Daktari: Mirembe kuna Wagonjwa wengi Wanaume kuliko Wanawake

Daktari: Mirembe kuna Wagonjwa wengi Wanaume kuliko Wanawake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FeuLuJRX0AUpwXs.png

Imeelezwa Hospitali ya Mirembe ambayo ni Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Afya ya Akili iliyopo Dodoma kitakwimu ina idadi kubwa ya wagonjwa wa aina hiyo Wanaume kuliko Wanawake.

Bila kubainisha namba, Daktari wa Mirembe, Veronica Lyimo amesema takwimu za umri zinaonesha wanapokea zaidi vijana kuanzia wenye umri wa miaka 20 hadi 45.

Amesema “Kuna wagonjwa wenye umri wa miaka 50 hadi 70 lakini ni wachache sana, pia kwa siku tunaona wagonjwa kuanzia 150 hadi 250 na kati ya hao 30 hadi 70 unakuta wana shida ya akili."

Ameongeza kuwa vyanzo vya magonjwa ya akili vipo vingi lakini mambo makubwa matatu inaweza kuwa Kibaiolojia, Kijamii na Kisaiokolojia.

Amesema wengi hawajui inakuwaje hadi mtu anapata changamoto hizo, akifafanua amesema

Kibaiolojia ni kama vile kurithi au pindi mtu anapopata matatizo ya kawaida ya magonjwa ya ndani ya mwili mfano presha kifafa au VVU.

Kisaikolojia inaweza kutokana na malezi, mtoto kukua akilelewa na mzazi mmoja, kutengana kwa wazazi, maisha kuwa magumu, kufiwa au kuondokewa na mtu wa karibu.

Kijamii ni kama vile changamoto za kiuchumi, maisha kuwa magumu, mfano maisha ya ndoa, Mwanaume au mwanamke anaweza kupata shida ya ndoa.

Kuhusu kufanyiwa vipimo anasema mtu yeyote anayehitaji kufanyiwa vipimo muhimu huwa wanafanyia vipimo vya Magonjwa ya Sonona, wasiwasi, matumizi ya pombe na matumizi ya dawa mbalimbali za kulevya.

Chanzo: EATV
 
Back
Top Bottom