Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Je..mnamjua mtu anaitwa pharmaceutical engineer?Jielimisheni jamani
Bro embu kuwa na elimu na kitu ndio uongee.
Dawa ya graseofulvin na engineer wapi na wapi?!
Anaetufanya sisi tufanye kaz mfamasia sio engineer.
Duuuh baba uinjinia na madawa wapi na wapi.!?
 
Je..mnamjua mtu anaitwa pharmaceutical engineer?Jielimisheni jamani
Achana nao sijui wanafikiria kwa kutumia nini,,waambie hakuna kiwanda cha kutengeneza dawa na vifaa tiba duniani hapa ambacho hakina Engineer
 

Hapo kwenye red nifafanulie ni kwa namna gani mnaweza kugundua ugonjwa wa mtu kwa kutumia prescribing

Je prescribing ni nini ndugu tabibu?
 
Sema hawa mainjinia waudsm hawajagundua wala hata kuweza kutengeneza hata kimoja ya ulivyovitaja....wapowapo tu kama viazi
 
Sio kweli.Huo ualimu mnaoudharau hauna ajira kwa sasa.
 
Kwa vifaa tiba kweli ma engineer ila madawa waachie mafamasia mkuu maana madawa yana uwanda mpana mkuu
Achana nao sijui wanafikiria kwa kutumia nini,,waambie hakuna kiwanda cha kutengeneza dawa na vifaa tiba duniani hapa ambacho hakina Engineer
 
Prescription ni kule kupata maelezo juu ya ugonjwa wa mtu kwa kumuhoji anavyojisikia na kwa kumfanyia test wewe mwenyewe either kwa kumtizama temperature yake kwa thermometer ama kwa kuchunguza heart beat zake kwa stethoscope na kuoanisha dalili za yule mgonjwa na magonjwa stahiki.
Mfano wewe umekuja hospital.
Unalalamika ukikojoa unakojoa mkojo wa damu na kibofu kinauma sanaa.
Dalili hii inafanania na magonjwa mawili ya Urinary tract infections pamoja na magonjwa ya zinaa asa mm nitakua nishagundua tatizo lako.
Nitakupa antibiotics ya ampiclox+clavulate ili kuua UTI ikiwemo na nitakuandikia Fluconazole vidonge kumi tyuu vikaue vimelea vya magonjwa ya zinaa.
Hapo nimekugundua kwa prescription.
Wala sikuhitaji uende maabara.
Ila hvyo vifaa vinatumika kuturahisishia kaz na kutuletea uhakika wa tunachokifanya mkuu.
Mm nilipokuwa nachoka kazin mtu akija kulalamika kuhusu magonjwa yake ofisini namuhoji natake history then namwandikia dawa anapitia pharmacy ya palepale kituo chetu cha afya kaZ inaisha
Hapo kwenye red nifafanulie ni kwa namna gani mnaweza kugundua ugonjwa wa mtu kwa kutumia prescribing

Je prescribing ni nini ndugu tabibu?
 
ameandika fasta ile 6 ikageukia juu
 
Madaktari na wahandisi wabongo ni garbage , mnapasua watu vichwa badala ya miguu na wahandisi mnalipua miradi kila siku , hovyo kabisa . Tena mlifaa mlipwe 20000 kwa mwezi pambafu nyie
Haaa kuna mmja kamng'oa mgonjwa meno mazima kaacha mabovu jamaa yuko as dish limeyumba,madokta bana
 
Irrelevant comparison:
Daktari North Mara gold mine anakunja 4M
Hapo unasemaje???
Hao Madaktari waende tu TANROAD wafanye kazi. Kasema Daktari anakula 1,500,000.00. Nimjulishe tu Mhandisi Daraja la I wizarani au halmashauri anakula 900+. Bakharesa hajasoma kabisa anakula bilions, hauna haja ya kuanghaika na bahati za wenzako.
 
