Daktari kesi ya Afande Rama asema baada ya vipimo amebaini kuna uwazi sehemu za siri za nyuma za mshtakiwa

Daktari kesi ya Afande Rama asema baada ya vipimo amebaini kuna uwazi sehemu za siri za nyuma za mshtakiwa

Shahidi namba moja Dkt. Fahad Nassor Mohammed katika kesi namba 59 ya Mwaka 2023, inayomkabili Mshtakiwa Ramadhan Hassan Ali ambaye anashtakiwa kutenda makosa mawili ikiwemo kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na kosa la pili la maudhui ya king’ono ametoa ushahidi wake mbele ya Mahakama ya Mkoa Vuga, Mjini Unguja.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Vuga, Khamis Ali Simai amesema baada ya kumfanyia mtuhumiwa uchunguzi alibaini kuwepo kwa uwazi katika sehemu za siri za nyuma zenye uwezo wa kupitisha vidole viwili jambo linaloashiria kuingizwa kitu kigumu kutoka nje.

Shahidi wa Pili katika kesi hiyo Sajenti wa Polisi, Ame Suleiman Ame amethibitisha mbele ya Mahakama kuwa yeye ndie aliyempiga picha mshtakiwa Ramadhani Hassan baada ya kukamatwa na Polisi kwa kutuhumiwa kutenda kosa na picha hizo kutumika kama kielelezo cha kumtambua mshtakiwa wa kesi hiyo.

Kwa upande wa Wakili wa Utetezi, Hassan Kijogoo aliibua maswali kwa mashahidi wote wawili akitaka kufahamu kabla ya uchunguzi huo wa kitabibu kufanyika ridhaa ilipatikana kutoka kwa mhusika na kumtaka shahidi athibitishe kielelezo cha ridhaa hiyo.

Shahidi alisema alipata ridhaa ya kauli kutoka kwa mshtakiwa Ramadhani.

Hata hivyo, Wakili kutoka Ofisi ya Muendesha wa Mashtaka wa Serikali, Mohammed Saleh ameiomba Mahakama kuzuia vielelezo vya ushahidi mwengine wa video ukionyesha tendo likifanyika ili kuheshimu mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kesi hiyo imeharishwa hadi tarehe 17 Aprili, 2023 huku mshtakiwa akiendelea kuwa rumande.

Chanzo: Wasafi TV
Hiki kipimo cha kuingizwa vidole viwili kamwe siyo kipimo himilivu.
 
Hizi kesi unafanya uchunguzi wa nn wakati videos zinaonesha kabisa jamaa analilia mkunyenge. Huyu kupigwa shaba hadharan tu wenzake wajifunze
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] acha sheria ifuate mkondo wake.
 
Naona maswali muhimu sana ambayo sina hakika kama yameulizwa ni;

1. Shihidi aieleze Mahakama kama yeye ni mtaalamu wa mfumo wa chakula wa mwanadamu na kama ametoa ushahidi
Kwa kweli, yaan natamani hii case mie wakili wa utetezi wa afande Rama, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mbna mahakama ingefurahiii.
 
Mnahangaika na mambo ya kipuuzi si kaamua mwenyewe.
Mpeni adhabu basi sasa kumtia vidole tena nyuma viwili ndo nini?
Ni yaleyale tena
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wanamtekenyaaa na ndoleee.
 
Afande rama shikilia hapo hapo, hii case ndogo kwakoo, kwanza hadi hapa hii ni irrelevant case,

Ushahidi wa kuingiliwa kinyume na maumbile ni sperms, yaan shahawa sasa km hajakutwa nazo, case inaendelea vipi???

Afande rama aachiwe huru. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]watu weuweeeeer
 
Back
Top Bottom