Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Duh hii ni ya kibabe zaidi.....sie tunatumiaga mbinu ya kublock tu,unajua Mtu akigundua kapigwa block stimu zinamkata bila kujua aliyeblock sio mhusika,Sasa na muhisika nae Ili asiwashwe unaipindua number halafu unaicha vilevile alivyosave...hapo wataongea lugha kama ule mnara wa babeli
Mimi nafuta namba naweka yangu ila jina naliacha ili nione dhambi zake 😂😂😂
 
Mimi nafuta namba naweka yangu ila jina naliacha ili nione dhambi zake 😂😂😂
Waaaoooh!hii kiboko....ila hamna kitu naogopa kama kujua dhambi za mywangu maana zitanikata stimu huku bado namtaka😁😁😁
 
Let's go..............

Tukiwa tupo geto kwa Mercy ile jpili tukawa tunapitia pitia researches na baadae tukaanza kujisomea somea kwa disc.
Baada ya kuchoka basi tukawa tunapiga piga stors.
Niliamua kumuliza Mercy juu ya ile likizo fupi kwamba ataenda homa au atabaki, Mercy alinambia kwamba kwao wamekwambia aende wamemmiss lakini pia nayeye amewamiss.
Nilikubaliana naye nikasema haina shida yeye ataenda lakini mimi nitabaki maana kilikizo ni kifupi sana. Bado Mercy hakuweza kunambia chochote kuhusu Dokta na mimi pia niliamua kujikaza nisimsemeshe chochote kuhusu Dokta.

Nilimuaga Mercy nikarudi zangu geto, nipo njiani narud kwangu nikapokea cm ya Mercy fek akaniuliza nipo wapi nikamdanganya nipo kwa Mercy maana anaujinga wa kutokea mageto kwangu sometimes tena bila hata taarifa, alikuwa anapenda kuja kwangu hasa boom lilipokuwa likiisha ili aje kugongea vichenji vya msosi.
Akanambia anashida ya kuonana na mimi na ni very urgent, nikampuuza nikajisemea Hana lolote anataka kuniweka 18 nimle.

Basi nikampa ahadi kwamba wakati nitakapokuwa natoka kwa Mercy basi nitapita kwake ila sitaingia magetoni tutakutana nje.
Nikaona kuna haja ya kumsikiliza pengine atakuwa na jambo la maana. Nilifika mageton kwangu nikavunga kama nusu saa then nikamchek nikamwambia nipo njiani nakuja atoke nje maana kwake hapakuwa mbali sana na kwangu.
Nilivofika karibu na kwake nikamkuta nje, alikuwa kipens cha filla, chini open shoes na juu alivaa t-shirt na kikot cha jeans.
Tukasalimiana tena pale nikamuliza vipi kuna issue gani, akanambia kwamba anajua mimi ni mwanaume nina uwezo wa kupokea kitu chochote regardless uzito wake na nikakimudu.
Nikamwambia aendelee asiwe na shaka, Mercy fek hakuwa na muda wa kupoteza akaanza kufunguka akasema ndugu yangu kidem chako kinakusalit na Dokta. Hapa moyo ulilipuka lakini nilivokumbuka maneno yake kwamba mimi ni mwanaume inabid nikaze bas nikaona nikipanic ataniona mrembo.
Nikakaza nikamuliza unauhakika na umejuaje?

Akanijibu wewe niamini Mercy anakusalit na Dokta, nilimsihi sana athibitishe. Akanambia ukweli kwamba alitafuta namna nyingne ya kujikonekt na Dokta maana alipatwa na tamaa baada yakuona Dokta ni mwepes kutoa pesa. Alinambia kwamba alienda mpka hospital aka act kwamba anasumbuliwa na jino, na walikuwa wanachat mpka Whatsapp na Dokta akawa kashamtumia Mercy fek picha kwahyo ikawa rahisi kumfaham yule Dokta.

Akanambia alipokutana na Dokta pale hospital akamuomba namba na akaanza kuwasiliana naye kwa namba nyengine kabisa.

Aligunduaje Mercy wangu anawasiliana na Dokta ilikuwa hivi.

Mercy fek alipoanza mawasiliano na Dokta kama nilivowambia huyu ni malaya hivo haikuchukua muda akajiingiza mwenyewe kwenye laini. Anasema kuna siku walitoka out na Dokta na walipokuepo huko viwanja Dokta alikuwa anaenda sana toilet na cm alikuwa anaacha pale mezani kwahiyo Mercy fek alikuwa anachungulia chungulia. Sasa katika kuchungulia akaona mesej imeingia na namba ilikuwa haijaseviwa na namba ya Mercy anaijua akanambia Ile mesej alikuwa kaituma Mercy mesej ilisomeka "baby where are you now mbona kimya"".


Seeee you............

===
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
Manyoya 😂😂😂😂
Hii story why nilichelewa kuiona imenikumbusha mbali sana aiseee..!!
 
Back
Top Bottom