Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Daktari wa Dental Clinic iliyoko Sinza Mori, Dr Awadh Juma mkazi wa Kunduchi ambaye anatuhumiwa kwa utoaji mimba ambao ni kinyume cha sheria za nchi , amefikishwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akishitakiwa kwa makosa 7 likiwemo la utakatishaji wa kitita kikubwa cha pesa za kitanzania cha shilingi 260,000 ( laki mbili na elfu sitini)
Pamoja naye ameshitakiwa pia muuguzi wa clinic hiyo aitwaye Kidawa Ramadhan ambaye ni mkazi wa Manzese.
Kesi hiyo iko mbele ya Mh Hakimu Vicky Mwaikambo, ambapo mashtaka yamesomwa na Wakili wa serikali Simon Wankyo akisaidiwa na Glory Mwenda .