Daktari FEKI akamatwa Muhimbili

Daktari FEKI akamatwa Muhimbili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
gvgvghv.JPG


Mkazi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akijihusisha kutapeli wananchi wanaopata huduma kwa kujifanya daktari.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi Bw. Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini daktari huyo feki akiwa kwenye harakati za kuwatapeli wananchi wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bw. Aminiel Aligaesha ametoa rai kwa watu wote wanaojihusisha na kutapeli wananchi katika eneo la Hospitali kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama
 
Ajira hakuna wacha watu wajiongeze.
Nanyi raia kuweni makini katika kila ofisi matapeli ni wengi sana.
 
Hadi mochwari kuna utapeli, unazungushwa kumpata ndugu yako. Mara ufunguliwe kule mara huku
 
Mfumo wakupata huduma ukibireshwa, rushwa kudhubitiwa kikwelikweli, haya mambo hatutayasikia. Tuboreshe utohaji huduma mambo mengine yatakaa kwenye mstali yenyewe
 
Ndo anamwaga (mke na watoto) nyumbani asubuhi anasema anaenda kazini
Na amekuwa akirudi na chakula+mahitaji ya home kila uchaoo DUHH
mara paaa mama + watoto wanaona picha baba amekamatwa kwa uzururajii (Dr feki)
 
Back
Top Bottom