Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Una point flani lakini ualimu pia nao unaadaraja....mwalimu anayemfundisha daktari naye huyo ni kama daktari tu anaweza kutibu...mwalimu anayemfundisha engineer nae ni engineer ma anaweza kudesign na kusimamia ujengwaji wa daraja. Ila mwalimu wa nursery, primary na secondary nao ni walimu lakini hawawezi kulipwa sawa na mwalimu wa daktari ama sawa na daktari mwenyewe ama mwalimu wa pilot ama pilot mwenyewe. Ila yeye (Mwalimu wa Nursery/primary &secondary) kulipwa sawa na polisi, afisa maendeleo, afisa utumishi, mwanasheria hapo sio sawa!!!
 
Kwani wewe umewahi kuwa engineeer.

Na kama wewe siyo engineer, unajuaje ugumu wa kazi ta engineer.
Mm sijasema kuwa uinjinia sio kazi ngumu popote pale....engineering is a very tough work...ninachokataa ni hii tabia ya injinia wa hapa bongo kuhisi udaktari sio kazi ngumu wakat wao wameshindwa kutengeneza hata sindano licha ya kuwa na elimu kubwa.....
Hebu angalia vifaa vyote almost vya tanesco vinatoka ulaya na China licha ya kuwa tuna a lot of ekectirical engineers wakutosha,barabara znajengwa na wachina na hilo tunaona kwa macho,kama huamin nenda hata hapo ubungo maji au mbezi pale utaona n kiasi gan wachina walivyodominate wakat civil engineers tunao sana,haya redio,TV,simu,computer vyote tunaagiza nje..how comes u become proud of our engineers?? What engine are they engineering?? Wao n kugovern vifaa tu walivyogundua wazungu tu,wao ni wa kutukanwa na wachina daily...I will never appreciate engineers of Tanzania unless I see their task.
 

Sio lazima niwe dokta kulijua hili tunalojadili hapa, hiyo 70% unayosema ndio ninayokwambia ni theory na kitabibu hairuhusiwi kumpa mtu dawa bila kumfanyia investigation - NI MAKOSA. Hizo dawa pia unazompa mgonjwa zimetengenezwa kiwandani ambako lazima Either Engineers, Engineering au Engineering concept ziwepo - NDIO MAANA NIKWAMBIA UDAKATARI WAKO HAUWEZI KUWA NA TIJA AU KUFANYIKA PASIPO UWEPO WA ENGINEERING AND ITS CONCEPTS.

Nilichokiona kwenye aya yako ya pili na tatu ni CHUKI YAKO KWA ENGINEERS sijui wamekufanya nini, lakini kwa suala la sijui Engineers wa kibongo hakuna wanachojua na blah blah nyingine, naomba nikwambie tu hata MADAKTARI wakibongo nao ni ZERO tu ndio maana vifo vingi vyakizembe vinatokea kutokana na uwezo mdogo wa matabibu, Mngekuwa mko smart pia sidhani watu kama wangeenda India, SA na Nairobi na wengine Ulaya. Pia fahamu ulichosomea kumdiagnostic binadamu hata Engineer pia amesomea kudiagnose machuma, Daktari anadeal na binadamu labda na wanyama that just the part wakati engineers wanadili na vyote vilivyomo duniani ndio wameingia huko kwenye udaktari wako na kukutengenezea vifaa na dawa, Niambia daktari yupo kwenye ujenzi wa barabara, daktari yupo kwenye ujenzi wa meli na ndege...
 
Mwalimu hana kazi kubwa kihivyo kuliko madaktari,labda walimu wa ngazi za chini wafikiliwe zaidi otherwise hao wa degree hiyo 20,000 kwa siku inamtosha sana na ana muda mwingi wa kufanya mambo yake
Mwalimu ana kazi kubwa kuliko daktari...!! Akitimiza majukumu yake kihalali..
 
Eng wa bongo buree kabisaa...[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kila mtu ni bora kwa nafasi yake...!! Yani hakuna aliebora wala mwenye Umuhimu mkubwa kuliko Mwingine.
 
Nikweli kwamba engineers wa bongo hawajagundua chochote kati ya ulivyosema, bali vimegunfuliwa nje?

Lakin hebu nikuulize swali, umewahi kusikia kiongozi, au mtu tajiri wa tanzania anaenda kutibiwa Muhimbili na analazwa hapo hapo? Au umewahi kusikia amefia kwenye hospitali zetu hizi hizi?



Maoni yangu mimi ni kwamba, wote wanafanya kazi kubwa sana, na kila mmoja ana umuhimu wake, daktari unafanya kazi kubwa sana na unatumia akili nyingi, lakini pia engineer anafanya kazi kubwa na anatumia akili nyingi pia.

Kwa hiyo, TUHESHIMIANE
 
Umeongea vizuri sana !
 
umeandika uharo hapo. Bila waalimu kusingekuwa na madaktari wala ma injinia. Tetea madaktari bila kuwa undermine walimu. Kazi nyepesi kukaa na watoto? Hujui ukiharibu kwenye msingi ndo umeharibu taifa zima? pumbavu kabisaa
 
Ni kweli kabisa, ila sasa unapofanya kazi ya ndoto zako usianze kulalamika kwamba kwanini wanaofanya kazi zingine wanalipwa mshahara mkubwa zaidi yako ( ambao kwa mtazamo wako ulipaswa kuwazidi mashahara) .
Mtu anafanya amachopenda ndio ndoto yake
 
Ulinganifu mbovu. Daktari wa halmashauri analinganishwaje na Engineer wa Taasisi. Hizo sehemu mbili zina scale tofauti za mishahara. Labda ungeangalia Daktari aliyeajiriwa Tanroads analipwaje. Ila sasa Tanroads inahitaji mainjinia zaidi kuliko madaktari. Na taasisi nyingi huwa zinahitaji madaktari wachache. Madaktari wengi wanabaki kuajiriwa na halmashauri. Ulinganifu sahihi ungekuwa kulingalisha mhandisi wa halmashauri na daktari wa halmashauri. Lakini ukianza kulinganisha halmashauri na Tanroads, tayari kuna tofauti ya mishahara sio tu kwa madaktari na mainjinia bali kwa wafanyakazi wa sehemu hizo mbili. Mfanyakazi yoyote wa Tanroads analipwa zaidi ya wa halmashauri. Hoja yako umeshindwa kuijenga vizuri sababu umetumia ulinganifu ambao si sahihi. Ni kweli madaktari wanapaswa kulipwa vizuri. Na pia hata walimu nao wanapaswa kulipwa vizuri. Wafanyakazi wa sekta ya afya ni wengi zaidi ya wahandisi. Tunahitaji uchumi mzuri kuwaboreshea wote maslahi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…