wale wakujichetua alikuwa anaropoka ropoka sana na mautani mengi.

Alipokuwa ananambia vile sikuwa naweka naye ligi nilikuwa namuacha tu aongee mpka aridhike. Sasa baada ya kipindi jamaa akanifata anaitwa James huyu mwamba, jamaa kanifata akanambia leo Mercy kashushwa kwenye gari nikastuka sana nikamuliza gari aina gani, akanijibu ni X-trail. Nikakumbuka siku ile tulivoenda na bro kuongea na Dokta pembeni kulikuwa na Nissan X-trail basi nikajionea huruma nikaishiwa nguvu.

Nikawaza inamaana Mercy kaamua kuonesha kabisa kwamba haina haja tena ya kuficha ujinga wake.
Baada ya kumalizana na James nikaona liwalo na liwe ngoja nimulize Mercy, nikamfata alikuwa back bench anapitia pitia cm yake nilivofika nikakaa pembeni yake, nikamuliza Mercy chuo umefika sangap? Akasema alipata lift ya anko wake alikuwa anaelekea mahali karibu na chuoni kwahyo akampitisha chuo. Nikamuliza hiyo gari ilokuleta unauhakika niya anko wako? Akanijibu ndio ni ya anko. Nikajikuta nalopoka "Ile gari ni ya Dokta na ndiye alikuleta chuo Leo".

Mercy alivosikia vile nahisi akapata loop hole ya kuniingia akajibu ndio ni yeye hafu akapenya kwenye desk pale akapita akasepa. Akasema tena ni Dokta ndio si ndo ulitaka kuambiwa hivo ili uridhike, nikainama kwenye desk huku natoa machozi. Hii ni kweli siwez vunga nilitoa machozi lakini nilikuwa nimeinama kwenye desk na kitambaa najifuta futa. Uzuri palikuwa na watu wachache sana na walikuwa bize na mambo yao sidhani kama waliosikia ule mzozo wangu na Mercy.

Baada ya pale nikakumbuka Mercy fek alikuwa ashanitumia zile pics za chats nikaunganisha na zile Dokta alikuwa anatuma basi nikamtupia Mercy kupitia whatsap. Nikiambatanisha na ujumbe "hivi Mercy nini kimekupata? Inamaana umetekwa na pesa za Dokta kumbuka hizo pesa ni zake na familia yake atakuja kuharibika maisha huyo". MERCY hakujibu chochote, aliniblue tick tu ikabid nimtafute rafiki wa Mercy anaitwa Recho nikamsihi aongee na Mercy kwani anachokifanya sio kizuri ukizingatia tuoo semester ya mwisho ataniharibia masomo.

Recho alikubali akaongea na Mercy lakini Mercy hakumpa majibu ya kuridhisha kifupi hakuonesha wazi kwamba yupo wa Dokta au yupo kwangu majibu sahihi alibak nayo Mercy mwenyewe.
Nikawa namtumia mesej Mercy lakini alikuwa hajibu sm hapokei nilifanya vile kwa siku mbili mfululizo nikaona ni bora nijikaze nitulie nione whats next.

Hali ilizid kuwa mbaya kwani Mercy alizid kuwa chui kwangu, nakumbuka kuna siku tulikuwa kwenye kimbweta na washkaji zangu wakiwemo Mbwambo na James tulikuwa tunapitia pitia researches zetu. Ghafla tukaona gari kwamba mbali kidogo kama mita mia hivi ilikuwa ni gari ya Dokta kwan nilikuwa naijua kwakua gari ilikuwa mbali basi tulioiona tulikuwa ni mimi na Mbwambo tu kwan tulikuwa tumekaa kuelekea uelekeo sawa, na huyu mshikaji alikuja kuwa msaada sana kwangu hapo baadae hakika ni rafiki mzuri kwangu.

Kuangalia vizuri tulimshuhudia Mercy akishusha katika Ile gar akasepa zake venue, nilitaka nimchek Mercy nimwambia kwamba anachofanya sio vzr nilimshirikisha Mbwambo na nikamwambia kila kitu kuhusu hali ilokuwa inaendelea kati yangu na Mercy.

