Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Tuendeleee..........

Nilienda town nikachukua viraba vya mazoez vya buku 8 haikuwa njumu kabisa ila ni raba nyepesi ambazo ni nzuri kwa kuchezea mpira kwa sisi ambao tulikuwa tunacheza kujifurahisha.
Siku ile ile nilianza kwenda chuoni kwaajili ya mazoez.

Baada ya tizi nikachukua baiki yangu kurudi magetoni njiani nilikuwa nakokota huku nikichat na Mercy na akanambia anaendelea vizur na safar na yalikuwa yamebak kama masaa mawili au matatu wafike. Siku ile nilichoka sana nikaamua kuoga then nikaenda kijiweni kula ili mambo yasiwe mengi.

Baada ya kula nipo zangu geto Mercy fek kanichek kaniuliza nipowapi nikamjibu home akasema anakuja kwani ana kitu cha kuongea na mimi.
Nikajiuliza huyu dem anataka nini ila nikasubr aje nimsikilize.

Hazikupita hata dakika mtu huyu hapa, kachoma ndani kanikuta kitandani naye akakaa pembeni yangu. Nikamkaribisha, nikamuliza nambie kuna mpya gani. Kaniuliza ni hatua gani nitachukua endapo atanithibitishia kwamba Mercy anatembea na Dokta nikamjibu mimi ni mwanaume na nishaanza kujifunza kuwa mvumilivu na kuhimili changamoto za mahusiano.

Mercy fek akatoa cm akafungua gallery akanionesha picha, alichukua cm ya Dokta akapiga picha chat za Dokta na Mercy. Chat zilikuwa zinaonesha Dokta alikuwa anamuliza kuhusu safar na kumtakia safar njema.
Mercy fek akanambia hakutaka kupiga zile texts mbya zaid za kiniumiza lakini it's true Mercy wangu alikuwa ananicheat silently.

Nilimkatisha asiendelee kuongea na nikavuta pumzi ndani kwa nguvu na kuitoa nje ili nitafute relief angalau. Mercy fek akaanza kama kuleta pigo za kutaka dudu ya yuyu nikamkata jicho elekezi na hapo alinielewa na akaahirisha mpango wake. Akavunga vunga pale anasikiliza mziki then akasepa zake nikabak alone. Siku ile pia nililia kisa Mercy, lakini mwisho wa siku nikaona hata nifanyaje wa kuokoa penz letu sio mimi hali ni Mercy kwahyo ikabidi nirelax tu nisiwe na makuu kwani hata kama ningegaagaa chini isingesaidia kitu.

Nikajikaza kitandani ghafla simu ikaita alikuwa Mercy,nikapokea kinyonge sana. Akanambia kafika nikampa pole basi nikamwambia apumzike ili aniache nilale zangu pia. Usiku ule ulikuwa mbaya sana maana niliandamwa na ndoto za kijingajinga sana nikaona dalili za kupata shida ya afya ya akili japo sikulitilia maanani sana hilo swala kwa muda ule.
Kesho yake niliamka nikafua fua pale, nikapika tea nikapiga.

Mercy alipiga cm tukaongea kwa muda kidogo nikajikuta naanza kuongea sana kumsihi Mercy asiruhusu mapenz yetu yavurugike. Mercy aliniuliza kwani kuna shida gani? Umeona nini mbona unanihubiria sana kuhusu kuwa muaminifu? Nikaona hili ni swali ya kizushi namimi nkampunch nkamwambia hakuna shida ila awe tu makini asije kuniharibia future yangu.

Asee pamoja na kuwahi kupitia katika mahusiano kadhaa kabla ya Mercy lakini nikiri wazi kwamba Mercy aliuteka sana moyo wangu na sikuwa na la kufanya ila hatma yangu ilikuwa mikononi mwa Mercy.

Siku zilienda likizo ikaisha na Mercy akawa anakuja siku hiyo yani anarud chuoni. Siku hiyo Mercy alinambia kwamba atachelewa kufika kwasababu gari imepata shida njiani kwahyo watafika usiku around saa tano, akanambia haina haja ya kwenda kumpokea kuna anko wake ataenda kumchukua stand na atalala kwake.