You have hinted the point. Wengine interest ilikuwa kuona uchi wa watu tuu
 

Kwani formula ya kupanga mshahara kwa mujibu wa uchumi zipoje?
 
Hao Madaktari waende tu TANROAD wafanye kazi. Kasema Daktari anakula 1,500,000.00. Nimjulishe tu Mhandisi Daraja la I wizarani au halmashauri anakula 900+. Bakharesa hajasoma kabisa anakula bilions, hauna haja ya kuanghaika na bahati za wenzako.
Bakharesa hajasoma lakin kaajiri wasomi. Hivi kweli hajajiendeleza kweli kielimu au kuhudhuria course fupi fupi?
 
Ni wivu tu, Ni wivu tu na Ni wivu tu...nenda kasome engineering
 
Mshahara mkubwa hauondoi rushwa Mkuu wangu. Ni commitment.
 
Mkuu hiyo dhana imepitwa na wakati zama hizi
nenda kaajiriwe wanakolipwa zaidi, kama umeajiriwa na serikali na umeridhika usiangalie wengine wanacholipwa utaumia sana, nilifundishwa na mzazi wangu ukiona kazi haikufai au masilahi kidogo andika barua ya kuacha kazi, wanaoweza watafanya na wewe utatafuta unayoitaka na yenye mshahara unaoutaka. Kamwe usijifananishe na kazi ya mtu mwingine! HAMNA ALIYEKULAZIMISHA USOMEE UDAKTARI
 
Ni kweli serikali inatakiwa kupitia upya viwango vya mishahara kwa watumishi wake hasa kwa kuzingatia mazingira anayokutana nayo huyu mfanyakazi. Mishahara iliyonona kidogo inasaidia kumpa mtumishi morali na nguvu ya kukataa rushwa, maana hata kama mtu ni mzalendo lakini kila siku anakutana na vishawishi vikubwa kila siku kwa kazi yake na akiangalia mshahara wake dah..mtakuja mfungulia kesi za rushwa na kumuona sio mzalendo kumbe wasababishi ni serikali wenyewe.

Mwanasheria wa Serikali analipwa gross TZS 969,000/= (amesoma miaka 4 chuoni pamoja na mwaka 1 wa mafunzo pale shule ya sheria Tanzania). Huyu mwanasheria anatetea serikali kwenye kesi zote za madai, ambapo serikali kulingana na uhaba wa fedha pamoja na uzembe tu wa viongozi wa taasisi wakati mwingine, haikaukiwi kesi, kila siku watu wanaishtaki (wakandarasi na wazabuni mbalimbali). Sasa mtu anaoambana kuokoa mabilioni yasilipwe (hata madai ya halali) halafu ndio take home yake hiyo 900, hapo anatakiwa kuvaa suti kila anapoingia mahakamani (ndio sababu ya wengi kuvaa makoti yaliyopauka sana), halafu bado tunajiuliza ni kwa nini serikali inashindwa katika kesi zake nyingi..mazingira haya huyu mtu hata akinunuliwa suti 2 mpya na viatu, anachomokaje (ni mfano tu). Opponent advocate kwa kesi hiyohiyo unakuta kala retianer 30m..

Serikali irekebishe haya, ama sivyo kila siku kwenye hotuba tutaendelea kuulizana kwa nini serikali inashindwa kwenye kesi zake. Unamlipa mwanasheria hiyo 900 wakati Ubalozi wa US wanatangaza kazi ya karani mtanzania mwenye elimu ya kidato cha 4 mshahara wake ni 1.2m kwa mwezi
 
Hahahaha hii kichekesho cha mwaka , jiulize kwann waalimu WA arts ni wengi kuliko waalimu WA sayansi
Hawa wingi wao ulichangiwa na upatikanaji wa mkopo wa masomo wa serikali. Wengi walisoma ualimu ili tu wapate mkopo, ilikuwa ni moja ya kozi zenye vipaumbele, ikumbukwe zamani miaka ya 2000 mwanzoni nayo ilikuwa ni kozi ya miaka 4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…