Mbwambo akanambia acha usimtumie mesej act kama hujamuona kwani Mercy tyr akili yake haipo kwako kwahyo hata ukifanya vile utajichoresha tu na atakuona unateseka sana na atajiona mshindi kwahyo wewe mute tu as if hujaona chochote.

Siku ile ilipita na ilikuwa kama siku3 mfululizo bila kuongea wala kukutana na Mercy.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kutoka kwa matokeo ya semester ya1 ya mwaka wa3, matokeo yalivotoka Mungu mkubwa mimi sikuwa na sup na nilikuwa na GPA ya 4.1 Mercy alikuwa na sup moja ya analytical chemistry na GPA ya 3.9, Basi nikaona kwa sabab sijafeli inatakiwa nikaze japo kwa ugumu hivohivo ili nisipate sup ile semester ya mwisho.

Yale mateso kutoka kwa Mercy yalianza kuniathiri kiakili na kisaikorojia pasipo mwenyewe kustuka maramoja.

See you ........

===
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
 
Hivi wewe DeMostAdmired na huyo dakatari mnapata wapi nguvu ya kugombania mwanamke mmoja, yaan mimi ni huu uvivu wangu wa kutongoza wanawake, nianze kugombania mwanamke mmoja aisee naona kama ni kazi ngumu kupita maelezo.
Kutongoza tuu mwanamke nahic kama ni tiresome process, sembuse kugombania.

Kwanza nikiona tuu mwanamke ana mtu mwingine interest yote inapotea, pia nikiona mwanamke niliyokuwa nae ana interest na wanaume wengine interest huondoka(hapa nazungumzia ku-reply message za wanaume ambao anajua kabisa wanamtaka), sasa nyie wanang mkoje????

Ningekuwa wewe baada ya kupata ushahidi wa usaliti, ningeenda kwake kiroho safi tuu, ningechukua vitu vyangu vyote, ningehakikisha na yeye hajaacha kitu kwangu, then ningekata mawasiliano, sio kum-block wala sio kutopokea simu zake, ni kukaa tuu kimya, simpigii na sijibu text zake, akipiga napokea namsikiliza, akituma message sijibu, akiniuliza shida nn namjibu "Niko sawa".

Najua inauma lakini if a woman doesn't want to be what you want her to be, don't force or cry about it, just move on, yes it's going to hurt but that's life, life is not supposed to be easy, especially when dealing with emotions, kuna muda ndio utam-miss na uta tamani umpigie lakini utakapo fanya hivo utashusha dhamani yako, wanaume tuelewe kwamba mwanamke aliyekusaliti ukamsamehe hatakuona una upendo au mvumilivu atakuona mpumbavu na huna uanaume kwasababu mwanaume wa kweli hasamei usaliti, unapomsamehe au kumchekea au kumkalia kimya mwanamke aliyekusaliti ni kama vile unamwambia "Mimi sio mwanaume" na hio kitu naona wanaume wengi wanafanya.

Mwanamke aliekusaliti ukaachana nae pamoja na yeye kuomba msamaha hata kutoa machozi yote atabaki anakuheshimu milele, lakini mwanamke aliyekusaliti na ukamsamehe atabaki anakudharau milele.
We tunafanana kwa mbali.
Kwamba ina maanisha nini kupendana na mwanamke na unaona hayupo tena kwenye frequency zako!
Napenda kujiweka pemben mapema.
Ili nimpe thaman ambaye anaongea lugha moja na mimi.
Sometimes hata kuachwa kuna raha yake!
Mtu pekee sijawai kumwelewa dunian ni ile anapigania penzi, anatumia nguvu mwili kudhibiti mambo ya moyoni!
Nijuavyo hakuna ushindi halisia kama kukubari kupoteza kinachoitwa penzi!
Mana penzi halisia lazima llijiendeshe!
 
Back
Top Bottom