Mmmmh nikaona hapa tayari gari imekata break kwenye mteremko sitaweza kuikontrol labda niichome mtaroni.
Kiukweli sikuridhishwa na majibu ya Mercy nikamwambia hapana mimi nitakuja kuchukua nitakuja na bodaboda asiwaze wala kumsumbua anko wake.
Mercy kweli aliwahi kunambia ana anko wake pale mjini na siku moja moja alikuwa anaenda kuwasalimia.

Nilimganda sana Mercy mwisho wa siku akakubali niende kumpokea. Kwasabb alikuwa kanambia jina la gari hasi nikawaza niwahi mida ya saa4 niwepo around ili akishuka anikute pale. Ilipofika saa3 na dk45 nilimpigia boda tukasepa stand.

Cha kushangaza nilipofika stand nikakaa kama dk 20 ile gari ikaingia.
Mercy alivoshuka alistuka sana alivoniona akaniuliza umefika mda gani hapa? Dereva kakimbiza sana gar ndomana nimefika kabla ya muda nilokuelekeza.
Nikampokea sikutaka tuongee sana pale, tulipanda boda tukapotea. Njiani cm ya Mercy iliita kama mara tatu hivi na sms ziliingia kadhaa. Lakini sikutaka kumuuliza Mercy kuhusu hizo cm na sms.

Hii ndo ilikuwa siku rasmi Dokta alianza kuonesha ROHO mbaya mpaka ikapelekea kuandika Uzi huu na kuupa jina hilo.

See you............

===
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
Mapicha picha yako na kutojiamini ndio kumepelekea yote hayo…!!
Wanawake tukiona red flag nyingi kifuatacho ni kufanya cha kupooza moyo
 
Tuendeleee.......

Mercy aliendelea kunisumbua ili aje Tanga lakini namimi nikakaza sana na kumuomba Mungu nisiingie kwenye mitego yake tena.
Nilifanya kila mbinu ili kumkatisha tamaa Mercy asitishe kutaka kuja Tanga kuniona.
Nilipata wazo la kutafuta sababu ili tugombane kila mtu aendelee na mambo yake lakini mwisho wa siku anakaa kimya week weeks mbili ananitafuta tena.
Nisipojibu mesej wala kupokea cm zake anatumia namba nyengine kunitafuta.

Sasa mwezi wa tisa mwaka jana alinambia kwamba ananiona simpendi tena kwasababu tayar anamtoto. Akanambia yeye kuwa na mtoto ambaye siyo wangu siyo tatizo na kuna wanaume wengi ambao wanamtaka vilevile alivo na mtoto.

Alivonambia vile nikamjibu kwamba kama kapata wa kuolewa naye basi aolewe aachane namimi.
Hii kauli ni kama niliuchochea moto nilishushiwa ma sms mixer ma cm ya kutosha akilalamika kwamba simpend mpka namruhusu aolewe na wengine basi nikawa cmjibu na ilifika hatua nikawa sipokei tena sm zake.

Hakuchoka akawa anatumia namba mpya kunitafuta na kuendelea kulalamika mpk nikaanza kuwa nakwazika kutokana na malalamiko yake.

Sasa hapa mpka nabaki dilemma hivi mwanamke anaweza kupretend vyote hivi na bado akawa hakupendi?

Sio kwamba maumivu alonisababshia kipindi tupo chuo nimeyasahau hapana ila ananichanganya kwahiyo Nia na nguvu alokuja nayo kipindi hiki.


See you later.......
Sio kwamba anakupenda,hana kwa kwenda...isipokuwa kwako bwana mdogo,waelewe hawa raia

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Nikamuliza mimba ya nani, Mercy hakutaka kunidanganya alinambia kwamba mimba anahisi ni ya Dokta sio yangu.
Ufala sasa huu yani mwanamke nimeumia hivi, vipi kwa ww mwanaume?? We jinga sana nyie ndio mnapewaga na watoto sio wenu mfyuuuu!!!! Nimekupa na dislike umenikera kishenzy 😡😡😡
 
Tuendeleee.......

Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".

Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.

DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.

Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.

Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.

SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.

Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.

Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.

Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.

Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.

Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.

Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.

Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.

Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.

Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.

NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.

Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

AHSANTENI 🫶🫶🫶.
USIMUOE ACHANA NAYE, OYAA NIMEONGEA KWA CAPITAL LETTER UJUE NAMAANISHA UMENIUDHI MWISHONI HAPO 😏😏😏😏
 
Back
Top Bottom