Daktari: Kama una Kilo kuanzia 80 na kuendelea unatakiwa kuwekewa Puto la Kupunguza Uzito

Daktari: Kama una Kilo kuanzia 80 na kuendelea unatakiwa kuwekewa Puto la Kupunguza Uzito

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Madaktari Bingwa Dr. Eliasa Mkongo , Dr. Edwin Muhondezi. pamoja na Dr. Eric Muhumba (Surgeon) ambao ni Madaktari Bingwa wazawa Wakizungumzia Namna Uwekaji Puto Ndani Ya Tumbo unavtofanyika, watu gani wapaswa kuwekewa na Faida na Hasara Zake.
 
Sidhani kama gharama yake kila mtu anaweza kumudu, hivi ni sh ngapi?
 
Fanyeni mazoezi

Kg 80 zinakatika vizuri tu

Acheni uvivu

Mistake kuliwa pesa zenu kizembe

Ova
Halafu siyo kweli kuwa kilo 80 ni madhara kwa kila mtu!! Inategemea huyo mtu:
1. Ana urefu gani
2. Je hufanya mazoezi?

Kilo 80 kwa mtu mwenye urefu wa zaidi ya cm 180 wala si tatizo kwake! Pia kilo 80 kwa mtu mwenye mazoezi ya kutosha pia si tatizo kabisa kwake!!
Jueni pia kuwa kazi ya mazoezi siyo kupunguza uzito, bali ni kukuwezesha kuumudu na kuubeba uzito wako bila kulemewa! Mazoezi yanakujengea misuli itakayokupa nguvu ya kumudu kuubeba uzito wako!! Ila mazoezi yanaenda na lishe bora ili yakupe matokeo bora yaliyokusudiwa!! Usishangae ukifanya mazoezi halafu badala ya uzito kupungua kinyume chake uzito unaongezeka kiasi fulani lakini bado utajisikia ni mwepesi!! Maana unaumudu vizuri uzito wako!! Msitishwe na hao wafanyabiashara wa maputo, wanachofanya ni kuganga njaa tu!!
 
Mtu anatakiwa ajishtukie tu, kitambi hakina faida, unene hauna faida
Kuwa na uzito mkubwa haina maana uwe na kitambi!! Kitambi si afya lakini uzito mkubwa si mara zote ni kiashiria cha afya mgogoro. Inategemea na urefu wa mtu na mazoezi ya mtu pia. Si kila mtu mzito ana kitambi na si kila mtu mwenye uzito kidogo hana kitambi!! Ipate hiyo!!
 
Halafu siyo kweli kuwa kilo 80 ni madhara kwa kila mtu!! Inategemea huyo mtu:
1. Ana urefu gani
2. Je hufanya mazoezi?

Kilo 80 kwa mtu mwenye urefu wa zaidi ya cm 180 wala si tatizo kwake! Pia kilo 80 kwa mtu mwenye mazoezi ya kutosha pia si tatizo kabisa kwake!!
Jueni pia kuwa kazi ya mazoezi siyo kupunguza uzito, bali ni kukuwezesha kuumudu na kuubeba uzito wako bila kulemewa! Mazoezi yanakujengea misuli itakayokupa nguvu ya kumudu kuubeba uzito wako!! Ila mazoezi yanaenda na lishe bora ili yakupe matokeo bora yaliyokusudiwa!! Usishangae ukifanya mazoezi halafu badala ya uzito kupungua kinyume chake uzito unaongezeka kiasi fulani lakini bado utajisikia ni mwepesi!! Maana unaumudu vizuri uzito wako!! Msitishwe na hao wafanyabiashara wa maputo, wanachofanya ni kuganga njaa tu!!
Umeongea sahihi ..kuna uwiano kati ya urefu/ kimo na uzito wa mwili ambao unapimwa kwa kipimo kiitwacho BMI
 
Piga zako mbio za kutosha kitambi utakiona Kwa wenzio wapenda Kula tu mazoezi hawataki
 
MBOWE ANATOFAUTIANA NA MAKAMU WAKE (LISU) HADHARANI, HII HAINA AFYA, wamalizane chemba tafadhari.
 
Unawekewa puto alafu unakufa kwa Corona. BTW aneongea na Mama??
 
Back
Top Bottom