Daktari anayedaiwa kumpiga trafiki aachiwa kwa dhamana

Daktari anayedaiwa kumpiga trafiki aachiwa kwa dhamana

Mkuu Ikishakuwa jinai siku zote mshtaki ni Jamhuri kupitia mwendesha mashtaka.
Itakuwa jinai kama dkt. atashtakiwa kwa kumzuia askari akitekeleza majukumu yake. Na hili hao jamaa watalipenda zaidi ili kumkomoa dkt.
Lakini mm naona itakuwa ni ya madai kwani walitwangana ktk. mazingira tatanishi e.g. kwani ni kazi ya askari kukusanya ushuru?
 
Kwani chargesheet imesomekaje mkuu.
Na itakuwaje madai kabla haijathibitika mkosaji ni nani?

Btw: iwe ni shambulio la kudhuru mwili au kumzuia askari kutekeleza majukumu yake yote ni mashtaka yanayoangukia kwenye kundi la jinai.
 
Kwani chargesheet imesomekaje mkuu.
Sijaiona.
Na itakuwaje madai kabla haijathibitika mkosaji ni nani?
Hii watasema Mahakama na sio Polisi. Polisi ni waongo mno na wanajua sana kufremu tukio ili ionekane mkosaji ni Dakt.
Btw: iwe ni shambulio la kudhuru mwili au kumzuia askari kutekeleza majukumu yake yote ni mashtaka yanayoangukia kwenye kundi la jinai.
OK.
 
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, Conrad Kahyoza ameachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka moja la kushambulia mwili.

Kahyoza anadaiwa kumshambulia askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, F.8886 SGT Andrew, Septemba 8, 2026, majira ya saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, eneo la Makongo, wakati askari huyo akiwa akitekeleza majukumu yake.

Soma: Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani, 10/09/2026

Akisoma hati ya mashtaka, Leo Septemba 102026 mwendesha mashtaka wa Serikali, Irene John, amesema mtuhumiwa huyo anashtakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 243(d) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 16, kama kilivyofanyiwa marekebisho.

Baada ya kusomewa shtaka hilo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Jacqueline Rugemalila, Dk Kahyoza alikana kutenda kosa hilo.
Kipindi cha Ulimboka kuna kamanda aliugua akajipeleka hospitali binafsi kukwepa kulipizwa na timu Ulimboka, huko hospitali binafsi wakasema tiba kamili iko kule waliko mashabiki wakubwa wa Ulimboka na akalengeshewa huko, alipofikishwa huko badala ya kueleza shida yake ya kiafya akaanza kujitetea kuwa yeye siye aliye muumiza ulimboka!
 
Back
Top Bottom