Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Udaktari tiba ni fani nyeti na ngumu sana lakini cha kushangaza daktari anapata salary ya Tsh.1,500,000 gloss hukuhandisi wa Civil pale TANROADS(case study) anapata 2,000,000
Clinical officer/tabibu =950,000 huku Civil Technician=1,118,000 per month

Kwa staili hii case za rushwa zitaisha huko hospitali na vituo vya afya?

Tafadhali serikali wapeni madaktari uzito unaostahili kwenye malipo,wanatumia kusoma na wanaumia kazini.

Hata kwenye stahiki za posho na benefits zingine daktari hamfikii mhandisi lakini pia mhandisi hasa wa civil wako kwenye industry ambayo possibility ya yeye kupata pesa ni kubwa kuliko watu wa afya hadi semina zije.

Chonde chonde serikali mnapopanga viwango mliangalie hili na ule mpango wa kuwianisha malipo ya wafanyakazi walio na elimu moja limeishia wapi?

Leta mshahara wa mhandisi wa Halmashauri ulinganishe na dakatari wa hospitali ya wilaya au mkoa. TANROAD ni kama mashirika mengine ya UMMA kama NSSF, NHIF nk
 
Hawajapewa nafasi ya kufanya hvyo.
Mbona wakipewa nafasi hata wanafunzi tu Wana uwezo wa kutatua hizo changamoto.
[emoji23][emoji23][emoji23]Wapo wewe...!! Ushawahi toa proposal wizara ya husika likakataliw??
 
Unasomea fani unayoipenda si mshahara
Hivi bila kulipwa stahiki zako vizuri maisha utayaendeshaje ilihali fani uliyosema hata kama umeichagua mwenyewe lakini sio fani rahisi pia madaktari wanaheshimika sana mataifa mengine ila hapa Tanzania ni fani ya ovyo sana, msipende kuchukuli mambo kama yalivyo au kikawaida kuna wakati mtu unatakiwa kuhoji kwanini hivi na sio vile
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Wapo wewe...!! Ushawahi toa proposal wizara ya husika likakataliw??
No inabidi watangaze tenda ili watu waje na proposal.
Huwez kwenda mwenyewe tu bila kutangazwa hyo itakuwa ni kujipendekeza na watakusumbua hadi kiatu kitaisha soli.
 
No inabidi watangaze tenda ili watu waje na proposal.
Huwez kwenda mwenyewe tu bila kutangazwa hyo itakuwa ni kujipendekeza na watakusumbua hadi kiatu kitaisha soli.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tatizo wengi wenu wezii wakubwaaa
 
Nnachokiongea nna uhakika nacho mkuu,sijakurupuka.

Clinical Officer II anaanza na TGHS B ambayo ni 680,000/=
Clinical Assistant II anaanza na TGHS A ambayo inacheza kwenye 450,000/=
Assistant Medical Officer (AMO) ipo kwenye TGHS C ndiyo hyo 980,000/=
Duu haya majanga,nurse mwenye diploma anaanza na ngapi sasa?
Huyo AMO elimu yake inakuaje?
 
Sawa mkuu kwa mm namtoa MD nataka c.o ndio ashughulikiwe maana MD wanakula bata nao vile vile.
Ila nimekuelewa mkuu.
MD akishapata mishahara ya hospital mbili akiikutanisha kaka kasha win hapo wa kuangaliwa C.o maana wanamtumikisha 24 hours mshahara mbuzi.
Kwa mimi navyoona mkuu labda kama nimetereza nielimishe. Maana ukutanishe million 1.5 ya Mnazi mmoja na ya Hindumandal million 3 tayar mkuu huoni kuwin tayar hapo?!
Kama fikra zangu duni mkuu nipambanulie zaidi
Sidhani kama kuna upungufu wa madaktari wa kawaida mtaani hadi mtu atumike sehemu zaidi ya moja,kwa madaktari bingwa hakuna shaka kwa hilo
Serikali iwalipe madaktari salary inayoridhisha
 
Duu haya majanga,nurse mwenye diploma anaanza na ngapi sasa?
Huyo AMO elimu yake inakuaje?
Katika kada ya afya, ngazi ya mshahara inakuwa flat kwa Diploma na Certificate. Tofauti inapatikana kuanzia Bachelor.
 
Yale mabati yamewekwa kwa maelekezo ya hao ma eng wa bongo unaowaita takataka. Mchina kazi yake ni kujenga tu.
Eng wa bongo taka takaa tu... Yani mchina kaja Kaweka tu mabati pale Ubungo foleni kwisha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Maeng wetu hakuna kitu ni mzigo tu kwa taifa..!
 
Back
Top Bottom