SI KWELI Daktari aliyemkosoa Rais wa Burkina Faso kushindwa kushughulika na ugaidi apelekwa kukabiliana na ugaidi huo

SI KWELI Daktari aliyemkosoa Rais wa Burkina Faso kushindwa kushughulika na ugaidi apelekwa kukabiliana na ugaidi huo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu,

Habari hii imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba huyu Daktari baada ya kumkosoa Rais wa Burkina Faso Kpt. Ibrahim Traore kuhusu kushindwa kupambana na magaidi, alikamatwa, akavishwa magwanda kwenda kupambana na magaidi hao kwakuwa yeye analiweza suala hilo kuliko jeshi.

Hii taarifa ni ya kweli au tunapigwa kamba tu?

ameyakanyaga.jpg
 
Tunachokijua
Kapteni Ibrahim Traore ni Rais wa Sasa wa Burkina Faso. Rais huyu aliingia madarakani mnamo Septemba 30, 2022 baada ya kufanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Serikali iliyokuwa madarakani wakati huo.

Tangu kuingia madarakani Nchini Burkina Faso, yameibuka makundi mbalimbali pinzani ndani na nje ya yakipinga mambo mbalimbali katika Utawala wa Rais Ibrahim Traore.

Nchi nyingi zinapinga serikari ya Rais huyu hasa sababu ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi. Ndani ya nchi yake baadhi ya wadau wanapinga namna mambo mbalimbali yanavyoendeshwa ndani ya nchi hiyo ikiwamo namna Rais huyu anavyoongoza mapambano ya vikosi vyake dhidi ya magaidi.

Sakata Daktari Kumpinga Rais
Kumekuwapo picha mbili zinasambaa katika mitandao mbalimbali ikiripoti Daktari wa Burkina Faso aliyemkosoa Rais kuhusu anavyopambana na Ugaidi kupelekwa kwenye Jeshi la Ulinzi.

Picha ya kwanza inamuonesha mwanaume huyo akiwa ndani ya mavazi ya kidaktari huku nyingine akiwa katika mavazi ya kijeshi ameshika silaha kama ilivyoletwa na mleta mada hapo juu.

Mathalani Blogu ya Spectacle inaandika:

Mtaalamu wa Afya Daktari Ahmed Diallo alikuwa akikosoa kwa uwazi Rais Kapteni Ibrahim Traoré, akijiuliza uwezo wake wa kupambana kwa ufanisi na tishio linaloendelea la ugaidi ndani ya nchi.

Serikali ya nchi hiyo imemjibu kwa vitendo kwa kumpa mafunzo ya kijeshi Kisha kumfanya mtu anayesimama mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Ugaidi yanayoendelea
.

Nao, Nairaland hawatofaitiani na Blogu ya Spectacle ambao pia wanaandika:

Daktari wa matibabu wa Burkina Faso ambaye alikosoa Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, amepelekwa mstari wa mbele.

Daktari huyo aliikosoa vikali serikali ya Traoré kwa jinsi jeshi lilivyokuwa likishughulikia hali ya kutokuwa na usalama nchini, hivyo rais alimkamata na kumtia katika jeshi la ulinzi.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa usalama, Zagazola, Traoré alimpeleka daktari huyo mstari wa mbele ili aone kwa karibu ukweli wa ugaidi.


Ukweli wake upoje?
Baada ya kufuatilia suala hili kwa undani wake, JamiiForums imekosa ushahidi mahsusi kuthibitsha madai haya ambayo hayajaandikwa na chombo chochote cha kimataifa wala kutolewa kauli na mamlaka rasmi kutoka Burkina Faso.

Hata hivyo, ni muhimu kuufahamisha umma kuwa picha zinazooneshwa ni halisi, na daktari husika yupo. Isipokuwa sababu za kwenda vitani sio kama zinavyobainishwa mitandaoni.

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari na Mawasiliano wa nchi hiyo, Jean Emmanuel Ouédraogo, ni wajibu wa kila mwananchi wa Burkina Faso kuhakikisha kuwa nchi hiyo inakuwa salama, pia ni jambo la kujivunia kusimama mstari wa mbele kupigania dhidi ya magaidi.

Vyanzo vya kuaminika vinabainisha kuwa kama ilivyo kwa wananchi wengine walio mstari wa mbele kukabiliana na magaidi nchini humo, daktari huyu pia alijiunga na jeshi kama sehemu ya kuilinda nchi yake na sio kwa kuwa alimkosoa Rais.

Aidha, kuna tofauti kubwa ya majina ambapo baadhi ya vyanzo vinamtaja kama Daktari Ahmed Diallo huku vingine vikimtaja kama Daktari Arouna Loure.

Katika hatua nyingine, JamiiForums haijapata andiko, sauti au ujumbe wowote wa daktari huyu akiituhumu Serikali na Rais wa nchi hiyo kushindwa kushughulikia kikamilifu suala la magaidi.
Raisi anadili na watu wa mitandaoni ajui hata hadhi ya urais
Mtandaoni Sio Watu ?

Anyway angemchukua kama mshauri ili ashauri kile anachoona kimeshindikana ni vipi watakiweza au huenda kaende kumpa field / practical work ili aone mambo kwa uhalisia aje aongezee kwenye ushauri wake ni vipi watawaweza magaidi...

Anyway ni chizi pekee anyedhani magaidi wanaondolewa kwa mbavu badala ya education na uelewa kwa potential magaidi wa kesho ili wasiwe brainwashed leo.... (Ila kwa fikra duni za watu hata humu ndani naweza kuona watu ambao wanaweza wakawa magaidi kwa urahisi sana)
 
Ufaransa na America ndio magaidi al kaida na boko haram na isis hivi ni vyombo vyao katika mpango kuadhibu au kumiliki nchi.
 
Wakuu,

Habari hii imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba huyu Daktari baada ya kumkosoa Rais wa Burkina Faso Kpt. Ibrahim Traore kuhusu kushindwa kupambana na magaidi, alikamatwa, akavishwa magwanda kwenda kupambana na magaidi hao kwakuwa yeye analiweza suala hilo kuliko jeshi.

Hii taarifa ni ya kweli au tunapigwa kamba tu?

View attachment 2766292
Madikteta ndivyo yalivyo,hukumuona Mwendazake alivyo?
 
Afrika ndio tunashangilia kuongozwa na hawa wapumbavu na kuwaita eti ni wakombozi...kazi tunayo..😂😂😂

Ni mhuni tu kama wengine na atajimilikisha utajiri na familia yake hadi hapo watakapopinduliwa na wao,
Si mlikuwa mnamsifia? Nilishawaambia Jiwe like takataka hakuna Cha maana atafanya sana sana mtaambulia propaganda,vitisho na maigizo
 
Watawala wa kiafrika Sio wa kuwaamini sana labda kamvalisha tu magwanda ili kuwatisha wakosoaji
Kwa sentensi yako utaona kwamba tatizo ni wananchi..., karne hii hakuna watu wanaohitaji watawala popote pale.., kiongozi maybe ila mtu akishakuwa mtawala wewe mwananchi hauna haki wala say bali ni kufuata anachosema
 
Magaidi ni kama panyaroad au vibaka huwezi waondoa kwa mtutu maana magaidi Sio jeshi Wala hawana military base
 
Back
Top Bottom