Daktari kesi ya Afande Rama asema baada ya vipimo amebaini kuna uwazi sehemu za siri za nyuma za mshtakiwa

Daktari kesi ya Afande Rama asema baada ya vipimo amebaini kuna uwazi sehemu za siri za nyuma za mshtakiwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Shahidi namba moja Dkt. Fahad Nassor Mohammed katika kesi namba 59 ya Mwaka 2023, inayomkabili Mshtakiwa Ramadhan Hassan Ali ambaye anashtakiwa kutenda makosa mawili ikiwemo kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na kosa la pili la maudhui ya king’ono ametoa ushahidi wake mbele ya Mahakama ya Mkoa Vuga, Mjini Unguja.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Vuga, Khamis Ali Simai amesema baada ya kumfanyia mtuhumiwa uchunguzi alibaini kuwepo kwa uwazi katika sehemu za siri za nyuma zenye uwezo wa kupitisha vidole viwili jambo linaloashiria kuingizwa kitu kigumu kutoka nje.

Shahidi wa Pili katika kesi hiyo Sajenti wa Polisi, Ame Suleiman Ame amethibitisha mbele ya Mahakama kuwa yeye ndie aliyempiga picha mshtakiwa Ramadhani Hassan baada ya kukamatwa na Polisi kwa kutuhumiwa kutenda kosa na picha hizo kutumika kama kielelezo cha kumtambua mshtakiwa wa kesi hiyo.

Kwa upande wa Wakili wa Utetezi, Hassan Kijogoo aliibua maswali kwa mashahidi wote wawili akitaka kufahamu kabla ya uchunguzi huo wa kitabibu kufanyika ridhaa ilipatikana kutoka kwa mhusika na kumtaka shahidi athibitishe kielelezo cha ridhaa hiyo.

Shahidi alisema alipata ridhaa ya kauli kutoka kwa mshtakiwa Ramadhani.

Hata hivyo, Wakili kutoka Ofisi ya Muendesha wa Mashtaka wa Serikali, Mohammed Saleh ameiomba Mahakama kuzuia vielelezo vya ushahidi mwengine wa video ukionyesha tendo likifanyika ili kuheshimu mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kesi hiyo imeharishwa hadi tarehe 17 Aprili, 2023 huku mshtakiwa akiendelea kuwa rumande.

Chanzo: Wasafi TV
 
Naona maswali muhimu sana ambayo sina hakika kama yameulizwa ni;

1. Shihidi aieleze Mahakama kama yeye ni mtaalamu wa mfumo wa chakula wa mwanadamu na kama ametoa ushahidi kuthibitisha hilo

2. Shahid, upo uwezekano wa puru/m.kundu wa mwanadamu kuwa wazi kutokana.na maradhi kama bawasiri?

3. Shahidi mlimpima mshtakiwa kama anaugonjwa wa bawasiri?

4. Shahidi, ieleze Mahakama bawasiri zipo ya aina ngapi na huwa inaathiri sehemu gani ya mwili wa mwanadamu

5. Je, upo uwezekano mtuhumiwa kuwa na ugonjwa wa bawasiri

6. Shahidi kama mtaalamu wa afya je, wapo watu wanaozaliwa na uwazi kama alionao mtuhumiwa?

7. Je, na wao wameupata kwa kuingiliwa na vitu vigumu kwa nje?

8. Vitu vigumu unavyovitaja ni vitu gani hivyo, shahidi?

Alafu inavutwa pumzi maana maswali yanayofuata yataharibu swaumu za waja.

Uwazi sio hitimisho kuwa mtu analiwa tako.
 
Back
Top Bottom